Mziki wetu (Bongo Fleva) ni wakala mzuri wa Utawala, "Wanaufurahia"

Kakumamoto

JF-Expert Member
May 6, 2015
1,214
1,675
Habari wanajamvi, ukisikiliza redio zetu na ukiangalia luninga zetu, mziki unaochezwa na ambao ni kivutio kikubwa kwa rika zote japo sio kwa asilimia mia, hauna chembe ya juhudi ya kututoa tulipo kijamii na kiuchumi pia. Zaidi unatupumbaza, watoto, vijana na baadhi ya wazee wanapumbazwa kwa namna moja au nyingine.

Sikiliza bongo fleva yetu yenye vionjo vya Zouk au Pop wenyewe wanaita Afropop, unaburidisha ila unatukumbusha nini? tunapata kipi cha ziada zaidi ya burudani tele? Mafanikio yao machache yanatupumbaza jamii nzima na rundo la watoto na vijana wanawaza muziki huu! Angali BSS utajua ninichomaanisha. Na kwakuwapitia Wabongo Fleva, Wanasiasa na Watawala kiujumla wanawatumia vilivyo kutupumbaza.

Wajanja wa Mjini kulijua hili wakatumia technolojia wametulazimisha kizazi hiki kwamba muziki ni Bongo fleva pekee! hakuna kingine, Hip Hop hailipi na Reggae ni bangi tu! huiburudishi miziki hii! Sikiliza mapenzi mwanzo mwisho akili yako ibaki hapo hapo, plus WACK MCs.

Bongo fleva inajenga jamii nyingine kabisa inayowafanya wanasiasa na watawala wasipate shida kabisa, wafanye watakavyo.
 
Nape amewatumia sana kwenye kampeni za ccm .
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom