Na nyie wamiliki wa bastola mbadilike!

Na nyie wamiliki wa bastola mbadilike!

mwitu

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2012
Posts
856
Reaction score
200
wenye bastola mimi sijawahi kusikia mmeua jambazi au kibaka zaidi ya kusikia mmeua au kujiua kwa uwivu wa kimapenzi au kumjeruhi mfanyakazi wake. Kwanini?
 
Kweli kabisaa utabidi saiv gun permits zizuiliwe maana tuna hatarisha maisha yetu
ila haya maswala ya kuacha kuachwa yata toa roho wengi
 
Wapimwe akili zao kwanza kabla hawajamilikishwa. Vigezo na mashariti iwe kujeruhi au kuuwa wezi na vibaka tu.
 
mtu anayrmiliki bastola wa kumwangalia sana maana lengo la kuwa na silaha ya moto ni nini????
 
Matumizi ya bastola , visu , mapanga, shoka, nk yalikuwepo toka zaman cha msingi ni watu kubadilika kudhibiti hasira pind kunapotokea kutokuelewana ndan ya nyumba

Sent from my BlackBerry - jamiiforums
 
Kumiliki bastola siyo tatizo ,tatizo utacontrol vipi hasira pale unapotatizwa.....maana km huwezi hata kisu pia ni siraha pia ....just tuwe tunacntrl hasira hasa tunapo piga tungi
 
wenye bastola mimi sijawahi kusikia mmeua jambazi au kibaka zaidi ya kusikia mmeua au kujiua kwa uwivu wa kimapenzi au kumjeruhi mfanyakazi wake. Kwanini?

ni kweli mkuu,hazina faida ktk jamii zaidi ya kuua watu wa karibu!SIJAWAHI PIA SIKIA MTU KAJITETEA DHIDI YA JAMBAZI NA KAMUUA
 
wenye bastola mimi sijawahi kusikia mmeua jambazi au kibaka zaidi ya kusikia mmeua au kujiua kwa uwivu wa kimapenzi au kumjeruhi mfanyakazi wake. Kwanini?
Tubadilike kwenye lipi mkuu!!?? Matukio ya kuuwawa Majambazi na Wahalifu yapo...labda haujayasikia au kukutana nayo.

mtu anayrmiliki bastola wa kumwangalia sana maana lengo la kuwa na silaha ya moto ni nini????
Kuna wamiliki wa Bastola wanatumia kikazi,kujihami binafsi na Ulinzi wa Familia majumbani.
Kuna tukio lilimtokea jamaa mmoja mtoto wa kigogo hapa mjini...alijikuta ameenda uswahilini maeneo ya Kawe ndani ndani kumshusha mtoto wa kike, kwa Bahati mbaya hiyo barabara ilikuwa inaishia na haitokezei kokote (dead end street). Ghafla alivamiwa na Vijana Kama wanane hivi wakiwa na Mapanga makali wakitaka ashuke kwenye gari (Range Rover). Alipoanza kurudi nyumba taratibu wakaanza kushambulia gari kwa mapanga. Kilichomuokoa jamaa pale kwa bahati alikuwa na Bastola akapiga Juu kupitia sun roof...ndio jamaa wakatawanyika na wenyeji wa pale wakatoka.

Kumiliki bastola siyo tatizo ,tatizo utacontrol vipi hasira pale unapotatizwa.....maana km huwezi hata kisu pia ni siraha pia ....just tuwe tunacntrl hasira hasa tunapo piga tungi
Ulichozungumzia ni cha msingi sana mkuu. Tatizo sio kumiliki Silaha,tatizo kubwa ni elimu ya matumizi ya silaha.
Kwa mfano mimi binafsi huwa Silaha wakati wa mchana huwa naiweka kwenye buti...giza likiingia ndio nakuwa nayo kwenye kiti cha Dereva. Kuna siku haya mambo ya udereva kuna jamaa bahati mbaya sikumuona...akaja akanibloki na kunitukana sana MATUSI makali huku kwenye gari nikiwa na wife..watoto 2 na mama mkwe nawapeleka hospital. Mimi nikampuuza jamaa nitaendelea na safari yangu. Kumbe ile kumpuuza ikamtia jazba...akanikimbiza kwa gari akaja akanibloki halafu akashuka kwenye gari na kunifuata kwa nguvu huku ameshika spare ya kufungulia tairi na kupiga mlangoni kwangu. Hasira iliyonipata Kama silaha ingekuwa karibu siku ile ningetoa mtu uhai. Katika watu kumshika huku akipandisha Mzuka ..nilifungua buti na kushuka...wife akajua nini kinafuata akaanza kupiga kelele na watoto pia. Huwezi Amini ule muda wa kutoka kwenye kiti cha Dereva mpaka kwenye buti Hasira sijui zilipotelea wapi mkuu. Ikaishia hivyo hivyo tu nikaondoka zangu. Lakini jamaa siku ile aliuweka utu wake rehani bila kujua Haki ya Mungu.
 
Kuna wamiliki wa Bastola wanatumia kikazi,kujihami binafsi na Ulinzi wa Familia majumbani.
Kuna tukio lilimtokea jamaa mmoja mtoto wa kigogo hapa mjini...alijikuta ameenda uswahilini maeneo ya Kawe ndani ndani kumshusha mtoto wa kike, kwa Bahati mbaya hiyo barabara ilikuwa inaishia na haitokezei kokote (dead end street). Ghafla alivamiwa na Vijana Kama wanane hivi wakiwa na Mapanga makali wakitaka ashuke kwenye gari (Range Rover). Alipoanza kurudi nyumba taratibu wakaanza kushambulia gari kwa mapanga. Kilichomuokoa jamaa pale kwa bahati alikuwa na Bastola akapiga Juu kupitia sun roof...ndio jamaa wakatawanyika na wenyeji wa pale wakatoka.

Duh gari ilishambuliwa kwa mapanga!!!!!!
 
Ndio hivyo mkuu. Yale masela ilikuwa nia Yao mshikaji asimame na kushuka kwenye gari ili wafanye Yao. Ikawa bahati nzuri jamaa alikuwa na silaha. Majirani walipotoka walimwambia hiyo ndio ilikuwa salama yake...la sivyo angejikuta yuko uchi na majeraha ya mapanga...so you can Imagine. Kuna maeneo ukijichanganya hovyo unaumia mkuu.
 
nilishasema kuhusu wamiliki wa bastola
 
wapi ntapata ka bastola used ka bei rahisi wajameni? Kuna jamaa nae aligonga mwendesha bodaboda bahati mbaya, si wakaitana kundi wanataka wamfanyizie? kama sio kuwa na hiyo kitu leo angekua hayati.
 
Tubadilike kwenye lipi mkuu!!?? Matukio ya kuuwawa Majambazi na Wahalifu yapo...labda haujayasikia au kukutana nayo.

Kuna wamiliki wa Bastola wanatumia kikazi,kujihami binafsi na Ulinzi wa Familia majumbani.
Kuna tukio lilimtokea jamaa mmoja mtoto wa kigogo hapa mjini...alijikuta ameenda uswahilini maeneo ya Kawe ndani ndani kumshusha mtoto wa kike, kwa Bahati mbaya hiyo barabara ilikuwa inaishia na haitokezei kokote (dead end street). Ghafla alivamiwa na Vijana Kama wanane hivi wakiwa na Mapanga makali wakitaka ashuke kwenye gari (Range Rover). Alipoanza kurudi nyumba taratibu wakaanza kushambulia gari kwa mapanga. Kilichomuokoa jamaa pale kwa bahati alikuwa na Bastola akapiga Juu kupitia sun roof...ndio jamaa wakatawanyika na wenyeji wa pale wakatoka.

Ulichozungumzia ni cha msingi sana mkuu. Tatizo sio kumiliki Silaha,tatizo kubwa ni elimu ya matumizi ya silaha.
Kwa mfano mimi binafsi huwa Silaha wakati wa mchana huwa naiweka kwenye buti...giza likiingia ndio nakuwa nayo kwenye kiti cha Dereva. Kuna siku haya mambo ya udereva kuna jamaa bahati mbaya sikumuona...akaja akanibloki na kunitukana sana MATUSI makali huku kwenye gari nikiwa na wife..watoto 2 na mama mkwe nawapeleka hospital. Mimi nikampuuza jamaa nitaendelea na safari yangu. Kumbe ile kumpuuza ikamtia jazba...akanikimbiza kwa gari akaja akanibloki halafu akashuka kwenye gari na kunifuata kwa nguvu huku ameshika spare ya kufungulia tairi na kupiga mlangoni kwangu. Hasira iliyonipata Kama silaha ingekuwa karibu siku ile ningetoa mtu uhai. Katika watu kumshika huku akipandisha Mzuka ..nilifungua buti na kushuka...wife akajua nini kinafuata akaanza kupiga kelele na watoto pia. Huwezi Amini ule muda wa kutoka kwenye kiti cha Dereva mpaka kwenye buti Hasira sijui zilipotelea wapi mkuu. Ikaishia hivyo hivyo tu nikaondoka zangu. Lakini jamaa siku ile aliuweka utu wake rehani bila kujua Haki ya Mungu.

Unaniangusha mkuu bhana!!!!!!

Keep on training on anger management mpaka uweze kuwa na uwezo wa kuongea bila kufikiria bastola kama mazingira sio hatarishi!!!!!!!Zoeana nayo kama rafiki ambaye sio kila ukizozana yeye anarusha ngumi,chagua rafiki anayekupatanisha zaid kuliko kukuchochea ugomvi "talk with him" asikupe kiburi kila inapotokea kutoelewana,mwambie awe anakushauri hata kukimbia ukipata upenyo!!!!!!!

Halafu nani kakuambia silaha inakaa kwenye buti????!!!!!Kama mtu anakutaka hivi hilo buti utalifikia kweli???!!!!Mkuu mpaka watoto wanajua dad una silaha na inakaa kwenye buti ya gari kwa nini????!!!

Anza na.kutenganisha silaha na.mag hapo ulipo lakini sio kuacha kwenye buti mkuu!!!!!!!

Ukiamua kuwa na.silaha mkuu ashakum si matusi ni kama una "nanihii mbili" unatakiwa kujua bila dhana wapi ni wapi na nini ni nini,wapi unafanya nini na kwa nini,yaani sio kitu cha kuacha un attended hata ukiwa ndani kwako!!!!!!!
 
Mkuu haujanielewa nilichoandika kwenye hiyo post yangu uliyoquote.
Mimi naweza silaha kwenye buti ni uamuzi wangu binafsi...ni ninapoiweka kutokana na aina ya gari ninayotumia naweza kuifikia bila hata kushuka kwenye gari.
Sijaandika sehemu yoyote Kama watoto wangu wanajua namiliki silaha....Ila MKE wangu anatambua Hilo kutokana na Kazi yangu.
Mtu akinitaka na kunipata itakuwa ndio Mungu amepanga iwe hivyo...lakini najiamini na mafunzo niliyopata kuhusu kutumia silaha ninaweza kupambana na wewe ukiwa na silaha yako bila woga. Sio kila Mwenye silaha anajua kutumia silaha.
Hiyo technic ya kutenganisha Mag na silaha ni ya kizamani sana.
Naweka silaha kwenye buti mchana kwa kuwa najiamini na niko makini na mazingira yaliyonizunguka. Na kila radius fulani kunakuwa na rapid response team Kama unanielewa kwa Hilo....kwa hiyo it's a matter of a phonecall away.
 
Back
Top Bottom