N.B.C Limited Kugoma 22.02.2010

Sumbalawinyo

JF-Expert Member
Sep 22, 2009
1,282
247
Wafanyakazi wa Benki ya Taifa ya biashara wataingia msituni siku ya Jumatatu ya tarehe 22.02.2010 kugomea utaratibu mbovu unaotumiwa na menejimenti ya benki hiyo kwenye suala zima la kugawa mgao wa bonus na nyongeza ya mishahara.
katika kikao cha wafanyakazi wa NBC LTD na FIBUKA (chama cha kutetea haki za wafanyakazi wa taasisi za fedha) kilichofanyika jana Mhasibu House, wameulaumu uongozi huo kwa kuwapendelea baadi ya wafanyakazi kwa kuwapa bonus nzito na kuwaacha wengine wakiwa hoi kwa kuambulia tu vijihela tusito tosha hata kununua gurudumu la bajaji.
FIBUKA wanataka washirikishwe kwenye mchakato mzima wa bonus na kinyume cha hapo basi mgomo utarindima.
Bonus na mishahara mipya vimepangwa kutolewa tarehe 18.02.2010
 
poleni sana, mipaka ya wanyonyaji imo mikononi mwa wanaonyonywa, ila ni lazima wanaonyonywa watambue haki zao, na wachoke kunyonywa.
 
Back
Top Bottom