Na hili pia katiba mpya ifanye liwe la lazima

mchemsho

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
3,212
867
Suala la chama cha mapinduzi kuwaepusha wagombea wao na midahalo ya wazi 'debates' kutokana na kutowaamini kiuewezo, imepelekea ofisi za umma kukaliwa na matango pori eti viongozi. Debate itasaidia sisi wananchi kuwapima na kufahamu uwezo halisi wa mgombea. Ccm imeligarimu taifa hili kwa kuandaa watu wasio na uwezo kushika nafas kubwa kabisa halafu hakuna cha maana wanafanya kaz kutoa majibu mepesi katka mambo magumu. Tume ya uchaguzi iratibu midaharo itakayowashindanisha mbele ya public. Marekani hili linafanyika kila uchaguz na linamanufaa sana kwa hiyo ingefaa liwekwe kwenye katiba mpya hivyo liwe la lazima na wananchi tukione hcho ambacho ccm hawataki tukione kwa kukacha midaharo. Kama unajiamini kwann uogope ku debate??
 
Hata kama halitawekwa kwenye katiba, ni muhimu wananchi waelimishwe namna ya kuwatambua viongozi wao kabla hawajawapigia kura. Kama mgombea atakimbia mdahalo bila sababu ya msingi, basi atakua amejipotezea uhalali wake kwa wananchi katika kupata ridhaa yao. Pia itasaidia sana katika vyama kupitisha wagombea makini watakaoweza kujenga imani kwa wananchi kuhusu wao wenyewe pamoja na vyama vyao.
 
Man you talk wisdom sio kama Ritz.
 
Tatizo jingine kubwa ni kuwa vyama vyetu havina sera zinazoeleweka. Nimeangalia mdahali Marekani na inaonekana jinsi wagombea walivyobobea katika ku=artiuculate sera za vyama vyao. hapa kwetu tuna siasa za ubinfsi mno, za kuangalia watu badala ya issues
 
Back
Top Bottom