Mzee ruksa tunakuheshimu sana, hili la kumuongezea muda JPM noooo....

COARTEM

JF-Expert Member
Nov 26, 2013
3,598
3,644
Mzee anasema isingekuwa katiba ya nchi kuruhusu only 10 years ya kuwa Rais, yeye angependekeza Magufuli atawale muda wote bila ukomo. Kasema barrier ni Katiba ya nchi.
MY TAKE: Mzee ruksa amesahau kwamba nchi hii inawatu wazuri wenye vipaji zaidi ya JPM vya kuwa marais. Kama mfumo wa kutafuta marais ungekuwa wa haki na uwazi, Tanzania ina best presidential candidates kuliko hata huyu baba Jesca.
New-Doc-2017-06-27_15.jpg
 
View attachment 531291
Anajishushia sana. Utapingwa nchi nzima!
 
Hata yeye kuna watu walimpigia kampeni ili ongezewe kipindi. Wakati watu wakipiga hizo kampeni, yeye alinyamaza kimya, nadhani alifurahia. Mwalimu alikemea huo upumba.vu kwa nguvu zote. Kipindi cha Kikwete kuna watu walianza kampeni ili aje kuongezewa muda. Kikwete aliwakemea, ikawa kimya.

Kwa hiyo siamini wapiga kampeni hizi huwa kweli wanaamini kuwa kiongozi ni mzuri bali hunena maneno hayo kutokana na tabia za kinafiki. Na ukiwa na kiongozi mjinga mpenda madaraka, hufurahia sana akiwapata hao wanafiki ili apate sababu ya kuhalalisha tamaa yake ya madaraka.

Tunasema huo ujinga uliowakumba baadhi ya ndugu zetu katika Afrika, hatuutaki Tanzania. Mwalimu alionesha mfano, hatumtaki wa kuturudisha nyuma.
 
Haya mambo ya kubadilisha katiba ili kumruhusu rais aliyepo madarakani yalianza kusikika toka enzi za Mwinyi. Tatizo ni kwamba Mwinyi angeogoza bila kikomo tusingempata Mkapa, Mkapa angeogoza kikomo tusingempata Kikwete, Kikwete angeogoza Kikomo tusingempata huyu wa sasa.

Watu wajifunze kuheshimu katiba.
 
Back
Top Bottom