Na hili ndilo linalowawia vigumu ccm kuiongoza nchi kwani awali ilikuwa ikiongoza waoga na wajinga na sasa ni wasomi na wajanja mtaacha kutoka madarakani kweli?
Mkuu habari ya asubuhi!ngojanikusalimu kwa salamu hii ,kidumu chama tawala na zidumu fikra za mwenyekiti daktariNa hili ndilo linalowawia vigumu ccm kuiongoza nchi kwani awali ilikuwa ikiongoza waoga na wajinga na sasa ni wasomi na wajanja mtaacha kutoka madarakani kweli?
Du embu tusikie baadae wangapi watadondokewa na vitu vyenye ncha kali
wanafunzi wa kipaji maalum mzumbe wameandamana wakielekea kwa mkuu wa mkoa ili kumuelezea matatizo yao ambayo yamekuwa yakipuuzwa na uongozi wa shule na hivyo kupelekea kufungwa kwa muda barabara Morogoro lringa kabla ya kuzuiwa na askari.source redio one breaking news
umepotoshwa mkuu walipanga kwenda kwa mkuu wa mkoa morogoro sio dodoma
kila mahali mandamano kweli nchi haitawaliki
Unafikiri kwa kupotosha napata faida yoyote? Mleta habari, niko katika jumuiya husika ingawa sifanyi kazi hapo. Unasikiliza sehemu ya ujanja wa wanafunzi hao kutoka redio one Dar na unaamini huku ukiniona mleta habari toka eneo la tukio napotosha watu na huniamini! Poa!
Ni nyuma kidogo ya Kasanga, Maliasili. Matatizo yao ni mengi. Ujue shule ya Mzumbe ni ya siku nyingi, imechoka! Na Headmaster, Njawa, ni kijana na hana uwezo wa kuwavuta wakubwa huko serikalini ili waendelee kujali shule hiyo. Hivyo matatizo yaliopo Mzumbe ni makubwa kuliko umri wa huyo headmaster. Na serikali inataka kuziweka shule zote kuwa za kata kwa ukata! Inaumiza hata shule zake za wanafunzi wenye vipaji?! Bogus government!
Du embu tusikie baadae wangapi watadondokewa na vitu vyenye ncha kali
Shule yetu Mzumbe secondary...
Yasifika kote Tanzania,
Malezi ya Mzumbe,elimu yake,ni kamilifuu ya Kitanzania,daima mbele nyumaa mwiko.
Kwa juhudi pia na nidhamu,tutaendeleza sifa zake...
Naukumbuka vizuri huu wimbo wa shule yetu pendwa.
Matatizo Mzumbe kweli yapo.
Nimeona picha za Mzumbe za hivi karibuni, hali si nzuri.
Hata hivyoi, bado sijaelewa uamuzi wa kwenda Bungeni umedhamiria vipi kutatua matatizo yaliyopo.
Je, ni kwanini wameamua kwenad leo? kwanini hawakwenda jana au kesho? Nategemea kusikia hatua mbalimbali zilozofuatwa mpaka kufikia uamuzi huo wa kwenda Bungeni.
Mara nyingi terminal exams zikikaribia kuna wanafunzia ambao wanabehave abnormally. Je, hiki ni kipindi cha mitihani ya muhula? If yes, kwanini harakati hizo zifanyike kipindi cha mitihani?