Na nembo hii hatuitaki kwenye shirikisho letu

Na nembo hii hatuitaki kwenye shirikisho letu

Status
Not open for further replies.

GHIBUU

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2011
Posts
4,432
Reaction score
3,016
NEMBO-TANGANYIKA.jpg

Nembo ya Tanzania

Nembo ya Tanzania ni ngao ya askari inayoshikwa na watu wawili.

Ngao ina sehemu nne: juu sehemu ya dhahabu, chini yake bendera ya taifa, halafu sehemu nyekundu na chini kabisa sehemu ya buluu-nyeupe
a) robo ya juu inaonyesha mwenge wa uhuru juu ya rangi ya dhahabu inayokumbusha juu ya utajiri wa madini ya taifa
b) robo ya pili ni bendera ya Tanzania
c) rangi nyekundu inamaanisha ardhi nyekundu ya Afrika na kilimo kama msingi wa maisha ya watu.
d) milia ya buluu na nyeupe katika robo ya nne inamaanisha mawimbi ya bahari na maziwa kwenye mipaka ya nchi pamoja na bahari inayozunguka Zanzibar kama sehemu ya Jamhuri ya Maungano.

Juu ya sehemu hizi kuna mkuki na majembe mawili yanayokumbusha juu ya utetezi wa uhuru na umuhimu wa kazi katika ujenzi wa taifa.

Ngao yote imeviringishwa na mapembe ya ndovu yanayomaanisha utajiri wa wanyamapori na hifadhi za taifa.
Ngao inalala juu ya mlima Kilimanjaro ambayo ni mlima mkubwa wa Tanzania.

Watu wawili wanaoshika ni mwanamume na mwanamke kama dalili ya ushirikiano wa jinsia zote mbili taifani. Wanasimama juu ya mpamba na mkarafuu ambayo yote inazaa mazao muhimu ya kibiashara ya Tanzania Bara kwa pamba na Zanzibar kwa karafuu.
Kanda njano ya maandishi chini ya ngao huonyesha wito la taifa "Uhuru na Umoja"


Dreceres ràpides: navegació, cerca
COA_Tanganyika_1.jpg
 
Ama kwe waswahili wakorofi mnaanza kuhoji vitu vya kipuuzi! .. Pole Dr Shein!
 
ha ha ha ha, jiti limewaingia. umenena wa nyumbani
ongeza mashambuliz hamna kurud nyuma
 
Hii ndio TANZANIA bhana!Ku chenchiana wenyewe kwa wenyewe hata na raslimali zetu kwa vijimaneno vya kijiweni hatuonagi hatari!NAKUPENDA NCHI YANGU TZ!
 
Pole pole wajameni sisi sote ni ndugu,kwa nini ugovi na vitu vidogo vidogo? Visiwa hivi ni sehemu ya ngapi ya Tanganyika?Visiwa hivi vina watu wangapi? na tanganyika ina watu wangapi?kwa nini tulinganishe kila kitu?
 
Yaani watu wengine badala ya kujadili mambo ya maana wanajadili nembo...
 
Bange mbaya...baada ya kupata stim umeona nembo ndio kilakitu...?
 
Hivi ni vijivisa, ukweli ni kwamba, muungano hatuutaki!
Kama imeshindikana kuendesha serikali moja, pamoja na kuwa miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa utegemezi wa misaada toka nje (ikiwa ni pamoja na misaada ya waliberali), hivi serikali tatu, tutafika wapi????? Tufunguke watz, serikali tatu inakula kwetu.
 
Tusibadilishe hiyo nembo bali tuongezee mambo ya upande wa Zanzibar,mfano tende na harua, waswahili waliovaa vibaraghashia, tuweke kisiwa cha Nungwi
 
Tusibadilishe hiyo nembo bali tuongezee mambo ya upande wa Zanzibar,mfano tende na harua, waswahili waliovaa vibaraghashia, tuweke kisiwa cha Nungwi

Hapo juu tunaambia ni mkarafuu mi naona ni majani ya bangi ,Tanganyika kuna bangi nyingi sana inalimwa.
 
Ni upuuzi kwa wanaotaka serikali tatu gharama zote za nn? 1 inatosha sana rais mmoja bunge moja. Serikali tatu then ardhi ya tanganyika itumike na wazanzibar wengi? Au Zanzibar itatoa pasu pasu kwenye kwenye maswala ya muungano? Shirikisho ninini?
 
Kejeli hazitosaidia,tanganyika bila ya z'br inawezekana.
 
Sasa ukiacha karafu na bahari mna nini? Au mnataka muweke picha ya matofaa? Au shokishoki? Au ulitaka awekwe shoga hapa?

mmoja kati ya hao watu 2 kwenye nembo anatakiwa awe amevaa kanzu, kikoi na kofia kuwakilisha utamaduni wa mzanzibari.
 
Mi sioni hata sababu ya kubeba hili zigo! Si mjiendee zenu na Zanzibari yenu! Nawaonea huruma vile mnavyopenda ubwabwa maana lazima mje huku bara atiiiii!
 
Sasa ukiacha karafu na bahari mna nini? Au mnataka muweke picha ya matofaa? Au shokishoki? Au ulitaka awekwe shoga hapa?

Ni ukweli ulio wazi kabisa kwamba hiyo nembo ilikuwa ni copy paste kutoka Tanganyika. Kabla ya muungano nembo ya taifa ya Tanganyika ilikuwa hii hapa: Hakuna tofauti kubwa sana na hii mpya ya muungano.


tanganyika_coa_n6791.gif
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom