Mzigo wa Rwanda waongezeka bandarini

Mzigo wa Rwanda waongezeka bandarini

Hivi kweli Tanzania tunajipima ufanisi wa Bandari kwa Mizigo ya Rwanda? Kanchi kadogo kabisa kana size ya Dar es Salaam! Hivi kweli tunashindwa kupigana kiume kuzitawala nchi kama DRC na Zambia zenye mizigo mikubwa na ya maana?

Kwa sasa kila siku ni Rwanda rwanda, hivi kuna nini cha zaidi huko?

Mikakati ya kuongeza shehena katika nchi za DRC, Uganda na Zambia na nyinginezo ipo na tunaendelea nayo kupitia Idara ya Masoko. TPA inatambua umuhimu na mchango wa kila soko katika kuongeza pato la nchi.
 
Local imports ndio zinazoweza kuifaidisha nchi kimapato/kiuchumi na sio Transit Cargo ambazo zinapita tu..
What's obtained from Transit Cargo is only Port Charges ambazo wala sio kubwa.. (na za Rwanda zimepunguzwa baada ya PK kumeet na JPM mara kadhaa)
Local consignments ndio mpango mzima kwa sababu Duty plus port charges na other local charges ndio zinakuwa collected..
Sasa ufanisi na mapato kiduchu wapi na wapi bwana..!??
Ndio sawa na kuwa na cheo kikubwa lakini mshahara wa karani.

Asante kwa maoni yako, kila biashara tunayoitekeleza ni muhimu na tunaipa kipaumbele.
 
Si nilisikia hiyo mizigo yao inapita bei chee hata kuliko yetu sisi hapa na nchi nyingine?

Tumeweka mazingira mazuri ya kuvutia soko na kufanya biashara katika hali ya ushindani hii ni pamoja na kuwa na ofisi nchini Rwanda.
 
Local imports ndio zinazoweza kuifaidisha nchi kimapato/kiuchumi na sio Transit Cargo ambazo zinapita tu..
What's obtained from Transit Cargo is only Port Charges ambazo wala sio kubwa.. (na za Rwanda zimepunguzwa baada ya PK kumeet na JPM mara kadhaa)
Local consignments ndio mpango mzima kwa sababu Duty plus port charges na other local charges ndio zinakuwa collected..
Sasa ufanisi na mapato kiduchu wapi na wapi bwana..!??
Ndio sawa na kuwa na cheo kikubwa lakini mshahara wa karani.
watanzania mna tabu sana, mwaka wa 2016/2017 serikali iliongezea VAT kwenye hii mizigo ya transit mkalalamika sana kwamba bandari yetu inakufa, kwamba sera zetu zimewakimbiza wateja wote wa nje na hivo kupunguza ajira hasa za madereva wa magari makubwa! leo hii zimeanza kuongezeka mnasema tena kwamba hazina maana! Nani katuroga aisee????????
 
Ile pekee kuifananisha Rwanda kijiografia na Dar es salaam,ni kielelezo tosha kwamba huyo jamaa ni mweupe!
Mkuu ungetufahamisha tusiojua basi... alipaswa atuambieje ili nasi tuelimike?
 
Haya bwana TPA ila nadhani unajua kwanini, mi na wewe hatujui raia namba moja alikubaliana vitu gani na mtusi Kagame
 
Mikakati ya kuongeza shehena katika nchi za DRC, Uganda na Zambia na nyinginezo ipo na tunaendelea nayo kupitia Idara ya Masoko. TPA inatambua umuhimu na mchango wa kila soko katika kuongeza pato la nchi.

Kuna sehemu mnakosea sana, Rwanda wana mizigo ya kuingia tu na wanatoa almost nothing, so sio nchi ya kufocus sana na kuwapa privileges nyingi pamoja examptions ili kuwavutia watumie Bandari yetu,

DRC na Zambia wana Advantage kubwa sana, kwani Wao wanaingiza mizigo mingi (kutokana na size ya nchi yao na idadi ya watu inayofanya demand ya mizigo kutoka nje iwe kubwa, na pia wao wanatoa mizigo mingi na mizito (Copper, Cobalt, Manganese, Coltan, ect) kwenda nje, so Truck linalopeleka Contena DRC na Zambia linaweza kurudi na Mzigo huo wa Base Metal, shida nyie TPA mnangangania Rwanda bila kuweka mikakati dhabiti ya kumonopoly Soko la DRC na Zambia

Kijiografia ya East na Central Africa Tanzania ndio kitovu au tuseme ndio gateway ya kwenda Asia pamoja na East Europa, kwa sasa Masoko ya Copper, Cobalt, Coltan na Manganese ni kubwa kwenye nchi za Asia namaanisha China, India, Japan, Korea na hata east Europa, Na Supplier mkubwa wa hizo product ni DRC na Zambia, na kama nilivyosema hapo awali Tanzania ndio geographically gateway

Tabu sijui hamna exposure au nini, badala ya kuangaika na huku kwenye Profit tuko bize na Rwanda, ukiangalia Mizigo mingi ya Zambia na DRC sasa inapitia Durban-RSA, ni long distance lakini ni bora kuliko urasimu wenu na old fashion ya utendaji wenu, pia mnatakiwa kujua kuwa Angola wako bize kuiupgrade Bandari yao ili waichukue mizigo hiyo ya Zambia na DRC

Nyie kama watu wa TPA, mngeangaika na kupigania sana hiyo Standard Gauge ijengwe kwenda Kigoma kwanza na sio Rwanda au Burundi, hiyo Rail ingefika Kigoma, kungekuwa na link ya kwenda Katanga kwenye hayo mabase Metal, maana kuna Rail inayotoka Kalemie mpaka Lubumbashi ambapo inalink na migodi ya Kolwezi, Likasi na Lubumbashi Copper belt, na pia inauwezo wa kulink pia na Kisenge kwenye Manganese

Pia kwa upande wa Zambia, kuna Bandari ya Mpulungu (Lake Tanganyika) ambayo wao Zambia wangeweza kusafirisha mizigo yao kwenye maji mpaka Kigoma kisha ingeingia kwenye SG,

alexelias
 
Ile pekee kuifananisha Rwanda kijiografia na Dar es salaam,ni kielelezo tosha kwamba huyo jamaa ni mweupe!

We mjuaji kuna mtu kaifananisha Rwanda na Dar es Salaam Kijiografia humu?
 
Shehena ya Rwanda kupitia bandari ya Dar es Salaam katika kipindi cha miaka mitano imekuwa ikiongezeka kwa wastani wa asilimia 9.9 kwa mwaka kutoka tani 630,000 mwaka 2012/2013 mpaka tani 950,000 mwaka 2016/2017.

Haya yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi Deusdedit Kakoko alipokutana na balozi wa Rwanda nchini Tanzania Mhe. Eugene Kayihura aliyetembelea TPA leo.

Kakoko amesema kwamba kwa sasa shehena yote ya mizigo inayokwenda na kutoka Rwanda na nchi zingine za jirani inahudumiwa ndani ya bandari ili kurahisisha uondoshaji na usalama wa mizigo hiyo.

Mkurugenzi Mkuu amesema katika mkakati wake wa kuimarisha uhusiano zaidi na wateja, Serikali kupitia TPA imetenga eneo kwa ajili ya kuhifadhia mzigo wa Rwanda katika bandari Kavu ya Kwala, Ruvu na kuwataka wafanyabiashara wa nchini Rwanda kuitumia bandari Kavu ya Isaka kwa ajili ya mizigo yao ili kuwapunguzia safari ya kusafiri hadi Dar es Salaam.

TPA tayari imeshakamilisha ujenzi wa ofisi yake nchini Rwanda kwa ajili ya kuhudumia wateja wake toka nchini humo. Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu, ofisi hiyo ya TPA nchini Rwanda imekamilika na kinachosubiriwa ni ufunguzi baada ya kukamilisha taratibu zote ili ianze kazi rasmi.

“Ufunguzi wa ofisi hiyo utasaidia sana kuimarisha huduma kwa wateja wetu wa Rwanda ambao wanatumia Bandari ya Dar es Salaam,” amesema Kakoko.

Naye Balozi wa Rwanda nchini, Mhe. Eugene Kayihura ameishukuru TPA na Serikali ya Tanzania kwa kuwapatia eneo la kuhifadhia mizigo iendayo Rwanda.

Balozi Kayihura amesema kwamba biashara kati ya Tanzania na Rwanda imekuwa ikiongezeka kwa kasi katika siku za hivi karibuni mara baada ya TPA kuimarisha huduma zake.

“Kwa sasa Bandari ya Dar es Salaam imekuwa ikihudumia asimilia 90 ya mizigo yote inayoingia na kutoka Rwanda hivyo kuweka rekodi ya ukuaji wa haraka sana wa mizigo ya Rwanda inayohudumiwa nchini,” amesema Mhe. Balozi Kayihura.

Amesema kwamba ziara yake aliyoifanya bandarini ni sehemu ya juhudi za Rwanda kuimarisha uhusiano wa kibiashara na Tanzania haswa kwa kupitia huduma bora zitolewazo na Bandari ya Dar es Salaam kwa sasa.

Katika mkakati wake wa kuhakikisha inakuwa karibu na wateja wake, TPA hivi karibuni ilishiriki katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa nchini Rwanda ambapo pamoja na mambo mengine ilikutana na wafanyabiashara wa nchi hiyo ambao walionesha kuridhishwa na huduma za bandari ya Dar es Salaam.

View attachment 592913
BALOZI WA RWANDA NCHINI, MHE. EUGENE KAYIHURA NA MKURUGENZI WA TPA, MHANDISI DEUSDEDIT KAKOKO HIVI KARIBUNI MAKAO MAKUU YA TPA KURASINI JIJINI DAR ES SALAAM.

Imetolewa na Ofisi ya Mawasiliano

Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)

S.L.P. 9184

DAR ES SALAAM

SIMU: (022) 2117816
Kiongozi wao ndio anatoa ushauri wa kuua wapinzani kama anavyofanya kule kwake!!?
 
Kama unampunguzia kodi zoote analipa kidogo wakati kwa uhalisia transit hazina deal sana linganisha na local imports hak hak kushangilia hapo!! Ni ujinga tu wa kuwafukuza kwanza na kuwarudisha kwa kodi zaidi 55% pungufu!! Uhayawaniiii uzwzwa huuu
 
Niseme nini sasa? Rwanda ni nchi ndogo sana kuizungumzia kwenye issue ya Bandari
Watanzania aisee ni shida, hivi bandari inahudumia nchi au inahudumia mteja? Ni sawa na kusema sina haja kupokea pesa ya mtu mwembamba, nitajikita kuhakikisha bidhaa zangu nawauzia watu wanene tu seriously?

Ndio akili zetu Watanzania zimefikia hapa? The wishes of any business is to make sure profits margins and productivity range zinapanda in any means no matter who's the customer, what we need is money only.

Bandarini pale inafanywa biashara kama zilivyo biashara nyingine zozote na anayeangaliwa ni mteja na kama alivyo mfanyabiashara yeyote anahitaji wateja wengi wapate Huduma zake hata maadui zake wakija atawatreat as if ni malaika hiyo ndio kanuni za biashara, sasa hii biashara ya chadema inayosisitiza kufanya biashara na watu wanaotoka kwenye ardhi kubwa tu ni ya wapi jamani?

Nyie akili zenu zina walakini naona Mungu anawaadhibu kwa style mbalimbali huku kupinga pinga kila kitu mwishowe mnaenda kuokota makopo.
 
Hakuna unachoelewa zaidi ya Siasa za kijinga kwenye vitu vya maana
 
Back
Top Bottom