Na ajabu katika matumizi ya awamu ya tano

Na ajabu katika matumizi ya awamu ya tano

HAPA NDIO TUNAPOPIGWA WATZ. 👇👇

Maajabu ya awamu ya tano, hakuna ajira mpya, wametoa watumishi hewa, hakuna nyongeza ya mishahara, lakini kila mwaka bajeti ya mishahara inapaa
Mwezi March mwaka 2014 serikali ilitumia Bilioni 375.9 kulipa mishahara kwa watumishi (Salaries and wages). Kumbuka kipindi hicho kulikua na watumishi hewa, kulikua na watu wanalipwa mishahara miwili miwili, kulikua na nyongeza ya mishahara, na watumishi wapya waliajiriwa kila mwaka.

Kipindi kama hicho (mwezi March) Mwaka 2018 serikali ilitumia Bilioni 527.4 kulipa mishahara. Kipindi kama hicho mwaka huu, serikali imetumia Bilioni 557.6 kulipa mishahara. Hizi ni takwimu rasmi kama zilivyotolewa na Wizara ya Fedha na Mipango. Yani gharama ya kulipa mishahara imekua ikiongezeka mwaka hadi mwaka licha ya kuondolewa wafanyakazi hewa na dili nyingine feki.

Kwa wale wachumi daraja la kwanza, hii inawezekanaje? Yani unaondoa wafanyakazi hewa, unazuia nyongeza ya mishahara, unazuia ajira mpya lakini gharama ya kulipa mishahara inazidi kuongezek. JK aliwezaje kuwa na wafanyakazi hewa na wote wakalipwa, akaweka nyongeza ya mishahara kila mwaka kwa watumishi wote hadi wale hewa, na akaweza kuajiri maelfu kila mwaka kwa gharama ndogo? Who can explain this Economic paradox?

View attachment 1183365

Baadhi ya comments za watu;
Hizi report ziko shallow sana au kisiasa zaidi ,nilitegemea nione hapo ,idadi ya wafanyakazi mwaka 2014 vs 2018, idadi ya wafanyakazi waliokuwa promoted kuanzia mwaka 2014 vs 2018 , mishahara ya group Fulani mwaka 2014 vs 2018 , ukileta ya report ya hivyo nitakuelewa kwa mbaliii, na kingine kama wanaweza kulipa mishara hiyo ina maana wafanyakazi wameboreshewa mishahara yao through allowances nk na walio ajiriwa ni wengi ,naomba mtoa post share data itapendeza sana vinginevyo uko kisiasa

mishahara ni pamoja na madeni na malimbikizo

weka idadi ya watu, promotions, madeni nssf wcf,n.k

make it professionaly presentable ndio uweze kujenga hoja from numbers kuwa unaibiwa

ila kama ulizoea uwizi au kuibiwa, jua na amini kiwa wezi wapo ila katika hao sio JPM

Trust me JPM ananyoosha nchi
 
Inaelekea unanufaika na hali hii.

Mke wangu ni mtumishi wa serikali anadai malimbikizo ya kupandishwa daraja kutoka 2015 hajalipwa hadi leo, hajapata increment toka 2016, na sio peke yake.
Mwezi wa tano watumishi wenzake wengi kwenye Halmashauri anayofanya kazi walipewa barua za kupandishwa vyeo lakini mishahara ni ileile.
Hili la upigaji ni la wazi kabisa.
Kasahau kwamba kuna walio panda madaraja na mishahara imebadilishwa, anasahau kwamba kuna waajiriwa wapya kada mbalimbali na wapo kazin tuwe wafuatiliaji wa mambo jamani tusiwe watu wa kutafuta lawama wakati wote
 
Unayo habari pia kwamba waliokuwa na mishahara mikubwa imepunguzwa?
Kasahau kwamba kuna walio panda madaraja na mishahara imebadilishwa, anasahau kwamba kuna waajiriwa wapya kada mbalimbali na wapo kazin tuwe wafuatiliaji wa mambo jamani tusiwe watu wa kutafuta lawama wakati wote
 
Mh Zitto aliwahi kusema..." Tumewakabidhi Nchi washamba na malimbukeni" hapa alimaanisha viongozi wa mihimili 2 yaani Rais na Spika...

Jamaa sio tu wanaiba bali "wanazoa"
Nchi imejaa malalamiko kila kona toka serikalini hadi Mkulima Mdogo wa mahindi wa kule Namanyele...
Jamaa ameshindwa na hafai kabisa !!
Hata washamba nao ni watanzania na wanahaki sawa...
hao wasio washamba toka uhuru wametufikisha wapi?
Faq Zitto na yeyote anaye support huu ujinga
 
Awamu ya washamba na malimbukeni yani wao matumizi ni makubwa kuliko makusanyo,msafara wake unatumia gharama kubwa utakuta unawatu na magari zaidi ya mia.
Wote hao wanahitaji posho za kujikimu
 
Kipindi kama hicho (mwezi March) Mwaka 2018 serikali ilitumia Bilioni 527.4 kulipa mishahara. Kipindi kama hicho mwaka huu, serikali imetumia Bilioni 557.6 kulipa mishahara.

Ongezeko linatokana na baadhi ya wanene kutumbuliwa na kuwekwa wapya, kumbuka kuwa mnene akidondoshwa mshahara wake unabakia uleule, na mwingine anayekuja anaongezewa iwapo alikuwa kwenye nafasi ya chini kabla ya hapo
 
jaribu kutuonesha kama idadi ya watumishi ni walewale please...
umekwapua namba ya pesa unalia nayo.... na unadai kuna ufisadi....
Base ya hiyo ni idadi ya watu, promotions etc.... Please tuongezee nyama tujadili
Kama idadi ya watumishi ni ile ie ntaungana nawe kuuita ni ufisadi
@sky eclat njoo na mchanganuo, mahakama zilienda ngapi, bunge, polisi, jeshi, magereza, uhamiaji wizara na halmashauri v/s mgao wao wa siku za nyuma ili tuone nani ana fungu zaidi na kwa nini ! Hivyo tuu, usituchukulie poa
 
Ongezeko linatokana na baadhi ya wanene kutumbuliwa na kuwekwa wapya, kumbuka kuwa mnene akidondoshwa mshahara wake unabakia uleule, na mwingine anayekuja anaongezewa iwapo alikuwa kwenye nafasi ya chini kabla ya hapo
Si kweli rejea sheria ya utumishi wa umma na kanuni zake, kwa mfano mtumishi amepata nafasi ya uteuzi halafu akatumbuliwa mshahara wake hadi kwenye cheo cha principal ambacho mshahara wake ni tsh 2,300,000/, na akitokea aliyetumbuliwa hakuwahi kuwa mtumishi ,mshahara unakoma mara moja.
 
jaribu kutuonesha kama idadi ya watumishi ni walewale please...
umekwapua namba ya pesa unalia nayo.... na unadai kuna ufisadi....
Base ya hiyo ni idadi ya watu, promotions etc.... Please tuongezee nyama tujadili
Kama idadi ya watumishi ni ile ie ntaungana nawe kuuita ni ufisadi
idadi ya watumishi imepungua
 
Kasahau kwamba kuna walio panda madaraja na mishahara imebadilishwa, anasahau kwamba kuna waajiriwa wapya kada mbalimbali na wapo kazin tuwe wafuatiliaji wa mambo jamani tusiwe watu wa kutafuta lawama wakati wote
Mmmh wamepandishwa madaraja? Serious? Tanzania? Tuliambiwa nyongeza haipo tangu 2015 wakapandishwaje madaraja tena wakati flyover bado?

Ukiwa upande wa utetezi nahisi unaota makengeza both machoni na kwenye ubongo!
 
Si kweli rejea sheria ya utumishi wa umma na kanuni zake, kwa mfano mtumishi amepata nafasi ya uteuzi halafu akatumbuliwa mshahara wake hadi kwenye cheo cha principal ambacho mshahara wake ni tsh 2,300,000/, na akitokea aliyetumbuliwa hakuwahi kuwa mtumishi ,mshahara unakoma mara moja.

Wale wakurugenzi wa awamu ya jana walikuwa watumishi na bado ni watumishi, Makatibu wakuu pia
 
Back
Top Bottom