RIP Timoth Apiyo au Baba IKU.
Hakika nimepata mshtuko mkubwa kusikia kifo cha Mzee wetu Apiyo. Kwa wengine ambaye tulifanyakazi naye kwa ukaribu sana tunamkumbuka namna alivyokuwa mchungu na mwenye uzalendo wa hali ya juu sana.
Nakumbuka mwanzoni mwa miaka ya 80's akiwa kule Majumba sita (Sitakashari njia ya kwenda Segerea Seminari) akiwa na majirani zake Mzee Brown Ngwirurupi (aliyekuwa Meneja mkuu Sigara TCC), Mzee Simbila aliyekuwa mmoja kati ya wakuu wa magereza, Balozi Mwasakafyuka, Mzee Timoth Apiyo (au wengi tulizoea kumwita baba IKU), Meneja wa TZ Fishernet Mzee Mwakipesile (aliyekuwa mkuu wa mkoa Mbeya na Mbunge wa Kyera), na kakaye Wasira. Hilo ndio eneo alilokuwa anaishi wakti huoo bila shaka sasa litakuwa limeendelea zaidi.
RIP baba IKU ( Mzee T Apiyo.