Uchaguzi 2020 Mzee Sumaye ahoji wapi alipo Mbowe katika kampeni za Lissu

Wapambe wa kaburu Mkoloni mweusi ndiyo mtaumia sana pindi mtukufu akirejea kijijini chato pindi Nchi ikiwa imepata uhuru upya na kutawala kwa misingi ya HAKI
We unaongea nini? Tanzania ipo huru wala hakuna mkoloni.. Uhuru na haki gani unaoutaka? Mbona nchi ipo huru na watu wanafanya mambo kwa uhuru,haki gani unayotaka? Maana kama ni haki watu wanapatiwa haki zao. Japokuwa kuna idara kama polisi na mahakama zina dosari kidogo
 
Waziri Mkuu Mstaafi Mhe Frederick Sumaye ameeleza kusikitishwa kwake kwa Mbowe kumtelekeza Mgombea wake mara baada ya kuona Rais Dr John Pombe Magufuli anashinda kwa kishindo.

Sumaye amesema hayo leo katika Mkutano wa kampeni wa Rais Magufuli mjini Babati Mkoani Manyara leo.


Angalia mkutano wa Kampeni wa Tundu Lissu KARATU utapata majibu:
 
Uhalisia nikua kamati kuu haikuana mpango na Lisu wao walimtaka Nyarandu kwakua alisha jipanga katika swala la fedha za kampen. Walipo ona kuna shinikizo kutoka kwa wanachama wakaonaona isiwe tabu wamwachie Lisu msala alafu wao wa mute. Wanajua Lisu hawezi kutoboa na ndicho kinacho tokea
Lissu hawezi kutoboa nini wakati anawalaza nje kila siku? Amewanyoosha sana. Polepole na bashiru wakawadanganya eti chadema imekufa wakati jiwe sasa anaenda gereji kila wiki.
 
Mimi ni mwana ccm lakini kamati kuu ya chadema ingempitisha Nyalandu kuwa ndio mgombea wa chadema, asee ccm ingeshinda kwa zaidi ya 99%,walau Lisu kaleta changamoto kidogo na i hope ameuchangamsha huu uchaguzi wa mwaka huu.

Kushinda, kuleta ushandani, na kuchangamsha hivyo ni vitu tofauti.
Kuchangamsha hata yule mzee wa ubwabwa anaweza kuchangamsha!

Sisi tunataka kushinda, na sio kuchangamsha.
Watu kutoka CCM huwa wana kitu ila tunashindwa kuwaheshimu.
Mfano wenye nguvu ED alijaribu kufanya kitu 2015 bahati mbaya akadakwa dk 90 kabla filimbi ya kumaliza mechi haijapulizwa.
Tunataka watu kama hao, sio waongeaji sana ila wana mipango.
 
Mimi sishabikii chama chochote lakini hoja nyingine ukizisikia unashangaa.
Mbowe naye sinimgombea sasa ataachia jimbo liende apigie mtu kampeni.
Sumaye atuambie amemwona Mwenyekiti wa CCM akiongozana na Mgombea wake kama kweli ni lazma kila Mgombea Urais atembee na Mwenyekiti wa Chama Chake.
 
Sijui huyu mzee anatafuta nini kwa Magufuli. Kama ni mashamba hayatarudishwa. Au naye anataka watoyo wake wakumbukwe kama wa Lowassa na Pinda.
 
Back
Top Bottom