Mzee wa Upako: Lowassa hawezi kuwa Rais 2020, CHADEMA wanahusika kunichafua

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,866
LOWASSA HAWEZI KUWA RAIS 2020 – Mzee wa Upako Anthony Lusekelo

Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ ametumia ibada aliyofanya kanisani kwake, Ubungo-Kibangu jijini Dar jana, kumvaa aliyekuwa Waziri Mkuu na Mgombea Urais Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa kuwa hawezi kuwa rais mwaka 2020.

Mzee wa Upako alisema kuwa, anajua anashambuliwa na baadhi ya wachungaji na watu wengine wakiwemo Chadema kwa sababu ya Rais John Pombe Magufuli kumjengea Barabara ya Kibangu jijini Dar hivyo kuona kama anakubalika kwa rais.

Mimi nashangaa chuki za nini au sababu ni Rais John Magufuli kuijenga Barabara ya Kibangu? Rais hakujenga barabara hii na kusema ni yangu bali amewajengea wakazi wa Kibangu, ingekuwa ni yangu, ningekuwa naweza kukatisha ushuru kwa wapita njia.

“Najua wanaonichafua, Chadema wanahusika kabisa kwenye hili, hivi unadhani Lowassa anaweza kuwa rais mwaka 2020 kwa akili yako? Kuwa na wabunge wengi bungeni wanaweza, lakini rais ni ndoto ya machana. Hata kama nitakuwa nimeaga dunia, Lowassa hawezi kuchukua nchi hii.

“Namshangaa sana Lowassa kutaka ving’ora, mbona alishapigiwa sana wakati akiwa waziri Mkuu, nakumbuka kuna siku nilikuwa eneo la Kamata (Dar), mara askari wa usalama barabarani akasimamisha magari likiwemo la kwangu, nikauliza kulikoni nikaambiwa Waziri Mkuu, Lowassa anapita. Sasa nini kingine anakitaka?

“Siku Lowassa akifariki dunia ni lazima atapigiwa mizinga kumi na nane kwa heshima kubwa aliyonayo katika nchi hii, sasa anataka heshima gani nyingine jamani?

“Mimi sikumtabiria Rais Magufuli, alitabiriwa na TB Joshua, sasa uhasama unatoka wapi jamani? Mimi sina kosa wananionea bure tu.

“Nampongeza sana Rais Magufuli, sina shaka na uongozi wake kabisa, kamatia hapohapo [akaanza kuimba wimbo wa Navy Kenzo wa Kamatia Chini] kamatia chini, kamatia chini…. . Si kweli kwamba Rais Magufuli ni mkali, hapana ni mtu mwema, mpole, mpenda amani na haki na anataka kila mwananchi awe na mafanikio kupitia nchi yake”.

[HASHTAG]#source[/HASHTAG] [HASHTAG]#magazetini[/HASHTAG] #
 
Mkuu utakufa wewe.
 
Sasa huyo Mzee wa Upako aka mzee wa Bapa, anadhani kwa kuwafagilia CCM ndiyo scandal yake ya kulewa chakari ndiyo itapoa?

Hata kama Mkuu wa nchi alifika pale kanisani kwake na kumfagilia na kumjengea barabara ya lami, lakini bado sisi wananchi tunamuona huyo 'mchunga kondoo' kuwa ni Chapombe tuu............
 
Back
Top Bottom