Mziki wetu Unapotea kwasababu ya Team

Mziki wetu Unapotea kwasababu ya Team

Hakuna cha timu wala nini, tatizo hasa ni hawa wasanii wa kibongo kuishabikia CCM kwenye kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka jana 2015. Kuanzia Diamond, Kiba, Raymond, Vanessa mpaka Ya moto band walikuwa busy kwenye majukwaa ya kampeni za CCM wakipiga push up na kumdhihaki Lowassa, wakidhania watanzania wote ni wajinga tu.

Wengi wetu tuliapa kamwe hatutawapigia kura tena hawa wasanii katika kuwania hizo Tuzo.
Na huu ni mwanzo tu, makubwa yanakuja zaidi. Kama wanabisha wamuulize yuko wapi Nakaaya na Maro. Mpaka leo wanajuta kuipigia kampeni CCM 2010, maana tuliwazika rasmi.
umeua kabisaa mkuu tatzo ccm
 
Wakuu habari nimekuwa naangalia tuzo za Mama Mtv leo. Tanzania ni nchi pekee iliyokuwa na wasanii6 kwenye hizo tuzo lakini cha ajabu tumekosa zotee! Nilicho jifunza mambo ya Team na u team fula mara team fulani yanagawa Kura kwa wasanii wetu! Mwishowe hatufanyinvizuri kwamfano kama Alikiba angehamasisha Watu wake wapige kura kwenye Category za Diamond ambazo yeye hashiriki na Diamond th same ange fanya hivyo tungeshinda! Nadhani sasa ni wakati wa vyombo vya habari nawatu wenye ushawishi mkubwa kumaliza hizi bifu za kijinga zinazo tushusha! Naomba kuwakilisha
Mi naona wasanii wazidi kutoa nyimbo nzuri zinazokubalika Afrika na ughaibuni....hiyo ndo njia pekee ya kutupeleka tuzo za GRAMY...
Teams zina madhara kwenye tuzo za KILI tu...
Na huwezi jua kama kura pekee ndo zimetuangusha...labda ulete ushahidi
 
Kovu la uchaguzi litazidi kuwaumiza Wasanii Team CCM Hatimiliki ya Albam mpaka Leo kwako ni ndoto harafu unataka ujilinganishe na WIZ KID wajiulize mbona miaka iliyopita DiAMOND alipata tuzo japo kulikuwepo na hizo team ni naungana na Zanzibar ASP
 
Tanzania sasa hivi hatuna muziki wetu, yote inayoimbwa sasa hivi kv bongo flavor, R&B, yote hiyo ni miziki ya nje. Muziki wetu ulikuwa enzi zile bendi zetu zinavuma kv Vijana jazz, Marquis orijinal, Msondo, DDC, Dar international, na nyinginezo.
 
Kwani Ali na Diamond ni akina mama mbona wanataka hizo tuzo za Mama?

Mimi mgeni nauliza tu
 
Tabu wasio na kazi wala fikra ndio wanakuza, pia Kiba aache kumtaja Diamond. Yaani wawe kama Nigerians wengi wao wote wanavuta pesa na wanaishi na kufanya kazi kivyao.

Timu zipo hata kwa big stars duniani kuendeleza wanaomshabikia na wengine wawapendao.

Tabu ya nchini kubwa ni watu kuonea wengine wanaojiendeleza WIVU.

Hata hasiye kwenye muziki wanajaa WIVU

Hata uishi maisha sio star nchini WIVU unaingia wengi waone umeshuka, badala ya kutaka kujua umefikaje ulipo nao wafike au wakupite.
Kwq nchi nyingine team zipo sanaa tu ila linapokuja swala la msanii mmoja kuwakilisha nchi huweka uteam pembeni, kitu ambacho watanzania tumeshindwa.
 
Msije mkasingizia timu, lugha, ......
Tatizo ni moja: Hakuna ubunifu zaidi ya makelele za video.
Huyo Diamond myamsififia kwa sasa mziki anaoufanya ni kunakili nyimbo za wasanii waliovuma zamani, kunakili video za wasanii wakubwa wa nje.
Je unadhani nitashawishika hata sekunde moja kusikiliza wimbo wa Saida Karoli uliorudiwa na Diamond???
Wamefanikiwa wakaamua kuwekeza kwenye ngono, kupiga mipicha, na kujisifia walivyo matawi.
Mbaya zaidi hata Clouds, EATV, .....hazina mvuto kwa wadau wa mziki waliona uelewa, je unadhani watapata wapi kura??
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom