Mengi tumeyasikia ktk hotuba ya mh Rais. Wengine wakidhani ni mwanzo wa nchi ya maziwa na asali. Kimtazamo ni mwanzo wa nchi isiyo na mipango. Hivi tutatoa wapi billion zaidi ya 200 za kufidia upungufu wa ada na michango ya mbalimbali? Mbona kuna ujenzi wa barabara nyingi umesimama haujazungumziwa au kwa kuwa ni madeni? Amewataja wamachinga nk mbona hakuna mkakati wowote kisera wa kuwawezesha hawa na mama ntilie? Nchi haijengwi na mtu mmoja bali uwepo wa taasisi imara na endelevu. Kuiga la Kagame ni sawa na kuiga kwa Gaddafi ambapo uendelevu wake unategemea uhai wa mtu.