MziziMkavu Umetishaaa!!!


N

Ntiliabhose

Member
Joined
Dec 31, 2012
Messages
78
Likes
3
Points
0
N

Ntiliabhose

Member
Joined Dec 31, 2012
78 3 0
Habari! Jamani Kati ya watu ninaowapa BIG RESPECT humu Jf ni huyu jamaa.

Nilikuja na Uzi wangu hapa kuomba USHAURI kuhusu mambo ya ujauzito nashukuru mzizi mkavu ushauri wako jinsi ya kupunguza uchungu wakati wa kujifungua,umenisaidia sana sababu nilikuwa mmoja wa wadada wanaoogopa sana uchungu.na weng wanachagua hata kupasuliwa kuliko ku-push

Niliingia leba nikiwa na ujasiri wa ajabu kulingana na somo ulilonipa,pamoja na uchungu mkali nilivumilia na nkafanikiwa kujifungua mtoto wa kike.

Mwisho nawashukuru member wote mlionishauri jinsia ya kujiandaa,kutokana na shughuli niliyoiona leba natumia fulsa hii kuwapongeza wadada na wamama wote mliojifungua kwa kupush. Pia namuheshimu mama miaka MIA 8

Being a mother is a great experience
 
A

Aine

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Messages
1,607
Likes
10
Points
0
A

Aine

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2010
1,607 10 0
hongera sana, uwe na afya njema wewe na mtoto na umlee ktk maadili ya kumjua Mungu
 
KakaJambazi

KakaJambazi

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2009
Messages
16,229
Likes
4,624
Points
280
KakaJambazi

KakaJambazi

JF-Expert Member
Joined Jun 5, 2009
16,229 4,624 280
Ushauri ulikuaje? Mbona nasikiaga mwanamke asipokua na uchungu wakati wa kujifungua huwa anapewa dawa za kumpa uchungu?
 
N

Ntiliabhose

Member
Joined
Dec 31, 2012
Messages
78
Likes
3
Points
0
N

Ntiliabhose

Member
Joined Dec 31, 2012
78 3 0
Ushauri nilopewa ulikuwa wa kisaikolojia zaidi.uchungu uko palepale na huwezi kupush bila huo uchungu.
 
steveachi

steveachi

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2011
Messages
5,032
Likes
2,726
Points
280
steveachi

steveachi

JF-Expert Member
Joined Nov 7, 2011
5,032 2,726 280
mi nilijua wengi wanao-opt kutumbuliwa ni kwa sababu wanatoa sana mtandao wa kabaang,kumbe wengine wanapenda wenyewe wanaogopa kuckia uchungu
 
Lovebird

Lovebird

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2012
Messages
2,538
Likes
355
Points
180
Lovebird

Lovebird

JF-Expert Member
Joined Sep 27, 2012
2,538 355 180
Big up Kwa ku-push yaelekea NYONGA bado iko fit! congrats for having a baby

Ila mi huwa nasikia muda wa ku-push endapo 0713/714 etc ka misuli haina ukakamavu huwa ni MAJANGAAAAAA
 
N

Ntiliabhose

Member
Joined
Dec 31, 2012
Messages
78
Likes
3
Points
0
N

Ntiliabhose

Member
Joined Dec 31, 2012
78 3 0
Big up Kwa ku-push yaelekea NYONGA bado iko fit! congrats for having a baby

Ila mi huwa nasikia muda wa ku-push endapo 0713/714 etc ka misuli haina ukakamavu huwa ni MAJANGAAAAAA
Yes naskia Inabidi wawekewe pamba huko kwenye kabang ili kumsaidia mama kujifungua.so wanakimbilia kisu kuepuka fedheha!
 
N

Ntiliabhose

Member
Joined
Dec 31, 2012
Messages
78
Likes
3
Points
0
N

Ntiliabhose

Member
Joined Dec 31, 2012
78 3 0
Kwani MziziMkavu alikushauri nini?
Kuna uzi wa mzizi mkavu unasema jinsi ya kupunguza uchungu wakati wa kujifungua,kwa ujumla ni namna ya kukabiliana na ule uchungu,mzizi ukikatiza hapa naomba tupia ule link wadau waicheki wenda mtasaidia wengne
 
neggirl

neggirl

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2009
Messages
4,828
Likes
94
Points
145
neggirl

neggirl

JF-Expert Member
Joined Jul 30, 2009
4,828 94 145
Mzizi mkavu njoo huku.. na invoice faster!
 
Last edited by a moderator:
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
40,026
Likes
5,488
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
40,026 5,488 280
Mzizi mkavu njoo huku.. na invoice faster!
Mkuu neggirl
[h=1]Jinsi ya kuufanya uchungu wa kujifungua ustahimilike[/h]Labda unawaza kuhusa uchungu utakaopata wakati wa kujifungua. Kuna mambo unayoweza kufanya ili uchungu huu ustahimilike.

 • Kutumia njia za kujipumzisha na kuvuta hewa
 • Dawa za kudungwa mishipani
 • Sindano itakayopunguza uchungu upande wa chini wa mwilio
 • Dawa ya kupunguza maumivu (anaesthesia) hasa unapotumia kibanio
 • ‘Pudenal Block' itakayo maliza hisi kwa uke na mwaranda.

Daktari wako atakusaidi kuchagua ni njia ipi nakufaa zaidi.

[h=1]Kujifungua/uchungu wa kujifungua[/h]Katika wiki zako za mwisho za mimba, mji wako mimba (uterus) utaanza kurudiana kujikunja. Hii huita Braxton-Hicks Contractions (au uchungu wa kujifungua usio wa kweli) na huwa wa kawaida. Kwa sana hili hutokea ukikaribia kujifungua, ni vigumu kwa wanawake wengi kujua kama ni uchungu wa kweli au usio wa kweli.

Ongea na daktari wako kama:

 • Unapata mikunjano hii (contractions) baada ya sekunde 30-70, inaendelea bila kukoma na inaendelea kuwa mikali zaidi.
 • Unaumwa na sehemu ya chini ya mgongo na uchungu huu haukomi.
 • Hata kama uchungu wa kujifungua huwa tofauti, huwa na awamu tatu kwa kawaida.

Awamu ya kwanza
Hiki kipindi ndicho hukoa sana. Huanza wakati mlago wa uzazi huanza kuwa mwembamba na kufunguka. Ule ulio na damu huanza kutoka ukeni (‘show'). Karibu na mwisho wa awamu hii mikunjano huu huana mikali zaidi na huchukua muda mrefu pia.

Awamu ya pili
Mlango wa uzazi hufunguka kabisa na mtoto anahitaji usaidizi ili atoke. Utahitajika kumsukuma mtoto ili atoke wakati wa mkunjano hadi mtoto atakapotoka. Awamu hii inaweza kukaa hata masaa mawili au zaidi hasa kama ni mara yako ya kwanza.

Awamu ya tatu
Baada ya kujifungua utaendelea kupata mikunjano ili kito ‘placenta'. Mikunjano hii huja ikikaribiana zaidi kuliko ile ya kabla hujajifungra lakini haina uchungu kama ya awali. Awamu hii inaweza kukaa kwa dakika chache na kukaa kwa dakika 15-20.

Baada ya kujifungua utachungwa kwa uangalifu mwingi ili kuhakikisha hauna matatizo yoyote. Joto la mwili wako, mpigo wa moyo, kupumua na mwendo wa damu zitachunguzwa mara kwa mara. Katika wakati huu, unaweza kuanza kumjua mtoto wako. Kama ulikuwa umepanga kumnyonyesha mwanao unaweza kuanza wakati huu.


[h=1]Majonzi baada ya kuzaa[/h]Wiki moja baada ya kujifungua unaweza kuanza kupata mabadiliko ya tabia (furaha na hasira) yanayo sababishwa na mabadiliko ya ‘Hormone', uchovu na mahangaiko kwa sababu ya mtoto wako kukufanya ukasirike. Haya ni matukio ya kawaida na hutoweka baada ya wiki chache.

Kwa matukio mengine, wanawake huhuzunika hata wanashindwa kujitunza na kutunza watoto wao. Haya majonzi huitwa 'Post natal' au 'Post partum depression'. Kama kukasirika huku kutaendelea kwa zaidi ya wiki mbili au kama una yafuatayo, hakikisha umemwona daktari wako:

 • Haupati usingizi au unakasirika haraka
 • Una huzuni, umekasirika na unakaa ukilialia
 • Hauna nguvu
 • Unaumwa na kichwa na kifua unapumua harakaharaka, moyo wako unapiga kwa kasi au unasikia kama moyo unaruka midundo Fulani.
 • Haukuli au unakula sana
 • Haufikirii vizuri, haukubuki mambo au hauwezi kufanya uchaguzi
 • Hauna hamu tena ya uliokuea unapenda kama kufanya mapenzi
 • Haupati shughuli na mtoto wako
 • Unajisikia kama hauna maana tena na unajihurumia
 • Unaogopa utamuumiza mtoto au utajiumiza

[h=1]Njia zingine za kukusaidia unapojifungua[/h]Wanawake wengi hujifungua kupitia kwa mlango wa uzazi, lakini wakati mwingine njia zingine huhitaji ili kisaidia kujifungua.

 • Kibanio (forceps) - Kifaa hiki hukaa kama vijiki viwili. Daktari hukiweka kwenye uke kasha anakishikisha kwenye kichwa cha mtoto na kumvuta mtoto kwa utaratibu ili atoke.

 • ‘Vacuum'- Kikombe cha plastiki huwekelewa kwenye kichwa cha mtoto kwa kutumia bomba la ‘vacuum' mtoto anavutwa taratibu baadaye.

 • Upasuliwaji - Mama mtoto hukatwa tumbo na mji wa mimba ili kumtoa mtoto (caesarean section) 
Last edited by a moderator:

Forum statistics

Threads 1,273,282
Members 490,351
Posts 30,476,855