Mzee Yussuf wa Jahazi Mahututi Muhimbili?

Junius

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
3,181
139
Muimba taarabu mashuhuri nchini Tanzania na Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Jahazi Modern Taarab, Mzee Yusuph Mwinyi maarufu kama ‘Mzee Yusuph’, leo majira ya saa sita mchana amedondoka ghafla na kupoteza fahamu kisha kukimbizwa katika Hospitali kuu ya Taifa ya Muhimbili.

Tukio hilo la kushtukiza limetokea wakati Mzee Yusuph akiwa katika ofisi za Radio Clouds FM, jijini Dar es Salaam alikokuwa amekwenda kwa shughuli zake za kikazi. Akiwa mapokezi(Reception), ghafla hali yake ilianza kubadilika na akaanza kulalamika kuwa anasikia kizunguzungu kabla ya kudondoka chini na kupoteza fahamu.

Kwa sasa yuko Hospitalini Muhimbili na madaktari wanahangaika kuyanusuru maisha yake.


source:Global Publishers Ltd
 
Tunajaribu kuwasiliana na ndugu wa karibu kujua kinachoendelea...wadau tusaidiane mlioko karibu uko.
 
Muimba taarabu mashuhuri nchini Tanzania na Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Jahazi Modern Taarab, Mzee Yusuph Mwinyi maarufu kama ‘Mzee Yusuph’, leo majira ya saa sita mchana amedondoka ghafla na kupoteza fahamu kisha kukimbizwa katika Hospitali kuu ya Taifa ya Muhimbili.



Du , Mkuu ulivyoripoti imenitisha sana mimi...Kwamba yu mahututi si jambo la mchezo mkuu!...
Mungu mwenyezi amrudishie afya yake kiumbe huyu, na aendelee na shughuli zake!
 
Mbona taarifa nilizozipata anadaiwa yupo TMJ na amerejewa na fahamu na kaanza kuzungumza ?
 
JAMANI............y.....kwa nini?mola amjaalie jamani MFALME MBONA KULALAA....aaa sijalalaa nautia kasiiiii
 
Mfalme ameruhusiwa aliwekwa mapumzikoni TMJ na sio Muhimbili tumeongea nae sasa hivi mashabike wake msitie hofu.
 
Mungu amponye haraka maana nasikia kifupi ndugu wameshaana kungangania funguo za gari lilipo hapo nje hospt
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom