Mzee wa Upako adai yeye ndiye anazuia mvua Dar

mogulnoise

JF-Expert Member
Oct 28, 2014
2,434
5,537
Jana katika Ibada mchungaji Antoni Lusekelo aka mzee wa upako amedai kuwa mvua Dar haitanyesha hadi ujenzi wa barabara inayojengwa kuelekea kanisani kwake ikamilike

Aliongeza akitamba kwamba yeye ana Mungu japo watu wanamzushia maneno

Nashauri mamlaka ya hali ya hewa imtumie huyu jamaa labda atasaidia kuleta mvua sehemu kame

Kazi kweli kweli hawa wachangiaji wenye a. k. a nimewavulia kofia
 
Mmmmh kuna MUNGU na miungu sasa mm nahisi iliyozuia ni miungu maaana sidhani kama MUNGU anaeweza akaruhusu watu wanaotegemea maji ya mvua wapate maji ya kunywa wakose,waliopanda mashamba yao na kulima bustani ndogo wasipate mazao kwa sababu ya barabara ya kuelekea kanisa moja. Dwaaaah wachungaji wetu hawa !!!
 
Mungu anayemzungumzia huyo bwana SIO yule Muumba mbingu na ardhi.Mungu muumbaji mbingu na ardhi ni MUADILIFU sana;hawezi kuwa karibu na watu wa batili.
 
Nina uhakika kuna watu walipiga vigere gere na makofi.
Imani inafanya ndugu zetu wasijue kama wanafungwa kamba tusiwalaumu sana.
 
Daaaah mungu mkubwa anaweza mpa mtu kipawa cha namna hii hongera sana mzee wa upako hiyo barabara ikishakamilika tujulishe ili tuanze kupata mvua kwenye hili jiji letu la dsm
 
Jana katika Ibada mchungaji Antoni Lusekelo aka mzee wa upako amedai kuwa mvua Dar haitanyesha hadi ujenzi wa barabara inayojengwa kuelekea kanisani kwake ikamilike

Aliongeza akitamba kwamba yeye ana Mungu japo watu wanamzushia maneno

Nashauri mamlaka ya hali ya hewa imtumie huyu jamaa labda atasaidia kuleta mvua sehemu kame

Kazi kweli kweli hawa wachangiaji wenye a. k. a nimewavulia kofia
K on yagi za asubuhi mbaya sana
 
Back
Top Bottom