Nimekuwa nikipata changamoto juu ya moderm unlock na moderm upgrade hivi nini faida ya kuunlock moderm na pili naomba kujuzwa juu ya upgrade firmware inafaida gani katika moderm wataalamu tujuzeni. Jingine ninaloomba kujuzwa ni nini kati ya moderm na cm card kinacho detect aina ya network kama ni g,e,3g,h,h+ n.k mfano nimechukua cm card nimechomeka ktk moderm na network ya cm card iliyopo ni 3g je nilazima na moderm ninayotumia iwe ni 3g ndo moderm isome mtandao 3g? Au ilimladi network ni 3g ukichomeka ktk moderm yoyote itasoma 3g? Nijuzeni tafadharini.. karibu.
Hauwezi Ku Uliza Umuhimu wa ku Unlock Modem ni Bora uulize maana yake maana inaonesha haujui maana ya Ku Unlock Modem ndo maana unauliza Umuhimu
Makampuni Mengi ya mitandao ya Simu yanauza Modem yakiwa yamezifunga usiweze kuzitumia kwa mtandao wa Simu nyingine e.g Ukinunua Modem ya Halotel ukaweka Line ya Halotel ukiweka Line ya Airtel haitokubali mfano waweza ambiwa Uingize Unlock Code(kwa lugha nyepesi ni kama PIN Code) kuifungulia milango ya kupokea ya Line nyingine au Unaweza ambiwa Line Uliyoingiza Sio sahihi.
Mpaka hapo tumeona mitandao inachojaribu kufanya ni kutufungisha Ndoa ya Kikristo ili tutumie mtandao wao pekee au tununue Vifaa vingine vya mtandao mwingine.
Sasa Kwa kuwa watu hawapendi kuharibu hela wanatafuta Njia ya kuifanya hiyo Modem ilofungiwa kutumia mtandao mmoja iweze kutumia mitandao mingine na hapo ndo tunaita ku Unlock Modem.
Njia zinazotumika Ku Unlock ni :-
1)Kutumia Network Control Key(NCK) au waweza kuita Unlock Codes/Pin na hizi Pin unaombwa uziweke pale unapoingiza line ya Simu ya Kigeni.
2)Njia ya pili ni Kubadilisha Firmware/Ku downgrade au ku Upgrade Firmware
Firmware ni Kama Operating Software ya Modem hivo Lock inakua imewekwa humo,hivo ukibadilisha hiyo software/Customized Firmware na kuweka Software Universal iliyokuwa compatible na hiyo modem husika utakua umeondoa Lock.
3)Kubadilisha Dashboard ya Modem pia ni njia nyingine inayotumika kwa baadhi ya Modem za ZTE ambazo Lock haiwekwi kwenye Operating Software bali inawekwa kwenye Dashboard/ Customized Dashboard
Kuhusu 2G/3G hii inategemea na mahali unapoishi kama Minala imefungiwa vifaa vya 3G utapata 3G kwenye Modem yako au Simu yako iwapo nayo ina uwezo wa 3G.Bahati Mbaya Sijawai Kuona Modem ya 2G pekee tokea nizijue modem hivo modem zote za Kileo zina Support 3G japo katika Speed tofauti WCDMA/HSPA(H)/HSPA+(H+)/DC-HSPA+.
Njia rahisi ya kuhakikisha Modem yako haishiki 2G/EDGE/E kwa Modem za Huawei ni kwenda Tools>>>>>Options>>>>Network type kisha ukaondoa WCDMA prefered na kuweka WCDMA Only.
Ukiona mtandao Umepotea basi hilo eneo hamna 3G nenda Ofisi za karibu yako za Halotel waulize kama 3G ipo hilo eneo lako wakisema ipo nunua line yao utumie hiyo(Maana yake hapa acha kukalili na kung'ang'ana na mtandao mmoja) Halotel wame cover 3G almost 95% ya Tanzania
Line haisuki katika kusoma 3G labda kwenye Teknolojia ya 4G ndo mitandao ya simu inakudai ununue Line ya Simu ya 4G
Bila Shaka utakua umeelewa mpaka hapo