CHA The GREAT
JF-Expert Member
- Nov 11, 2010
- 651
- 855
Jambo baya siku zote hulaaniwa na jamii iliyostaarabika, kwenye imani za kiroho mambo mabaya hulaaniwa, kwenye ulimwengu wa siasa mambo mabaya hulaaniwa, na kweye jamii yetu kwa ujumla, huwa tunalaani mambo mabaya.
Mambo mabaya ni kama vile:
1. UNAFIKI
2. UWIZI/ UPORAJI/UNYANG'ANYI
4. DHURUMA
5. UBAKAJI/UNAJISI/NA UFILAJI
Nachukua nafasi hii kulaani jambo moja kati ya hayo niliyoyaorodhesha. Kwamba, nalaani viongozi wa jumuiya za vyama vya wafanyakazi kwa kuwa wanafiki, hata kushindwa kupigania maslahi ya wafanyakazi. Nalaani kwa sababu unafiki wao unasababisha watu tunaoachiswha kazi tuteseke kwa kupigwa danadana katika suala zima la mafao. Eti wanaopunguzwa makazini wanapewa mafao yao, ila wanaofukuzwa kazi/kusitishiwa mkataba wa ajira hawapewi. Iwapo viongozi hawa wa vyama vya wafanyakazi wangekuwa wenye mioyo safi, wasingeacha hili lifanyike. Wanasahau kwamba, wamekuwa wakichukua sehemu ya mishahara yetu kwa ajili ya kujilipa marupurupu, na kulipana mishahara mizuri. Ila sisi tunaosababisha wao walipane marupurupu kutokana na hela zetu wanatusahau. Aya, tupo mitaani baada ya kupoteza ajira, ajira mpya hazipatikani, hatukopesheki kwa sababu hatuna dhamana, hatuwezi kuanzisha hata biashara ya kuuza ujugu kwa sababu ya vimishahara vidogo tulivyokuwa tunalipwa. Tunakwenda wapi jamani? Tunateseka wakati pesa zetu zimeshikiliwa na hii mifuko ya jamii!!! Nasema walaaniwe, hata wale wanasiasa tuliowapa kura zetu, na wanafumbia macho jambo hili, nao nasema walaaniwe. Eeh Mungu naomba usikie kilio changu.
Eeh Mungu, mimi mja wako.....najua wajua navyoteseka, najua wajua navyoumia na kukosa amani ya kiakili, najua wajua navyofedheheka kutokana na kutokuwa na pesa ambayo iko mikononi mwa hii mifuko ya jamii, naomba unisaidie mimi na watu wenye mahitaji kama mimi ili haki hii ipatikane, na uwalaani wale wote wanaosababisha tupate mateso haya. Ameni.