Nimefanya utafiti usio rasmi nikagundua kuwa Wanaume wengi wanapokaa
kwenye siti za daladala hupenda kukaa na wanawake. Hilo ni dogo la ajabu zaidi
Hufurahi hata kama amesimama lakini akawa amebanwa na wanawake pande
zote. Yaani hata kama amebanwa husikii malalamiko yake kuwa anaumia au
vipi tofauti na ambavyo ingekuwa kwa mwanaume mwenzake.
1.Naomba wanaume wa JF mnithibitishie hili!
2.Vipi kwa wanawake na nyinyi inakuwaje upande wenu?
hata wanawake hupenda kukaa siti moja na mwanaume, mara nyingi sana nimeshuhudia wanawake wakizipita siti walipokaa wanawake wenzao kisha wanakuja kukaa nilipokaa! Labda, ile law ya opposite side attract, same side repel ina apply...?
Mambo kama haya hutokea zaidi kwa wanafunzi wa vyuo na teenagers, sidhani mtu mwenye ofisi yako utapoteza mda wa kufikiria mambo kama hayo uwapo ndani ya daladala badala ya kufikiria business itakuwaje au ilikuwaje siku hiyo..