Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,259
- 20,914
Siku hizi vijana ambao hawajaoa wamekuwa wakisema kuwa mwenza wanaemhitaji wanataka awe hivi au vile ili kujiridhisha
Dhana hii inatokana na dhana nyingine ambayo vijana tumejijengea kuwa ukiwa na mtu wa aina fulani utaifurahia ndoa wakati hata ndoa yenyewe hatuijui,matarajio haya ndio ambayo yanasababisha vijana wengi kuja kuiona ndoa kama uongo ambao umekuwa ukihubiriwa sana na watu ambao umri umekwenda kwani hakuna raha na furaha ambayo imekuwa ikisemwa
Wakati vijana tukiilaani ndoa tunakuwa tumejisahau sana kuwa tulijenga maamuzi yetu kwenye dhana ambazo wala hatukuwa na ushahidi wowote kama zina ukweli wowote
Maisha ni mchezo ambao mara nyingi unaweza kumfanya mtu ajikute mahali ambapo anaweza kuwalaumu sana waliomleta duniani au kuwasifia
Vijana hawa ambao wamekuwa wakitarajia matamu mengi wenye ndoa au uhusiano na mtu mwenye sifa ambazo alidhani zinamsaidia kuyafanya mahusiano hayo kuwa matamu,mambo yanageuka na kuwa kinyume,anatendwa...
Hapo maisha hubadilika na kuwa mengine,kijana huyu anaishi kwenye hofu nyingi sana za kutendwa hadi anauharibu ujasiri wake kwenye mahusiano na kuanza kuwa mwoga wa kutendwa
Kitendo hiki kinamfanya kijana huyu kuanza kuchagua sana watu wa kuwa nae kwenye mahusiano huku akiwa hajiamini kwa kuandamwa na mzimu wa kutendwa na mtu wake wa mwanzo
Kufikia hatua hii kijana huyu hawezi tena kujisimamia,anaanza kuwa mtu wa kulaumu tu
Ni kweli kuwa sasa kutafuta mke wa kuoa au mume ni kazi ngumu pengine sawa kabisa na kutafuta hela,lakini kwa ambae tayari ametendwa na anaishi kwa kufuata maumivu ya kutendwa ni ngumu zaidi mara dufu
Inafikia mahali mtu hajiamini tena na anaweka sana masharti kiasi kwamba mtu ambae anakuwa nae kwenye mahusiano anaona kama yupo jela ndogo
Mwenza wake akitoka bila kuaga ni ugomvi,anawaza kaenda kufanya kama ya yule aliyemtenda,akichelewa kazini hivyo hivyo,akipokea simu na kutoka nje nako ni hivyo hivyo
Watu hawa wanakuwa wanayafanya maisha na mahusiano yao mapya kuwa magumu wenyewe kwasababu wanakuwa hawaamini tena wenzao na kuona kila mmoja ni mkosaji
Jifunze kujifunza na kuwaamini wenzako
Ukipita barabara hii na ukaporwa simu haina maana kuwa kila siku ukipita barabara hiyo au nyingine utaporwa pia!