Kama kumshambulia rais ndio sifa kuu ya utendaji kwa Tanzani; serikali ije JF na itapata washambuliaji wengi ambao wataweza kuliokoa taifa letu.
Watu wamepewa nafasi na wameshindwa, hao ndio tunaimba wanafaa kwasababu tu wamemshambulia rais? Give me a break! I will be the last one to buy into such argument.
na ukifika uchaguzi mkapige kura kweli sio blahblah tu.- Tatizo ni kwamba vijana nao wamepewa nafasi wameshindwa, na mimi mkuu kama wewe nitakuwa mtu mwisho kumpa mtu kura eti kwa sababu ni kijana tu hayo ni mawazo ni mufilisi sana in the wake ya vijana kama Serukamba, nilifikiri tutaona aibu hata kusema maneno ya vijana tena!
Respect.
FMEs!
- Tatizo ni kwamba vijana nao wamepewa nafasi wameshindwa, na mimi mkuu kama wewe nitakuwa mtu mwisho kumpa mtu kura eti kwa sababu ni kijana tu hayo ni mawazo ni mufilisi sana in the wake ya vijana kama Serukamba, nilifikiri tutaona aibu hata kusema maneno ya vijana tena!
Respect.
FMEs!
Kama kumshambulia rais ndio sifa kuu ya utendaji kwa Tanzani; serikali ije JF na itapata washambuliaji wengi ambao wataweza kuliokoa taifa letu.
Watu wamepewa nafasi na wameshindwa, hao ndio tunaimba wanafaa kwasababu tu wamemshambulia rais? Give me a break! I will be the last one to buy into such argument.
sijui ni nani aliyemention vijana akiashiria calibre ya akina Rostam, Masha Ngeleja. Ndulu na akina Serukamba..........walioshindwa/Wezi........
......hao vijana ukiangalia waliingiaje mpaka kufikia hapo walipo.....utaona/utajua........ni kwanini tumepata matokeo mabovu kutoka kwao..............
Sidhani kama kuna mwana JF ambaye atakimbilia kutaja majina ya hao vijana waliopitia kwenye System mbovu/iliyooza.......na bado wakachemsha eti ndio vijana wa kujivunia........
.........nobdoy hata Mkuu wangu Kasheshe siku hizi kabadilika........anamkoma Nyani kwa kwenda mbele..........
..........alikuwepo Zitto hapa JF........tulipomuona kachemka...wanaJF tulimshukia......hapendwi mtu....hapa....
Back to mada
........Wazee Kimiti na Mzindakaya wanaelekea kustaafu.......their action is plausible.......sasa watu wanapowashauri vijana waingie sidhani kama wana maana ya akina "Nungwi" or dizaini ya Rostam/Masha/Ngeleja/Serukamba waingie pale............
Tunataka watu wanaoelewa i.e wenye uwezo na uzalendo waingie kwenye kinyang'anyiro cha kuchukua hizo nafasi.......ili KUTUMIKIA wananchi wa hayo majimbo...........
Now the question comes back........how do we eliminate the Kinjes/Hizas type and Mzindakayas type.............CCM machinery failed us miserably.........give us your ideas Mkuu.........how?
- Siwezi kurudia rudia mkuu, mimi sina tatizo na wazee wala vijana, ninachotaka viongozi wenye uwezo ambao so far kwenye vijana na wazee tulionao hatunao, sasa what to do labda wewe ndio ungesema otherwise inachosha sana kurudia ruida yale yale!
Respect.
FMEs!
Nami sipendi kurudia rudia....isipokuwa kwenye hili siwezi kuachia watu mediocre wakitetewa............
- Mediocre wanaotetewa ni nani hapa? Viongozi waliotufikisha hapa tulipo in the last five years ni vijana, sasa kama ni mediocre ni taifa zima kuanzia viongozi mpaka wananchi hakuna wa kumlaumu mwingine!
tumependekeza njia mojawapo ya kupata viongozi ni kuwapa back nguvu yao wananchi........na sio uporaji wa demokrasia wa sasa hivi......watu waachiwe wachague....na wakitaka kuwawajibisha....the bucks stops to wananchi.......unlike sasa hivi tukisema the backs stops kwa wananchi tunawaonea..........
- Mimi simjui kiongozi yoyote mzee au kijana sasa hivi aliyepora uongozi kwa nguvu, wanaweza kuwa wametumia ujanja ujanja, lakini kupora hapna tusingekwua na viongozi wa upinzani bungeni, nani atawapa nguvu wananchi kama vijana wenyewe ndio hawa wamefilisi taifa, wazee waliwapa taifa likiwa na neema sasa imekwua ni kila kijana kupora tu, ndio hatuelewi tunapoambiwa eti vijana ndio wanafaa labda kwa wizi hilo kweli, lakini uongozi ni bure kabisaa!
- Na kinchosikitisha sana ni kwamba viongozi wetu ni reflection yetu wenyewe yaani wananchi wa Tanzania, sasa hapa nani wa kumlaumu mwingine ndio ninashindwa kuelewa!
One way ni Independent Candidates should be allowed........
- Hii inahitaji topic yake, hapa kwenye vijana na wazee sio mahali pake!
Respect.
FMEs!
- Mediocre wanaotetewa ni nani hapa? Viongozi waliotufikisha hapa tulipo in the last five years ni vijana, sasa kama ni mediocre ni taifa zima kuanzia viongozi mpaka wananchi hakuna wa kumlaumu mwingine!
........- Mimi simjui kiongozi yoyote mzee au kijana sasa hivi aliyepora uongozi kwa nguvu, wanaweza kuwa wametumia ujanja ujanja, lakini kupora hapna tusingekwua na viongozi wa upinzani bungeni, nani atawapa nguvu wananchi kama vijana wenyewe ndio hawa wamefilisi taifa, wazee waliwapa taifa likiwa na neema sasa imekwua ni kila kijana kupora tu, ndio hatuelewi tunapoambiwa eti vijana ndio wanafaa labda kwa wizi hilo kweli, lakini uongozi ni bure kabisaa!
- Na kinchosikitisha sana ni kwamba viongozi wetu ni reflection yetu wenyewe yaani wananchi wa Tanzania, sasa hapa nani wa kumlaumu mwingine ndio ninashindwa kuelewa!
- Hii inahitaji topic yake, hapa kwenye vijana na wazee sio mahali pake!
Respect.
FMEs!
Kisumo awavaa kina Malecela, awataka wasigombee ubunge 2010Mwanasiasa Mkongwe nchini Peter Kisumo ambaye amewataka wabunge wenye umri mkubwa kutogombea ubunge kwenye uchaguzi mkuu ujao
Daniel Mjema, Moshi
MWANASIASA mkongwe nchini, Peter Kisumo amewataka wabunge wenye umri mkubwa kutogombea nafasi hizo katika uchaguzi mkuu ujao na badala yake wawaachie nafasi hizo wagombea vijana.
Kisumo, ambaye ni mwenyekiti wa baraza la wadhamini wa CCM, aliwahi kutoa kauli kama hiyo mwaka 2005 alipomsindikiza Rais Jakaya Kikwete kutangaza nia yake ya kugombea urais.
Kauli ya Kisumo ya mwaka 2005 iliibua malumbano na baadhi ya wagombea, akiwemo John Malecela aliyelazimika kujibu mapigo kwa kusema hata kama ni mzee, akili yake inakata kama wembe.
Jana Kisumo alirejea kauli hiyo lakini safari hii akiwalenga wabunge na madiwani, wakati akipokea hati ya utambulisho ya kamanda mpya wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wilaya ya Mwanga, Seleman Mfinanga.
"Ni matumaini yangu kuwa safari hii wabunge wazee watawaachia vijana kwa kusema hivyo sina maana wazee hawa hawana kazi ya kufanya, wao watabaki kuwa washauri kwa vijana,"alisema Kisumo.
Kisumo aliwataka wabunge na madiwani wazee ambao wameshikilia nyadhifa hizo kwa miaka mingi kutoona nongwa kuwaachia vijana na akisisitiza kuwa kutokana na mabadiliko ya sasa, damu changa inahitajika.
Mkonngwe huyo alisema wapo vijana ambao wamejifunza uongozi na wana sifa za kuiongoza nchi kwa uadilifu mkubwa.
Alimpongeza mbunge wa Kwela, Chrisant Mzindakaya na Paul Kimiti wa Sumbawanga kuamua kwa hiyari yao kutogombea tena ubunge akisema wameonyesha mfano na akawataka wengine kuiga.
Katika Bunge la sasa, wabunge ambao wameshikilia viti vyao kwa muda mrefu ni pamoja na John Malecela (Mtera), Samuel Sitta (Urambo Mashariki) na Jackson Makwetta (Njombe Kaskazini).
Kisumo alitumia nafasi hiyo kukemea kile alichosema kuwa ni kuanza kwa kampeni zinazoegemea katika udini kwenye wilaya ya Mwanga na kuwataka wananchi kuwa macho na wagombea wa aina hiyo kwa kuwa hawafai.
"Kaeni macho, msiruhusu mtu yeyote kuwachonganisha hapo Mwanga kwa udini kwamba ooh mgombea wa dini fulani ndiye anayefaa kuwa mbunge, mtu wa iana hii ni mchochezi wa vurugu," alionya.
Mwanasiasa huyo alikemea pia kampeni za ukabila katika jimbo hilo ambako wagombea ubunge hutambulishwa kwa kutaja sehemu anakotoka, yaani ama Usangi, Ugweno au Tambarare akisema hiyo sio sifa ya uongozi.
Kisumo alifichua kile alichodai ni kuundwa kwa mabaraza ya wazee wa CCM katika tarafa mbalimbali za jimbo hilo akisema mabaraza hayo yanaundwa ili kutumika katika kampeni, lakini hayako katika katiba.
Kwa upande wake, Mfinanga, ambaye alifuatana na mwenyekiti mpya wa chipukizi wilaya ya Mwanga, Zena Salim alisema changamoto kubwa inayomkabili kwa sasa ni kupanua wigo wa ajira kwa vijana. Mfinanga ameteuliwa kushika wadhifa wa ukamanda wa UVCCM wilayani Mwanga baada ya Cleopa Msuya, aliyeshikilia nafasi hiyo kwa miaka zaidi ya 10, kuamua kungâatuka kwa hiyari.
Kwa muono wangu mitizamo kama hii inaashiria kuwa wengi tumegubikwa na hulka za ubaguzi wa kirika na jinsi gani tunapenda kutumia kauli mbiu ya UJANA kama nyenzo ya kuhalalisha uroho wetu wa UHESHIMIWA.
omarilyas
Ni muda muafaka sasa tukafikiria pia kuwa na Mabunge ya aina mbili kama Marekani ili wazee safi kabisa kama Kimiti, Makweta,... wakawa Maseneta. Kila Mkoa ukachagua Seneta mmoja na kila halmashauri ikachagua Mbunge mmoja tu kuliko utitiri wa majimbo tulionayo na hivyo kuwa na Wabunge wengi mzigo kwa uchumi mdogo wa Taifa letu. Bunge letu la sasa ni kubwa mno bila sababu yoyote ya maana mbali na watu kuwekeza kwenye siasa!