Mzigo wa Rwanda waongezeka bandarini

Mzigo wa Rwanda waongezeka bandarini

Local imports ndio zinazoweza kuifaidisha nchi kimapato/kiuchumi na sio Transit Cargo ambazo zinapita tu..
What's obtained from Transit Cargo is only Port Charges ambazo wala sio kubwa.. (na za Rwanda zimepunguzwa baada ya PK kumeet na JPM mara kadhaa)
Local consignments ndio mpango mzima kwa sababu Duty plus port charges na other local charges ndio zinakuwa collected..
Sasa ufanisi na mapato kiduchu wapi na wapi bwana..!??
Ndio sawa na kuwa na cheo kikubwa lakini mshahara wa karani.
Mkuu sasa hivi mizigo ya transit wanalipa wharfage ambayo ni 0.25% ya CIF value so somehow kuna income inaongeza kwenye taifa tofauti na zamani.

Ila kwa urafiki walio nao hawa viongozi wetu tusitarajie mizigo ya Rwanda ikapungua ila kwa uadui alionao huyu mkuu wetu na wafanya biashara wa ndani tusitarajie local imports ikaongezeka.
 
Hivi kweli Tanzania tunajipima ufanisi wa Bandari kwa Mizigo ya Rwanda? Kanchi kadogo kabisa kana size ya Dar es Salaam! Hivi kweli tunashindwa kupigana kiume kuzitawala nchi kama DRC na Zambia zenye mizigo mikubwa na ya maana?

Kwa sasa kila siku ni Rwanda rwanda, hivi kuna nini cha zaidi huko?
Watanua magoli mna tabu sana
 
Hadi wametengewa bandari kavu, huenda wanapitishiwa mizigo kwa bei isiyo na maslahi kwa nchi. Kweli JK alikuwa mzalendo na hakucheza na biashara bandarini.
 
Tumeweka mazingira mazuri ya kuvutia soko na kufanya biashara katika hali ya ushindani hii ni pamoja na kuwa na ofisi nchini Rwanda.
Mazingira mazuri ya kuvutia soko ndio kupitisha mizigo kwa bei chee?
 
Local imports ndio zinazoweza kuifaidisha nchi kimapato/kiuchumi na sio Transit Cargo ambazo zinapita tu..
What's obtained from Transit Cargo is only Port Charges ambazo wala sio kubwa.. (na za Rwanda zimepunguzwa baada ya PK kumeet na JPM mara kadhaa)
Local consignments ndio mpango mzima kwa sababu Duty plus port charges na other local charges ndio zinakuwa collected..
Sasa ufanisi na mapato kiduchu wapi na wapi bwana..!??
Ndio sawa na kuwa na cheo kikubwa lakini mshahara wa karani.
Weww binafsi umeshaimport nini?
 
Shehena ya Rwanda kupitia bandari ya Dar es Salaam katika kipindi cha miaka mitano imekuwa ikiongezeka kwa wastani wa asilimia 9.9 kwa mwaka kutoka tani 630,000 mwaka 2012/2013 mpaka tani 950,000 mwaka 2016/2017.

Haya yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi Deusdedit Kakoko alipokutana na balozi wa Rwanda nchini Tanzania Mhe. Eugene Kayihura aliyetembelea TPA leo.

Kakoko amesema kwamba kwa sasa shehena yote ya mizigo inayokwenda na kutoka Rwanda na nchi zingine za jirani inahudumiwa ndani ya bandari ili kurahisisha uondoshaji na usalama wa mizigo hiyo.

Mkurugenzi Mkuu amesema katika mkakati wake wa kuimarisha uhusiano zaidi na wateja, Serikali kupitia TPA imetenga eneo kwa ajili ya kuhifadhia mzigo wa Rwanda katika bandari Kavu ya Kwala, Ruvu na kuwataka wafanyabiashara wa nchini Rwanda kuitumia bandari Kavu ya Isaka kwa ajili ya mizigo yao ili kuwapunguzia safari ya kusafiri hadi Dar es Salaam.

TPA tayari imeshakamilisha ujenzi wa ofisi yake nchini Rwanda kwa ajili ya kuhudumia wateja wake toka nchini humo. Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu, ofisi hiyo ya TPA nchini Rwanda imekamilika na kinachosubiriwa ni ufunguzi baada ya kukamilisha taratibu zote ili ianze kazi rasmi.

“Ufunguzi wa ofisi hiyo utasaidia sana kuimarisha huduma kwa wateja wetu wa Rwanda ambao wanatumia Bandari ya Dar es Salaam,” amesema Kakoko.

Naye Balozi wa Rwanda nchini, Mhe. Eugene Kayihura ameishukuru TPA na Serikali ya Tanzania kwa kuwapatia eneo la kuhifadhia mizigo iendayo Rwanda.

Balozi Kayihura amesema kwamba biashara kati ya Tanzania na Rwanda imekuwa ikiongezeka kwa kasi katika siku za hivi karibuni mara baada ya TPA kuimarisha huduma zake.

“Kwa sasa Bandari ya Dar es Salaam imekuwa ikihudumia asimilia 90 ya mizigo yote inayoingia na kutoka Rwanda hivyo kuweka rekodi ya ukuaji wa haraka sana wa mizigo ya Rwanda inayohudumiwa nchini,” amesema Mhe. Balozi Kayihura.

Amesema kwamba ziara yake aliyoifanya bandarini ni sehemu ya juhudi za Rwanda kuimarisha uhusiano wa kibiashara na Tanzania haswa kwa kupitia huduma bora zitolewazo na Bandari ya Dar es Salaam kwa sasa.

Katika mkakati wake wa kuhakikisha inakuwa karibu na wateja wake, TPA hivi karibuni ilishiriki katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa nchini Rwanda ambapo pamoja na mambo mengine ilikutana na wafanyabiashara wa nchi hiyo ambao walionesha kuridhishwa na huduma za bandari ya Dar es Salaam.

View attachment 592913
BALOZI WA RWANDA NCHINI, MHE. EUGENE KAYIHURA NA MKURUGENZI WA TPA, MHANDISI DEUSDEDIT KAKOKO HIVI KARIBUNI MAKAO MAKUU YA TPA KURASINI JIJINI DAR ES SALAAM.

Imetolewa na Ofisi ya Mawasiliano

Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)

S.L.P. 9184

DAR ES SALAAM

SIMU: (022) 2117816
Swali je, wanalipia maana kuna tetesi kuwa ni vunja bei kwa Rwandaise..!???
 
Mi nadhani hatujatumia vyema akili zetu hapa, mtoa mada hakumaanisha kwamba TPA inalipuuza soko la DRC au zambia, bali la Rwanda lilikuwa linatutoka kuelekea Kenya, limerejeshwa. Kuhusu kodi na mapato, unadhani kipi kingefanyika kulitoa Kenya? Wakati mwingine tuwe tunawaamini wataalamu wetu, ndio usomi huo.
 
Je ukichukua hilo ongezeko tajwa, ni asilimia ngapi ya mizigo yote iliyopita hapo bandarini kwa miaka husika?

Tunatumia kipimo gani kupima ukuaji au la (annual port's performance)? Wangetupa takwimu kamili ili tuone shehena ya Rwanda ni % ngapi, DRC ni %? Zambia, Malawi nk nk
 
Hakuna unachoelewa zaidi ya Siasa za kijinga kwenye vitu vya maana
Hilo natumai limekuingia, uwe unatoka Uganda, Burundi, Malawi, Congo, Zimbabwe, Rwanda, Kenya popote pale bandari itakutazama kama mteja mpendwa cha msingi ni kulipa bills zote za bandarini ipasavyo.

Hilo la huyu anatoka kwenye eneo la mraba likubwa kuliko fulani akili yako pekee ndio inaweza kulichakata ila kwangu it's bloody rubbish.
 
Mkuu ungetuambia mapato yameongezeka kiasi gani ingekuwa vizuri zaidi, badala ya asilimia peke yake ungeweka vyote kwa kila mteja na kwa jumla. Kutupa asilimia bila kutuambia kiasi halisi inakuwa bado kidogo kueleweka.

Pia tungepata na data za mizigo ya nchi/wateja wingine zinazotumia bandari yetu.

Umesema mnajithaidi kuvutia wateja kutumia bandari yetu, ni vizuri pia ungeeleza mnafanya yapi katika kuvutia huko? Je ni wateja wote au baadhi tu? Mmejiewekea mipango au mpaka mpate maelekezo?

TPA
 
Hilo natumai limekuingia, uwe unatoka Uganda, Burundi, Malawi, Congo, Zimbabwe, Rwanda, Kenya popote pale bandari itakutazama kama mteja mpendwa cha msingi ni kulipa bills zote za bandarini ipasavyo.

Hilo la huyu anatoka kwenye eneo la mraba likubwa kuliko fulani akili yako pekee ndio inaweza kulichakata ila kwangu it's bloody rubbish.
Na wewe ndio miongoni mwa Washauri wakuu wa Serikali, unaowashauri wajenge Rail ya gharama kubwa kwenda maeneo yasiyo na mizigo na kushindwa kufikiria ujenzimwa Rail sehemu itakayoingiza pesa
 
Hivi kweli Tanzania tunajipima ufanisi wa Bandari kwa Mizigo ya Rwanda? Kanchi kadogo kabisa kana size ya Dar es Salaam! Hivi kweli tunashindwa kupigana kiume kuzitawala nchi kama DRC na Zambia zenye mizigo mikubwa na ya maana?

Kwa sasa kila siku ni Rwanda rwanda, hivi kuna nini cha zaidi huko?
Hata mimi nilitaka kusema hivyo,ka nchi kama wilaya moja! Kweli wametutawala akili.[emoji35] [emoji35]
 
Back
Top Bottom