Mzigo wa Rwanda waongezeka bandarini

Mzigo wa Rwanda waongezeka bandarini

TPA

Member
Joined
Sep 28, 2016
Posts
49
Reaction score
71
Shehena ya Rwanda kupitia bandari ya Dar es Salaam katika kipindi cha miaka mitano imekuwa ikiongezeka kwa wastani wa asilimia 9.9 kwa mwaka kutoka tani 630,000 mwaka 2012/2013 mpaka tani 950,000 mwaka 2016/2017.

Haya yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi Deusdedit Kakoko alipokutana na balozi wa Rwanda nchini Tanzania Mhe. Eugene Kayihura aliyetembelea TPA leo.

Kakoko amesema kwamba kwa sasa shehena yote ya mizigo inayokwenda na kutoka Rwanda na nchi zingine za jirani inahudumiwa ndani ya bandari ili kurahisisha uondoshaji na usalama wa mizigo hiyo.

Mkurugenzi Mkuu amesema katika mkakati wake wa kuimarisha uhusiano zaidi na wateja, Serikali kupitia TPA imetenga eneo kwa ajili ya kuhifadhia mzigo wa Rwanda katika bandari Kavu ya Kwala, Ruvu na kuwataka wafanyabiashara wa nchini Rwanda kuitumia bandari Kavu ya Isaka kwa ajili ya mizigo yao ili kuwapunguzia safari ya kusafiri hadi Dar es Salaam.

TPA tayari imeshakamilisha ujenzi wa ofisi yake nchini Rwanda kwa ajili ya kuhudumia wateja wake toka nchini humo. Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu, ofisi hiyo ya TPA nchini Rwanda imekamilika na kinachosubiriwa ni ufunguzi baada ya kukamilisha taratibu zote ili ianze kazi rasmi.

“Ufunguzi wa ofisi hiyo utasaidia sana kuimarisha huduma kwa wateja wetu wa Rwanda ambao wanatumia Bandari ya Dar es Salaam,” amesema Kakoko.

Naye Balozi wa Rwanda nchini, Mhe. Eugene Kayihura ameishukuru TPA na Serikali ya Tanzania kwa kuwapatia eneo la kuhifadhia mizigo iendayo Rwanda.

Balozi Kayihura amesema kwamba biashara kati ya Tanzania na Rwanda imekuwa ikiongezeka kwa kasi katika siku za hivi karibuni mara baada ya TPA kuimarisha huduma zake.

“Kwa sasa Bandari ya Dar es Salaam imekuwa ikihudumia asimilia 90 ya mizigo yote inayoingia na kutoka Rwanda hivyo kuweka rekodi ya ukuaji wa haraka sana wa mizigo ya Rwanda inayohudumiwa nchini,” amesema Mhe. Balozi Kayihura.

Amesema kwamba ziara yake aliyoifanya bandarini ni sehemu ya juhudi za Rwanda kuimarisha uhusiano wa kibiashara na Tanzania haswa kwa kupitia huduma bora zitolewazo na Bandari ya Dar es Salaam kwa sasa.

Katika mkakati wake wa kuhakikisha inakuwa karibu na wateja wake, TPA hivi karibuni ilishiriki katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa nchini Rwanda ambapo pamoja na mambo mengine ilikutana na wafanyabiashara wa nchi hiyo ambao walionesha kuridhishwa na huduma za bandari ya Dar es Salaam.

upload_2017-9-21_15-20-13.jpeg

BALOZI WA RWANDA NCHINI, MHE. EUGENE KAYIHURA NA MKURUGENZI WA TPA, MHANDISI DEUSDEDIT KAKOKO HIVI KARIBUNI MAKAO MAKUU YA TPA KURASINI JIJINI DAR ES SALAAM.

Imetolewa na Ofisi ya Mawasiliano

Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)

S.L.P. 9184

DAR ES SALAAM

SIMU: (022) 2117816
 
Vizuri, muwe mnatoa taarifa kila mara na mjibu maswali
 
Kumbe wenzetu mizigo inaongezeka! Yetu inapungua sijui kwa nini.
 
Hivi kweli Tanzania tunajipima ufanisi wa Bandari kwa Mizigo ya Rwanda? Kanchi kadogo kabisa kana size ya Dar es Salaam! Hivi kweli tunashindwa kupigana kiume kuzitawala nchi kama DRC na Zambia zenye mizigo mikubwa na ya maana?

Kwa sasa kila siku ni Rwanda rwanda, hivi kuna nini cha zaidi huko?
 
ili nchi yeyote duniani iendelee lazima kutegemeana kwa wale waliosoma development study watakuwa wanaielewa hii
 
ushahidi wa kuongezeka ufanisi katika bandari yetu.
Local imports ndio zinazoweza kuifaidisha nchi kimapato/kiuchumi na sio Transit Cargo ambazo zinapita tu..
What's obtained from Transit Cargo is only Port Charges ambazo wala sio kubwa.. (na za Rwanda zimepunguzwa baada ya PK kumeet na JPM mara kadhaa)
Local consignments ndio mpango mzima kwa sababu Duty plus port charges na other local charges ndio zinakuwa collected..
Sasa ufanisi na mapato kiduchu wapi na wapi bwana..!??
Ndio sawa na kuwa na cheo kikubwa lakini mshahara wa karani.
 
na mizigo itaongezeka zaidi hadi kufikia 100% na kodi wamepunguziwa sana kama sio kuondolewa kabisa
 
Hivi kweli Tanzania tunajipima ufanisi wa Bandari kwa Mizigo ya Rwanda? Kanchi kadogo kabisa kana size ya Dar es Salaam! Hivi kweli tunashindwa kupigana kiume kuzitawala nchi kama DRC na Zambia zenye mizigo mikubwa na ya maana?

Kwa sasa kila siku ni Rwanda rwanda, hivi kuna nini cha zaidi huko?
Ila kama ingeshuka kutoka laki 9 mpaka laki 6 ungesema?
 
Hivi kweli Tanzania tunajipima ufanisi wa Bandari kwa Mizigo ya Rwanda? Kanchi kadogo kabisa kana size ya Dar es Salaam! Hivi kweli tunashindwa kupigana kiume kuzitawala nchi kama DRC na Zambia zenye mizigo mikubwa na ya maana?

Kwa sasa kila siku ni Rwanda rwanda, hivi kuna nini cha zaidi huko?
Hufahamu lolote ktk nyanja hii,kaa kimya!
 
Kuna taarifa kwamba wamesamehewa kodi nyingi mno,labda hiyo imechangia,hata kama ningekuwa Mimi,ninalipa kodi pungufu ya wenzangu,lazima nipitishe mzigo mwingi,
 
Huyu jamaa anatumia opportunity vizuri kweli.
Its either of the following though, Sizonje akawa ASSET wa PANA
Au in return kuna kitu kikubwa sana anapokea,
coz clearing ya mizigo ya rwanda mpaka sasa ni sawa na bure
na hakiwezi kuwa kingine
ila ni maujanja ya kusupress upinzani na mikakati ya kuminya uhuru wa
vyombo vya habari pamoja na media manipulation na propaganda​
 
Back
Top Bottom