Mzee Warioba apewe ulinzi zaidi

Mzee Warioba apewe ulinzi zaidi

Ndinani

Platinum Member
Joined
Aug 29, 2010
Posts
7,812
Reaction score
4,817
Kufuatana na hali ya kiu salama ilivyo tete hivi sasa nchini kuna kila sababu ya kuimalisha ulinzi wa watu muhimu kwa Taifa letu hasa hasa mzee Warioba.
Nasema hivi kuwa hali ya kiusalama kuwa tete kutokana na vitendo vya kihalifu vilivyowapata watu wengi hivi karibuni akiwemo father Kitima! Cha kushangaza katika matukio yote haya polisi wanajifanya hawana habari ingawa ushahidi wa kimazingira unaonesha kuhusika kwao! Mfano ni taarifa ya kutekwa kwa Mdude Nyagali Kule Mbeya na kumuumiza vibaya na polisi wakisema hawahusiki ili hali kuna ushahidi kuwa wao walihusika! Taarifa ya polisi juu Mazingira ya kushambuliwa kwa Rev. Kitima jinsi ilivyopotoshwa inaonesha wazi kuwa polisi wanaficha ukweli wa tukio hilo.
Kufuatana na mwenendo wa serikali na vyombo vya dola hasa polisi ni wazi kwamba wananchi hawatapata haki nchini mwao hivyo ni wajibu wao kujilinda ili kupata haki yao!
Mzee Warioba anastahili ulinzi zaidi kwani ccm na serikali yake Sidhani kama watatimiza jukumu hilo kwani hata huko nyuma kwa msimamo wake wa haki walimtumia Makonda kumshambulia alipokuwa anatoa mhadhara kuhusu katiba mpya. Kwa mukutadha huo huo ningemuomba Mzee Warioba azatiti ulinzi wake na asitehemee serikali ya Samia hawaaminiki wamekuwa majambazi!
 
Katiba ya warioba ni nzuri mno sema wana siasa wa huu Ukanda wetu wao wakioga wewe uwe unachamba na kuvaa Kabisa mamaee
 
Rwanda, kagame alimfunga mpinzani wake na kuua wengine wee engine.
Uganda, bisigye anasta ndani kwa makosa ya kijinga kabisa.
Tanzania, lisu yu ndani kwa makosa ya kijinga kabisa.
Hawa maraisi huwa wakikutana kwenye zile summities zao wanaongeaga nini haswa?
 
Back
Top Bottom