Uchaguzi 2020 Mzee Shomari: CHADEMA na mgombea wao wameingia kwenye mpambano huku kisaikolojia hawako sawa

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Mimi kama mzee mjuvi wa mambo najua umuhimu wa saikolojia kwenye mapambano. Bondia akiingia ulingoni huku anajua anaenda kushindwa tambua huyo hayuko sawa kisaikolojia. Maana atafanya vituko ulingoni,mnaweza kukuta anamg'ata mpinzani wake.

Hiki ndio kinachotokea hapa Tanzania. Lissu na chama chake walijua kuwa hawawezi kushinda urais na hata ubunge watapata kwa mbinde. Na sasa ndio tunashuhudia rafu na faulo ambazo zinaonyesha hawakuingia kupata ushindi,bali walijua watashindwa hivyo waanze faulo na rafu zisizo na maana ili mradi kuvuruga uchaguzi.

Inakuwaje mgombea urais ambae una uhakika wa kushinda uanze kutishia kupeleka watu the Hague?

Inakuwaje mgombea urais ambae una uhakika wa kushinda urais umtishie OCD kuwa utampandisha kwenye karandinga? Hii yote ni dalili kuwa Lissu alijua hawezi kushinda ila aliingia ili afanye faulo na vitisho kama hivi, maana kama una uhakika wa kushinda huwezi kutabiri vurugu.

Mbaya zaidi ni hili la kudanganya kuwa utafuta sheria zinazokandamiza uhuru wa kutoa maoni. Mbona hata Usa tunaona wanatunga sheria kudhibiti watu wanaotumia vibaya haki ya kujieleza!

Na hili la kusema utafuta ushuru wa vitambulisho vya wajasiriamali wadogo ina maana unataka kuturudisha kuwa tunalipa sh 500 kwa siku ambayo ni 15000 kwa mwezi?

Hili limekunyima kura kwa wajasiria mali wadogo kama mimi muuza kahawa. Na mimi nasema uligombea urais ukijua huna sifa,na huwezi kushinda ila umekuja kuleta faulo na vurugu kwenye uchaguzi.
 
Mzee Shomari ndio nani?
Ni busara ukajibu hoja zake.

Awali, humu JF nilitoa ushauri kuwa Lissu apatiwe mtaalamu wa mikakati ya kampeni, mtu kama wewe hamkunielewa.

Kinachotokea Lissu anajikaanga kwa lugha yake chafu mwenyewe. Akidhani anapata wafuasi wa kweli kumbe wanashangilia upuuzi wake.

Sera zake mbili zote (utawala wa majimbo na maendeleo ya watu) ameshindwa kuzieleza zikaeleweka na hata wewe The Boss huwezi. Nikuulize wewe kama wewe unahitaji nini ili ujiendeleze?
 
Huu uchaguzi ishu sio sera
Huu uchaguzi ni kuendelea na mabavu na watu
Kukosa Uhuru wa kukosoa na watu kupotea
Au tubadili tupate new start

Simple sana..
Hili la watu kupotea,hatua zipi zimechukuliwa? Wewe una ndugu na jamaa wangapi wamepotea?
 
Freedom of speech inaendana na freedom of idea kwa pamoja.Nahii ni move kwa ccm jiyahidini mschemshe.
 
Huu uchaguzi ishu sio sera
Huu uchaguzi ni kuendelea na mabavu na watu
Kukosa Uhuru wa kukosoa na watu kupotea
Au tubadili tupate new start

Simple sana..
Muda si mrefu vyombo husika vitawaacha midomo wazi kuhusu hizo tuhuma za kushambuliwa na kutekwa kwa viongozi wa kisiasa.

Pamoja na hilo, una amini Lissu atachaguliwa kwa sababu ya nyomi? Au kwa sababu ya kumdharilisha Magufuli?
 
Kwani hukutaka Maghufuli apingwe kwenye uchaguzi huu. Swala la kushindwa na kushinda yawe matokeo ya haki. Kwanini wafuasi wa Ccm hampendi kisikia neno haki ?!
 
Ni busara ukajibu hoja zake.

Awali, humu JF nilitoa ushauri kuwa Lissu apatiwe mtaalamu wa mikakati ya kampeni, mtu kama wewe hamkunielewa.

Kinachotokea Lissu anajikaanga kwa lugha yake chafu mwenyewe. Akidhani anapata wafuasi wa kweli kumbe wanashangilia upuuzi wake.

Sera zake mbili zote (utawala wa majimbo na maendeleo ya watu) ameshindwa kuzieleza zikaeleweka na hata wewe The Boss huwezi. Nikuulize wewe kama wewe unahitaji nini ili ujiendeleze?
Iissu jamani Lissu jamani ni shida!
 
Back
Top Bottom