Mzunguko wa maisha...

Mzunguko wa maisha...

msakhara

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2019
Posts
297
Reaction score
405
Maisha ya mtanzania wa kawaida yamekua na mzunguko unaoelekeana sana. Anazaliwa, anakua, anasoma, anapata kazi/biashara, anaoa (anaanza kulalamika majukumu mengi ya familia, anahangaika na kipato na kumridhisha mke na watoto). Anasomesha, anazeeka, anaanza kuwategemea watoto wake.

Swali huwa nnajiuliza, ni kweli tuliumbwa ili tufwate cycle fupi namna hii? Furaha ya wanaume wengi hupungua miaka kadhaa baada ya kuoa na kuwa na familia, je kunaumuhimu gani wa mzunguko huu?

Mwanaume anasomeshwa na kulelewa kwa nguvu mzunguko wake unampelekea kwa mwanamke anayeamini mwanaume bila fedha si mtu na baadaye watoto wanaoamini baba yao ni insignificant. Mwanamke anasomeshwa kwa nguvu huku akiaminishwa yy ni mtegemezi by nature.

Je, tuliumbwa tuifwate hii cycle au tunajiweka wenyewe?
 
Asilimia kubwa ya sisi tumekua tukiongozwa kwa kuangalia familia zetu zilivyokua tangu tumezaliwa, pili tumekua tunaongozwa sana na taratibu za Dini, kama unadhani unaweza ukatengeneza KAsystem kako mwenyewe try it, but i'm sure hadi sasa umeshachelewa, nadhani unaviishi vilivyo kukuza.
 
Hapana

Kila mtu anachakua kuishi atakavyo, maisha unayatengeneza wewe mwenyewe
Kuna ambao hawataki kuoa wala kuolewa
**** ambao wanataka kuoa na kuolewa
N.k
Amua wewe mwenyewe unataka maisha yako yaweje.
 
Asilimia kubwa ya sisi tumekua tukiongozwa kwa kuangalia familia zetu zilivyokua tangu tumezaliwa, pili tumekua tunaongozwa sana na taratibu za Dini, kama unadhani unaweza ukatengeneza KAsystem kako mwenyewe try it, but i'm sure hadi sasa umeshachelewa, nadhani unaviishi vilivyo kukuza.
Ndio, uko sahihi....mkuu, usipoidisrupt ww unaweza wasaidia wanao waidisrupt
 
Ndio maana vijana wengi hawataki mahuano rasmi wanaishia kuzaa na kuzalishana, wanaliongezea taifa mzigo mwingine wakidhani wanatafuta HAPPYNESS kwa kuwa singo
 
Sawasawa...wanakwepa habari za kulea watoto nguvu zimeisha unaanza kuilaumu serikali, laumu majukumu,laumu wazazi etc
 
Ndio maana vijana wengi hawataki mahuano rasmi wanaishia kuzaa na kuzalishana, wanaliongezea taifa mzigo mwingine wakidhani wanatafuta HAPPYNESS kwa kuwa singo
Mzigo kivipi? Wanakua wanazaa bila uwezo wa kuwalea?
 
Ninachopendea waTanzania ni kula
Unazaliwa-tunakula
Unaenda shule-tunakula
Unamaliza shule tunakula
Unapata kazi tunakula
Unakufa tunakula
Tukikukumbuka tu--tunakula
What a nice cycle.
 
Back
Top Bottom