Mzizima, Tanga: Watu 8 wauawa kwa kuchinjwa shingo na watu wasiojulikana

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
20,404
24,990

‪Watu kadhaa wa kijiji cha Mikocheni karibu na mapango ya Amboni mkoani Tanga wameuawa usiku wa kuamkia leo.

Inasemekana watu waliouawa wanadaiwa kufichua vitendo vya uhalifu kijijini hapo na kwamba miili ya watu hao waliouawa imepelekwa hospitali ya rufaa ya Mkoani humo.

Mya take : Ulinzi shirikishi unaweka rehani maisha ya raia wema.
 
Watu kadhaa wa kijiji cha Mikocheni karibu na Mapango ya Amboni mkoani Tanga wameuawa usiku wa kuamkia leo kwa kile kinachodaiwa kufichua vitendo vya uhalifu vya baadhi ya watu kijijini hapo.

================
Jana nilikuwa nasikiliza taarifa ya habari, sasa huko Kigoma wanakijiji wanalalamika kuwa kila watoapo taarifa kama watu wema, askari waendapo kuwakamata wahalifu usema ''Asingekuwa fulani sisi tusingejua kama una bunduki/silaha''

Kauli hizo zimesababisha matatizo ya uhasama na wanakijiji wamesema endapo polisi wataendelea kutoa siri za wafichua uovu basi hawatashirikiana nao.

Hapo nilishindwa kuelewa ufanyaji wa kazi wa hao polisi, hawajui huo upuuzi wao unaongeza uhasama kwa wanakijiji na kupelekea mauji na uhalifu usiokuwa na msingi.

Tukirudi Tanga, naona itakuwa vile vile tu (Kumradhi),

Ombi langu kwa polisi: Sisi Raia wema tunapotoa taarifa kama hizi za uhalifu lazima mjua tumechoshwa na vitendo hivyo, tunajua majambazi na wahalifu wengine wana mitandao mikubwa, mnapotoa utambulisho wetu mnatuweka kwenye mazingira ya hofu zaidi. Ni nyema mkafanya kazi kwa weledi mkubwa na sio kutafuta sifa.
 
Hii mbaya sana Jeshi la polisi wachunguze kwa umakini kuwabaini wale wote wanaofanya vitendo hivyo vya kidhalimu
 
yaan jeshi la polisi hovyo sana wakiwa wanataka taarifa za wahalifu wanatubembeleza tuzitoe kwao tukizitoa inakula kwetu tunafirimbwa vibaya sana
 
Watu 8 katika kijiji cha Mikocheni karibu na mapango ya amboni Tanga wameuawa usiku wa kuamkia leo kwa kukatwa na mapanga.

Wahalifu hao baada ya kuwakatakata na mapanga walitokomea msituni na katika mapango ya amboni.

Inasemekana watu waliouawa wanadaiwa kufichua vitendo vya uhalifu kijijini hapo na kwamba miili ya watu hao waliouawa imepelekwa hospitali ya rufaa ya Mkoani humo.
 
Watu 8 katika kijiji cha Mikocheni karibu na mapango ya amboni Tanga wameuawa usiku wa kuamkia leo kwa kukatwa na mapanga.

Wahalifu hao baada ya kuwakatakata na mapanga walitokomea msituni na katika mapango ya amboni.

Inasemekana watu waliouawa wanadaiwa kufichua vitendo vya uhalifu kijijini hapo na kwamba miili ya watu hao waliouawa imepelekwa hospitali ya rufaa ya Mkoani humo.
Mkuu dadavua vizuri mbona habari nusu nusu japo kuwa inaogopesha Sana, mbona haya matukio yanazidi kila kukicha?
 
Jana nilikuwa nasikiliza taarifa ya habari, sasa huko Kigoma wanakijiji wanalalamika kuwa kila watoapo taarifa kama watu wema, askali waendapo kuwakamata wahalifu usema ''Asingekuwa fulani sisi tusingejua kama una bunduki/silaha''

Kauli hizo zimesababisha matatizo ya uhasama na wanakijiji wamesema endapo polisi wataendelea kutoa siri za wafichua uovu basi hawatashirikiana nao.

Hapo nilishindwa kuelewa ufanyaji wa kazi wa hao polisi, hawajui huo upuuzi wao unaongeza uhasama kwa wanakijiji na kupelekea mauji na uhalifu usiokuwa na msingi.

Tukirudi Tanga, naona itakuwa vile vile tu (Kumradhi),

Ombi langu kwa polisi: Sisi Raia wema tunapotoa taarifa kama hizi za uhalifu lazima mjua tumechoshwa na vitendo hivyo, tunajua majambazi na wahalifu wengine wana mitandao mikubwa, mnapotoa utambulisho wetu mnatuweka kwenye mazingira ya hofu zaidi. Ni nyema mkafanya kazi kwa weledi mkubwa na sio kutafuta sifa.
 
Shule,..shule,..shule ndogo ndio tatizo...maake haiwezekan mtu aripoti police kuhusu uhalifu....halafu baadae vyombo vya usalama vikaseme fulan ndio katuambia.
 
Sijakuelewa hapa, shule, unakanusha kuwa polisi hawawezi toa siri baada ya kupewa ripoti, ama polisi hawana shule ndiyo maana wanatoa siri, au wananchi wanakwenda kuripoti polisi ndiyo hawana shule. Hebu fafanua nua kidogo, maana maswala mengine hayahitajiki elimu ya darasani.
 
Back
Top Bottom