Mzee wa Upako ajitaja katika sakata la madawa ya kulevya

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
20,376
24,928
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) Ubungo-Kibangu jijini Dar, Lusekelo Anthony 'Mzee wa Upako' amejitaja kuwa ni mmoja kati ya watu mashuhuri ambao wamewahi kutuhumiwa kuhusika na biashara ya dawa za kulevya.


Amefunguka na kusema kuwa yeye ni mhanga wa suala hilo jambo ambalo lilimpa wakati mgumu sana katika maisha na kumfanya kunyanyapaliwa na jamii pamoja na watu wake wa karibu wakiwemo wachungaji wenzake.



Mchungaji Lusekelo amesema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachofanyika kupitia ukurasa wa facebook wa EATV kila Jumatano kuanzia saa nane mchana hadi saa kumi jioni.



Lusekelo anadai kuwa mwaka 1997 alituhumiwa kuuza dawa za kulevya lakini anakiri wazi kuwa polisi wa kipindi kile walikuwa ni wastaraabu kwani waliamuandikia samansi na kumuomba kufika kituo cha polisi kutoa maelezo, hivyo anasema alifika na kutoa maelezo yake lakini taarifa hiyo ilivuja mtaani jambolililopelekea watu kumtenga.


"Mimi ni mhanga wa dawa za kulevya mwaka 1997 nilituhumiwa kuwa nauza madawa, lakini wale askari walikuwa wastaarabu, waliniandikia samasi nikafika kutoa maelezo yangu, lakini baadaye niliwaambia kuwa wao ni polisi wafanye uchunguzi wao, walifanya uchunguzi na kugundua mimi sihusiki, watu walifuatilia na kugundua siyo kweli, na kila mtu akajitoa kwenye, ilionekana kuwa ni wivu tu, ila mbaya zaidi ile taarifa kuwa niliitwa polisi kwa madawa ya kulevya ilivuja, hadi wachungaji wenzangu walininyanyapaa, nikivaa suti au nikiendesha gari kila anajuani pesa za madawa" alisema Mzee wa Upako.



Paul Makonda - Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye kwa takriban wiki moja amekuwa akitaja watu mbalimbali wanaodaiwa kuhusika na dawa za kulevya ambapo katika majina 65 aliyotaja leo, limo jina la Mchungaji Josephat Gwajima, Mzee wa Upako ameshauri vita ya dawa zakulevya kwa watu wanaotuhumiwa ni bora viongozi wangetumia njia za kipolisi kuwataka kufika polisi kwani kutumia njia ya magazeti inaweza kushusha heshima ya baadhi ya watu ambayo wameijenga kwa miaka mingi.


"Mimi kutokana na tuhuma zangu kuvuja kuwa niliitwa polisi kwa madawa ya kulevya niliishi miaka saba watu wananinyayapaa, tena hiyo ni tuhuma tu. Imenichukua miaka saba kusafisha jina, nimekuja kuanza kusafisha jina mwaka 2005 hivi"

Amesema yeye binafsi anachukia sana dawa za kulevya kutokana na madhara yake kwa jamii, hivyo hawezi kuthubutu kujihusisha nazo wala hawezi kuunga mkono watu wanaofanya shughuli hizo kwa kuwa dawa za kulevya zinaua kizazi cha maendeleo na taifa kwa ujumla.



Baadhi ya watu katika kipindi hicho walitaka maoni yake kuhusu Mchungaji Josephat Gwajima kuhusishwa na dawa zakulevya ambapo Lusekelo alisema hawezi kulizungumzia suala hilo na kutaka watu wasubiri hadi mwisho wake ufike ndipo na yeye anaweza kusema lolote.Mchungaji Josephati GwajimaPia alishauri watu wanaowataja viongozi waliojijenga kwa muda mrefu kama Mchungaji gwajima wanapaswa kuwa na uhakika na ushahidi mkubwa usio na shaka, maana ikija kubainika kuwa siyo kweli, litakuwa ni kazi ngumu kwa viongozi hao kujisafisha kama ilivyomtokea yeye mwaka 1997.



"Kama kweli kuna wachungaji wanajihusisha au wanadhaniwa kuhusika kwenye madawa ya kulevya nashauri tungetumia njia ya wao kuitwa kwa samasi, tunapaswa kuwa makini katika hili kwani kujenga heshima ni kitu kikubwa, njia ya kuwaita watuhumiwa kwa njia ya magazeti si jambo nzuri kabisaa"


amesisitiza Mzee wa Upako Kwa wale waliotaka kujua jinsi anavyomuelewa Mchungaji Gwajima, Lusekelo amesema kuwa Gwajima ni rafiki yake, na wanaheshimiana sana.



20170208222613.jpeg
Chanzo : EATV
 
Ndo maana kikwete hakutaka kuweka majina hadharani. Mtikisiko MTANDAO wa madawa mtahangaika Sana kuteteana. Jiwe limetupwa penyewe
 
Ndo maana kikwete hakutaka kuweka majina hadharani. Mtikisiko MTANDAO wa madawa mtahangaika Sana kuteteana. Jiwe limetupwa penyewe
Kama hajaulizwa kuhusu kupiga bapa na kutukana jirani yake basi hicho kikaango kilikuwa feki
Mtu mwenye akili ndogo hawezagi kufikiri makubwa hata siku moja mzee wa upako kaongea vyema kabisa maana zipo taratibu zinazo fahamika ujinga hufanywa na wajinga pekee
 
Mtu mwenye akili ndogo hawezagi kufikiri makubwa hata siku moja mzee wa upako kaongea vyema kabisa maana zipo taratibu zinazo fahamika ujinga hufanywa na wajinga pekee
Kwa hiyo mzee wa upako anakuwa right Muda wote. Acheni kushikwa akili na matapeli..
 
Ndo maana kikwete hakutaka kuweka majina hadharani. Mtikisiko MTANDAO wa madawa mtahangaika Sana kuteteana. Jiwe limetupwa penyewe
Nawewe acha kiherehere. Unaongea pumba kila sehemu

Una biashara/dhamana yoyote katika jamii uelewe ubaya wa kuchafuliwa personality yako kwa tuhuma za kuhisi tu?

Mbona watu mnakosa busara hivi? Una miaka mingapi? Una kazi yoyote unafanya?

Uwe na kiasi kwa mambo yako.
 
Mzee wa Upako' ajitaja sakata la dawa za kulevya
WEDNESDAY , 8TH FEB , 2017
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) Ubungo-Kibangu jijini Dar, Lusekelo Anthony 'Mzee wa Upako' amejitaja kuwa ni mmoja kati ya watu mashuhuri ambao wamewahi kutuhumiwa kuhusika na biashara ya dawa za kulevya.

amefunguka na kusema kuwa yeye ni mhanga wa suala hilo jambo ambalo lilimpa wakati mgumu sana katika maisha na kumfanya kunyanyapaliwa na jamii pamoja na watu wake wa karibu wakiwemo wachungaji wenzake.
Mchungaji Lusekelo amesema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachofanyika kupitia ukurasa wa facebook wa EATV kila Jumatano kuanzia saa nane mchana hadi saa kumi jioni.
Lusekelo anadai kuwa mwaka 1997 alituhumiwa kuuza dawa za kulevya lakini anakiri wazi kuwa polisi wa kipindi kile walikuwa ni wastaraabu kwani waliamuandikia samansi na kumuomba kufika kituo cha polisi kutoa maelezo, hivyo anasema alifika na kutoa maelezo yake lakini taarifa hiyo ilivuja mtaani jambo lililopelekea watu kumtenga.
"Mimi ni mhanga wa dawa za kulevya mwaka 1997 nilituhumiwa kuwa nauza madawa, lakini wale askari walikuwa wastaarabu, waliniandikia samasi nikafika kutoa maelezo yangu, lakini baadaye niliwaambia kuwa wao ni polisi wafanye uchunguzi wao, walifanya uchunguzi na kugundua mimi sihusiki, watu walifuatilia na kugundua siyo kweli, na kila mtu akajitoa kwenye, ilionekana kuwa ni wivu tu, ila mbaya zaidi ile taarifa kuwa niliitwa polisi kwa madawa ya kulevya ilivuja, hadi wachungaji wenzangu walininyanyapaa, nikivaa suti au nikiendesha gari kila anajua ni pesa za madawa" alisema Mzee wa Upako

Paul Makonda - Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye kwa takriban wiki moja amekuw akitaja watu mbalimbali wanaodaiwa kuhusika na dawa za kulevya ambapo katika majina 65 aliyotaja leo, limo jina la Mchungaji Josephat Gwajima
Mzee wa Upako ameshauri vita ya dawa za kulevya kwa watu wanaotuhumiwa ni bora viongozi wangetumia njia za kipolisi kuwataka kufika polisi kwani kutumia njia ya magazeti inaweza kushusha heshima ya baadhi ya watu ambayo wameijenga kwa miaka mingi.
"Mimi kutokana na tuhuma zangu kuvuja kuwa niliitwa polisi kwa madawa ya kulevya niliishi miaka saba watu wananinyayapaa, tena hiyo ni tuhuma tu. Imenichukua miaka saba kusafisha jina, nimekuja kuanza kusafisha jina mwaka 2005 hivi"
Amesema yeye binafsi anachukia sana dawa za kulevya kutokana na madhara yake kwa jamii, hivyo hawezi kuthubutu kujihusisha nazo wala hawezi kuunga mkono watu wanaofanya shughuli hizo kwa kuwa dawa za kulevya zinaua kizazi cha maendeleo na taifa kwa ujumla.
Baadhi ya watu katika kipindi hicho walitaka maoni yake kuhusu Mchungaji Josephat Gwajima kuhusishwa na dawa za kulevya ambapo Lusekelo alisema hawezi kulizungumzia suala hilo na kutaka watu wasubiri hadi mwisho wake ufike ndipo na yeye anaweza kusema lolote.

Mchungaji Josephati Gwajima
Pia alishauri watu wanaowataja viongozi waliojijenga kwa muda mrefu kama Mchungaji gwajima wanapaswa kuwa na uhakika na ushahidi mkubwa usio na shaka, maana ikija kubainika kuwa siyo kweli, litakuwa ni kazi ngumu kwa viongozi hao kujisafisha kama ilivyomtokea yeye mwaka 1997.
"Kama kweli kuna wachungaji wanajihusisha au wanadhaniwa kuhusika kwenye madawa ya kulevya nashauri tungetumia njia ya wao kuitwa kwa samasi, tunapaswa kuwa makini katika hili kwani kujenga heshima ni kitu kikubwa, njia ya kuwaita watuhumiwa kwa njia ya magazeti si jambo nzuri kabisaa" amesisitiza Mzee wa Upako
Kwa wale waliotaka kujua jinsi anavyomuelewa Mchungaji Gwajima, Lusekelo amesema kuwa Gwajima ni rafiki yake, na wanaheshimiana sana.
 
Mzee wa upako akihojiwa EATV kipindi cha kikaangoni, aliulizwa swali kuhusu mchungaji Gwajima kutajwa kujihusisha na madawa ya kulevya
Amedai kuwa na yeye pia alishawahi kutuhumiwa kujihusisha na madawa ya kulevya mwaka 1997 lakini hakuitwa kwa staiili ya Makonda, amesema aliandikiwa summons kwenda polisi na baadae upelelezi ulipokamilika wakamwachia.



Japo ilifanyika bila kutajwa kwenye vyombo vya habari ila ilimuathiri kwa kuwa ilivuja na watu wakawa wanamnyanyapaa kwa kipindi cha miaka 7 kuwa yeye ni mfanyabiashara wa madawa ya kulevya.
Amesema hadi umtaje mtu yapasa uwe na ushahidi kuwa anafanya na sio kutaja tu kwenye vyombo vya habari kwa kuwa umeambiwa
 
Angewaita kimya kimya watu wangesema anawaogopa hii nchi watu ni wanafiki sana
 
SAKATA LA DAWA ZA KULEVYA: Maneno ya mchungaji Lusekelo Baada ya kutwaja Askofu Gwajima



DAR ES SALAAM. Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ ameshauri kuwapo kwa utaratibu maalumu wakati wa kuwaita kwa mahojiano watu wanaoitwa kwa mahojiano kuhusu dawa za kulevya.

Mzee wa Upako alisema hakukuwa na umuhimu wa vyombo vya habari kuhusika katika kuwataja watu hao hasa viongozi wa dini, bali wangeitwa kwa barua maalumu. Alisema inapotokea wachungaji wakahusishwa na dawa za kulevya ni muhimu kuwapo na ushahidi wa kutosha kinyume na hapo, itawavunjia heshima yao.

Mzee wa Upako alisema anaunga mkono kwa asilimia zote vita dhidi ya dawa za kulevya ila hajafurahishwa na namna suala hilo linavyofanyiwa kazi hali inayoweza kuwaharibia watu heshima.

“Kujenga heshima ni kazi kubwa sana inaweza kuchukua muda mrefu kuirudisha kama ilivyokuwa. Utakuta mtu ametumia muda mrefu kujenga jina lake halafu unakuja kumharibia, maisha ya mtu ni heshima yake, itamvuruga kwa muda na kumuachia kidonda kikubwa kujenga upya heshima yake.

“Binafsi sioni sababu ya vyombo vya habari kuhusika katika suala hili, ndiyo maana nasisitiza ni muhimu kuwa na ushahidi siyo kumtuhumu bila uthibitisho.”

Alisema ni vyema taratibu za kisheria zikafuatwa na ngazi husika zikachukua jukumu hilo bila kuingiliwa.

“Usalama wa nchi una intelejensia zake, naamini watu wa usalama wangeshughulikia suala hili kupitia Kamanda Siro au Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya wao wanajua wanafanya vipi kazi yao, huwezi kwenda kwenye vyombo vya habari kumuita unayemshuku,” alisema.

Akizungumzia sakata la Josephat Gwajima kutajwa kwenye orodha hiyo, Mzee wa Upako alisema hayo yaliwahi kumkuta yeye mwaka 1997.

“Niliwahi kutajwa nauza dawa za kulevya mwaka 1997. Askari walitumia busara nikaitwa makao makuu ya Polisi wakaniambia natuhumiwa, nikawaambia fanyeni uchunguzi. Walipogundua kuwa sina makosa wakaamua waniache.

“Niliishi miaka saba wachungaji wenzangu wakininyanyapaa kila nilichofanya ilionekana ni dawa za kulevya. Ilitumia muda mrefu kusafisha jina langu,” alisema.

Chanzo: Vipanga blog
 
"Raymond" yeye anatafuta "kiki" hata aseme nani hawezi kumsikia labda "baba" yake.
 
Back
Top Bottom