Na Wewe Unapinga Mabadiliko.....? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Na Wewe Unapinga Mabadiliko.....?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtoboasiri, May 30, 2011.

 1. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Wajameni,

  Nimesoma "article" moja hivi karibuni ambayo mwandishi wake anasema watu wengi hatuendelei kwa kuwa tunang'ang'ania hali zetu za zamani. Anatoa mifano ya watu kupaka rangi nywele ili kuficha mvi, kunyoa nywele zote ili kuficha kipara, "plastic surgery" kuficha ngozi ya uzee n.k., n.k, n.k.

  Mwandishi anadai kukubali mabadiliko ni mwanzo wa mtu kujitambua na kuendelea - ananukuu hadithi ya Bwana mmoja anaitwa Spencer Johnson inayoitwa "Who Moved My Cheese" (sitaki kurefusha bandiko, atakaehitaji kuisoma hiyo hadithi hata uki google utaipata -na kuna filamu yake pia). Kwa ufupi anasema mabadiliko hayakwepeki, kwa hiyo ni bora mtu ujipange namna ya Kuya -manage.

  Maoni yako tafadhali.
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  True..TRUE..true!!
  Watu hata kwenye mahusiano hua hawataki mabadiliko wakati yameshatokea na hapa ndipo wanapozaliwa wale VING¬ĎANG¬ĎANIZI...KUCHANGANYIKIWA...UKIWA...NA MACHOZI YASIYO YA LAZIMA!!
  ...nitafute kwa maelezo zaidi!!
   
 3. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #3
  May 30, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,658
  Trophy Points: 280
  95%ya wanadamu hawataki mabadiliko ndo maana watu hawapendi kufa,kuzeeka,kufilisika nk,kujitambu ni kitu kigumu sana kwa mwanadam,bahati mbaya ndo suluhisho la matatizo yote!
   
Loading...