Mzimu wa Sharomilionea waanza kazi, wezi warudisha vifaa vyake

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,868
30,337


sharo.jpg

Gari aliyokuwa akiendesha Marehemu Sharomilionea baada ya kuacha njia na kupinduka

“Vitu viliwasilishwa na wasamaria wema kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Songa Kibaoni, Abdi Zawadi ambaye alitoa taarifa polisi kwa ajili ya utambuzi na taratibu nyingine,” alisema Massawe.

JESHI la Polisi mkoani Tanga limefanikiwa kukamata vitu mbalimbali vya marehemu Hussein Ramadhan, ‘Sharo Milionea’ vilivyoibwa na watu wasiojulikana, muda mfupi baada ya msanii huyo wa filamu na muziki nchini kupata ajali katika Kijiji cha Songa Kibaoni, wilayani Muheza na kufariki dunia papo hapo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Costantine Massawe alisema Jeshi la Polisi limefanikiwa kukamata begi la nguo, simu ya mkononi aina ya blackberry, betri ya gari, redio, tairi la gari na saa ya mkononi ya marehemu.

Alitaja vitu vingine vilivyopatikana kuwa ni nguo ambazo marehemu alivuliwa baada ya kupata ajali, ambazo ni fulana na suruali ya jeans.

Alisema kuwa,vitu hivyo vilipatikana baada ya wakazi wa kijiji ilipotokea ajali hiyo kuvisalimisha vitu hivyo kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Songa kibaoni, Abdi Zawadi .

“Vitu viliwasilishwa na wasamaria wema kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Songa Kibaoni, Abdi Zawadi ambaye alitoa taarifa polisi kwa ajili ya utambuzi na taratibu nyingine,” alisema Massawe.

Aliwataka wananchi wa Kibaoni kuendelea kutoa ushirikiano ili viweze kupatikana vitu vingine vya marehemu na kuongeza kuwa, jeshi hilo linaendelea na uchunguzi, ili kubaini pesa na vitu vingine vilivyokuwamo ndani ya gari hilo ambavyo havikupatikana.

“Hivi vitu mnavyoviona hapa vimesalimishwa na watu ambao huenda walishiriki katika wizi, au waliviona mahali na kwa mapenzi yao kwa marehemu wakaamua kuvirejesha,” alisema Massawe

Alisema baadhi ya vitu hivyo vilikamatwa nje ya wilaya ya Muheza katika gereji na kwenye nyumba za watu.

Kamanda alifahamisha zaidi kuwa, hadi sasa watu kadhaa wanashikiliwa na jeshi hilo kwa kuhusika na tukio hilo.

“Tunaamini kuna vitu vingi vya thamani havijapatikana, bado tunaendelea na uchunguzi kwa kushirikiana na wananchi na mtu atakayekutwa na kitu chochote cha marehemu atashtakiwa,” alisema Massawe.

Alisema Jeshi la Polisi linawashikilia watu kadhaa waliokutwa na vitu hivyo, lakini hakutaja idadi yao kwa kuwa vitu vingine havijapatikana.

“Pamoja na hayo, vitu vilikuwa vinasalimishwa usiku na wengine walivileta mchana kwa mwenyekiti wao. Hata hivyo, si kwamba mtu aliyeleta anakamatwa papo hapo, ila wale watakaokutwa navyo tutawakamata na kuwashtaki,” alisema Kamanda Massawe.
DC atoa neno

Awali Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Subira Mgalu aliliambia Mwananchi kuwa, licha ya kusalimisha vitu hivyo hakuna mtu aliyekamatwa kwa sababu washukiwa bado wako mafichoni.

“Kwa kweli hadi sasa aliyekamatwa kwa sababu washukiwa wote wamejificha,”alisema Mgalu.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kupatikana kwa vitu hivyo, kulitokana na amri aliyoitoa baada ya mazishi ya msanii huyo, kuwataka wakazi wa eneo ilipotokea ajali kuvirejesha vitu hivyo ifikapo Ijumaa saa 12.

“Nilikuwa kijijini Songa kibaoni hadi saa 5.30 usiku juzi (Jumatano) nikiwa sambamba na wakazi wa kijiji hicho ambao walipiga kura ya siri za kuwafichua waliohusika katika tukio hilo,” alisema Mgalu.

Aliwataka waliokimbilia mafichoni kurejea haraka watu wanaopatwa na ajali. Kwani lengo la Serikali ni kutaka wanaoishi kando ya barabara kuacha kuwafanyia unyama majeruhi na maiti mara zinapotokea ajali kwenye maeneo yao.
Mzimu wa Sharomilionea waanza kazi, wezi warudisha vifaa vyake - Kitaifa - mwananchi.co.tz 

Ubungo

JF-Expert Member
Apr 7, 2012
1,246
274
Mambo ya kusikitisha sana haya, na mara nyingi ajali za barabarani zikitokea huu unyama hufanyika.
 

ITEGAMATWI

JF-Expert Member
Jan 26, 2012
5,208
3,835
Watanzania tumekuwa watu wa ajabu sana sijui roho ya kikatili namna hii tunaitolea wapi!Yaani unamvua nguo marehemu na kukimbia nazo kweli?
 

Jaslaws

JF-Expert Member
May 31, 2011
6,021
5,263
Mi lawama zangu ni kwa serikali iliyopo madarakan,chanzo cha yote ni umasikin ulokidhli w2 walionao.
 

Watu8

Platinum Member
Feb 19, 2010
61,352
66,296
Mkuu kichwa cha habari naona kama umekiweka kiimani zaidi, wakati ndani ya taarifa tunaona kumbe kuna wito uliotolewa na Mkuu wa Wilaya kusisitiza watu kuvirejesha vifaa na mali zote zilizoibwa.

"Mkuu huyo wa wilaya alisema kupatikana kwa
vitu hivyo, kulitokana na amri aliyoitoa baada
ya mazishi ya msanii huyo, kuwataka wakazi
wa eneo ilipotokea ajali kuvirejesha vitu hivyo
ifikapo Ijumaa saa"
 

THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
14,785
9,623
Sasa wanamvua nguo marehem ili ziwasaidie nin??na usikute zimelowa damu kutokna na ile ajali,,au ndio mambo ya ushirikina tena,ukatili huu umepitiliza sana

pumzika kwa amani mpendwa marehemu,,sisi tutafuata,safari hii yetu sote
 

elmagnifico

JF-Expert Member
Jul 7, 2011
8,266
9,654
naona siku hizi jf imekuwa sehemu ya kupost post zenye vichwa vya habari za magazeti ya shigongo. Baadae utasikia mzimu wa sharobaro unamtesa king majuto, mara imebainika mbaya wa sharobaro ni flani....

Back to the topic siku hizi binadamu tumepoteza utu, inapotokea ajali iwe ya gari, au moto watu badala ya kusaidia ukimbilia kupiga picha wakapost kwenye social networks na viblogs uchwara vyao, wengine ndo ukimbilia kuiba
 

Tayana-wog

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
17,764
15,395
naona siku hizi jf imekuwa sehemu ya kupost post zenye vichwa vya habari za magazeti ya shigongo. Baadae utasikia mzimu wa sharobaro unamtesa king majuto, mara imebainika mbaya wa sharobaro ni flani....

Back to the topic siku hizi binadamu tumepoteza utu, inapotokea ajali iwe ya gari, au moto watu badala ya kusaidia ukimbilia kupiga picha wakapost kwenye social networks na viblogs uchwara vyao, wengine ndo ukimbilia kuiba

Hili nalo neno
 

ha ha ha

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
638
83
sasa hapo jeshi limekamata au vitu vimesalimishwa? au umaarufu kunuka tu apo? kama tukio ni kukamatwa lingeambatana na kukamatwa washukiwa. awa jamaa wa polisi wanatuchanganya na kauli zao, wajifunze kureport..
 

snowhite

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
17,377
22,819
shemeji Nicas Mtei ilibidi uichukulie hatimiliki ile thread ujue!
yani hapa hujatumia akili ya kule rombo kabsa yani!
 
Last edited by a moderator:

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom