Muelekeo wa utawala wa Magufuli: Ulazima wa katiba mpya na Rasilimali za Taifa

Manelezu

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
1,907
2,769
Taifa lolote lile ili liendelee ni lazima liwe na viongozi wenye maono ya kuliongoza taifa hilo kwenye kilele cha mafanikio. Ukisoma kitabu kinachoitwa “DENG XIAOPING AND THE TRANSFORMATION OF CHINA” by Ezra Vogel, utaelewa kwanini kuna umuhimu wa kupata kiongozi jasiri anaeweza kulipeleka taifa kwenye kilele cha mafanikio.

Si rahisi kuona taifa linainuka na kuwa taifa lenye nguvu bila kuwa na viongozi wenye moyo wa kujitolea na wanasiasa wanaotanguliza maslahi ya nchi kwanza.

1. Muelekeo wa utawala wa Magufuli

Bila shaka kila mtanzania anaefuatilia siasa za Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atakubaliana na mimi kwamba ni mwanasiasa aliyejitolea kuona taifa lake linasonga mbele kwa gharama yoyote ile. Na hiki ni kitu muhimu sana. Mh. Rais ameanzisha kwa dhati kabisa mapambano zidi ya ufisadi, unyonyaji, ubadhilifu na utoroshwaji wa rasilimali za taifa.

Pia ameamua kutumia rasilimali nyingi za taifa kujenga economic infrastructure na kutoa msukumo mkubwa katika kujenga discipline ya kazi na kulipa kodi ili kujenga taifa lenye uchumi imara na unaojitegemea. Huu kwa ufupi kabisa ndio muelekeo wa utawala wa Mh. John Magufuli.

2. Ulazima wa katiba mpya na rasilimali za taifa

Katiba ndio kitu muhimu sana katika kukuza na kuendeleza taifa liwe na Amani, utulivu na umoja. Katiba ndio kitu pekee kinachoweza kulinda rasilimali za taifa hili. Sheria mpya iliyopitishwa na bunge mwaka huu haitakuwa na maana bila kuwa na katiba inayotoa ulinzi wa rasilimali za taifa.

--Dhahabu, mafuta, gas, uranium, chuma, etc lazima vilindwe na katiba mpya. Katiba mpya inatakiwa ili kumsaidia Mh. Rais kuliacha taifa salama na ningependekeza katika suala la katiba viingizwe vifungu vinavyokataza mabadiliko yoyote yale ya katiba katika baadhi ya vifungu bila kupelekwa na kupigiwa kura na wananchi wenyewe “Entrenchment Clauses”. Baadhi ya masuala haya (a) Mamlaka ya bunge kuita,kupitia au kuzuia mikataba au mkataba wowote ule unaoingiwa au inayoingiwa na serikali na mashirika ya kimataifa kuhusu rasilimali za taifa-hili ni suala muhimu sana katika kulinda rasilimali za taifa, kuondoa rushwa na kudhibiti utoloshwaji wa rasilimali za taifa.

--Suala linguine nyeti kwenye katiba mpya ni muhimu kuwepo na kipengele kitakachoondoa ukomo wa uongozi wa miaka 10. Katiba ni muhimu itamke uchaguzi utafanyika kila baada ya 5 na chama kitakachoteuwa mtu na akapigiwa kura na wananchi kwa uwazi basi aendelee kutawala na kuwa kiongozi wa taifa. Kwanini haya mabadiliko yana umuhimu? Hapa itawapa wananchi mamlaka ya kuamua kuendelea na kiongozi wanaemtaka na mwenye uwezo wa kuwaletea maendeleo hata baada ya miaka 10 na hili ni la muhimu sana ili kuleta continuity. Magufuli leo anapambana kuondoa ufisadi katika taifa, inaweza kutoa baada ya miaka 10 ya uongozi wake akatokea kiongozi atakayeturudisha nyuma kwenye ufisadi tena kwa kasi kubwa. Hivyo basi tuwe na katiba inayoruhusu kiongozi kuendelea pale wananchi watakapoona anafaa. Mfano mzuri ni katiba ya wiingereza au ujerumani.

Naomba kuwasilisha.
 
Well said..

But nina doubt kama vijana wa Buku Saba Payroll watakuelewa...

Hii ni kwasababu wao ni initiators na supporters wakubwa kwa huu upuuzi waliouanzisha wa " aongezewe muda... "

Unamuongezea mtu muda kwa grounds zipi?? Kwa kuvunja Katiba??

Huku si ni kuleta machafuko kwenye Nchi..??
 
Back
Top Bottom