Na ije ijumaa

Na ije ijumaa

Kitaja

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2011
Posts
2,836
Reaction score
1,383
NA IJE IJUMAA

1. Na ifike ijumaa, twaisubiri kwa hamu,
Hatutaki kuzubaa, siku ya mashamushamu,
Kusuka ama kunyoa, kwao wezi wa kalamu,
Na ifike ijumaa, tuone hatima yao.

2. Mmoja kakata kamba, kakimbia machinjio,
Imekuwa ni kasumba, wakikosa kimbilio,
Wengine wayumbayumba, kama siku ya gulio,
Na ifike ijumaa, tuone hatima yao.

3. Ijumaa sio mbali, twangojea uamuzi,
Naona moshi kwa mbali,wafuka bila ajizi,
Walishaonja asali, mzinga hawauwezi,
Na ifike ijumaa, tuone hatima yao.

4. Shoka limo shinani, kukata lipo tayari,
Limeanza mitaani, kutanguliza habari,
Laendelea mwakani, wakizidisha jeuri,
Na ifike ijumaa, tuone hatima yao.

5. Majizi yote pembeni, twaja mbio tupisheni,
Utani weka pembeni, ofisi zetu pisheni,
Fedha zetu rudisheni, vifungo ni haki yenu,
Na ifike ijumaa, tuone hatima yao.
 
Natabiri kwamba hatasema cha maana. Tena ushauri wangu afadhali asizungumze, atekeleze tu kimya kimya. Atajaribu kujinasua na hali hata kama hahusiki, kwa vile yeye ndiye aliyetuletea watu hao, anahusika.
Asijaribu katu kuleta excuses kwani hii si mara ya kwanza, ya pili, ya tatu wala ya tano. Kwa kweli WaTZ ni wavumilivu sana. Au tuseme............. wapumbavu.
 
Nahs ukituita wapumbavu utakuwa umetupendelea sana, tuite ashk majnun
 
Natabiri kwamba hatasema cha maana. Tena ushauri wangu afadhali asizungumze, atekeleze tu kimya kimya. Atajaribu kujinasua na hali hata kama hahusiki, kwa vile yeye ndiye aliyetuletea watu hao, anahusika.
Asijaribu katu kuleta excuses kwani hii si mara ya kwanza, ya pili, ya tatu wala ya tano. Kwa kweli WaTZ ni wavumilivu sana. Au tuseme............. wapumbavu.

Ni kweli usemalo ndugu ngoja tumsikilize mkuu kama atawatosa "washikaji"
 
Aiseee..! we ni nomaaaaa., big up! hongera! unfortunately dhaifu anakuja na ngonjera tena huku akicheka cheka bila sababu za msingi!
 
Hafanyi chochote huyo. Warema anatosha kuwafanya wamarekani name wamagharibi watowe fedha za walipa kodi wao wakati Kodi za wtz zinaporwa na hao wateuzi wake.
 
Hafanyi chochote huyo. Warema anatosha kuwafanya wamarekani name wamagharibi watowe fedha za walipa kodi wao wakati Kodi za wtz zinaporwa na hao wateuzi wake.

Inawezekana asifanye chochote ila atakuwa amekizika rasmi chama chake. kijijini kwetu hata akina bibi wanaelewa ishu ya escrow na kwa mara ya kwanza CHADEMA wamechukua mitaa kadhaa
 
Na ifike ijumaa tuone hatima yao, wana hali mbaya, nape ni shahidi
 
Kesho ijumaa, na ifike ijumaa isiyo na mawingu isijepatikana sababu ngiri imebana.
 
NA IFIKE-IJUMAA!

(1) Na ifike ijumaa, twaisubiri kwa hamu,Hatutaki kuzubaa, siku ya mashamushamu,Kusuka ama kunyoa, kwao wezi wa kalamu,Na ifike ijumaa, tuone hatima yao

(2.)Mmoja kakata kamba, kakimbia machinjio,
Imekuwa ni kasumba, wakikosa kimbilio,
Wengine wayumbayumba, kama siku ya gulio,
Na ifike ijumaa, tuone hatima yao.

(3)Ijumaa sio mbali, twangojea uamuzi,
Naona moshi kwa mbali,wafuka bila ajizi,
Walishaonja asali, mzinga hawauwezi,
Na ifike ijumaa, tuone hatima yao!

(4)Shoka limo shinani, kukata lipo tayari,Limeanza mitaani, kutanguliza habari,Laendelea mwakani, wakizidisha jeuri,Na ifike ijumaa, tuone hatima yao!

(5)Majizi yote pembeni, twaja mbio tupisheni,
Utani weka pembeni, ofisi zetu pisheni,
Fedha zetu rudisheni, vifungo ni haki yenu,
Na ifike ijumaa, tuone hatima yao!

Note:
Copied somewhere!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom