N.H.C ziko wapi nyumba za gharama nafuu?

ibanezafrica

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,261
6,552
Miaka ya 70s nilikulia magomeni na ilala tukiishi katika nyumba za NHC,enzi hizo baba na wajomba wakiwa wafanyakazi wa kawaida walizimudu nyumba hizo tukaishi miaka mingi.

Leo hi nyumba za sgirika hilo sifikirii hata kuzisogelea kwa gharama kubwa ambazo ya chini inatajwa kua ni almost milioni 30!Maswali yangu kwenu Nhc Ni lini mtarudia kupangisha watu wa kawaida/wa hali ya chini ktk nyumba zenu?na kwanini bei yenu bado ipo juu na bado mnasema ni rahisi je rahisi hii ni kwa nani?

Zanzibar Pale Michenzani Karume alijenga Flats zile hadi leo wapo wananchi wa kawaida mle je kwenu hilo haliwezekani?
 
Mbona mnalalamika sana, bei nafuu bei nafuu khaaa... kwani lazima uishi kwenye hizo nyumba?
Acha wenye uwezo waishi kwenye hizo nyumba
 
hiii nchi wezi hawaishi hiii magu atatumbua eeeeeh mpaka ataingia mwingine atawakuta tu ukiziona wanavyozisifia utafikiri kuna vyakula ndani mil.35? mwl mfanyakazi kada ya chini mwenye certificate daraja IIIA ,ni ndito kuimiliki.
 
Ni wazi kwa jinsi wanacyozitangaza hazina wateja, watanzania walio wengi maisha yao ni ya chini jambo ambalo Mwl Nyerere aliliona...Zitadoda hizi wasipo shusha bei
 
Miaka ya 70s nilikulia magomeni na ilala tukiishi ktk nyumba za NHC,enzi hizo baba na wajomba wakiwa wafanyakazi wa kawaida walizimudu nyumba hizo tukaishi miaka mingi,
Leo hi nyumba za sgirika hilo sifikirii hata kuzisogelea kwa gharama kubwa ambazo ya chini inatajwa kua ni almost milioni 30!Maswali yangu kwenu Nhc Ni lini mtarudia kupangisha watu wa kawaida/wa hali ya chini ktk nyumba zenu?na kwanini bei yenu bado ipo juu na bado mnasema ni rahisi je rahisi hii ni kwa nani?Zanzibar Pale Michenzani Karume alijenga Flats zile hadi leo wapo wananchi wa kawaida mle je kwenu hilo haliwezekani?
Kuwa na subira mkuu, siku ukianza kulipwa mshahara waliokua wanalipwa baba na wajomba zako, miondombinu ikiwa kama ilivokua wakati wa baba na wajomba zako, hospitali na idadi ya watu ikiwa sawa na wakati huo basi bila shaka na nyumba za nhc zitakua gharama unayoitaka.
 
Mi sielewi gharama ndogo mnazotaka ni zipi,toeni mawazo mnataka gharama kiasi gani. afu umu kuna watalaamu wa ujenzi watatufafanulia kama hizo gharama zinawezekana. ila tukumbuke nyumba sio masabuli kwamba kila mtu awenayo.
 
Mbona mnalalamika sana, bei nafuu bei nafuu khaaa... kwani lazima uishi kwenye hizo nyumba?
Acha wenye uwezo waishi kwenye hizo nyumba
Mkuu Root NHC wanafanya usanii wa kucheza na maneno,kama dhumuni ni sisi kuacha waishi wenye uwezo then wasiseme ni za bei nafuu,wanatangaza eti "wahi nyumba za bei rahisi"ukijipendekeza unaambiwa nyumba yenye room 2,sebule na choo 40mill Mtanzania maskini ataiweza hiyo bei..em waache usanii.
 
Mkuu Root NHC wanafanya usanii wa kucheza na maneno,kama dhumuni ni sisi kuacha waishi wenye uwezo then wasiseme ni za bei nafuu,wanatangaza eti "wahi nyumba za bei rahisi"ukijipendekeza unaambiwa nyumba yenye room 2,sebule na choo 40mill Mtanzania maskini ataiweza hiyo bei..em waache usanii.

tofautisha kati ya nafuu na masikini, maskini hana nafuuu ila kwa mwenye nacho
 
kuna siku nilikua natazama kipindi chao tv wakaonyeshwa wateja 2 wakikabidhiwa nyumba mmoja wao akiwa aliyewahi kuwa waziri ndg Nazir Karamagi
 
Back
Top Bottom