Mzee Ruksa hatarini kutua mahakamani

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
102,120
2,000
Mzee Ruksa hatarini kutua mahakamani
www.ippmedia.com/sw/habari/mzee-ruksa-hatarini-kutua-mahakamani

Sakata la baadhi ya vigogo wastaafu na wa sasa serikalini, pamoja na wakazi zaidi ya 4,000 wa vijiji vinne vilivyopo Mwanambaya Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani, kupatiwa notisi ya siku 21 kuhama maeneo hayo kwa ajili ya kupisha mipango miji, sasa limeingia katika sura mpya, baada ya Kampuni ya Ardhi Plan iliyowataka wahame sasa kufika mahakamani ili waondolewe kwa nguvu akiwamo Mzee Mwinyi.

Baadhi ya vigogo wengine zaidi ya Mzee Mwinyi ambao wanakumbwa na mkasa huo Waziri Mkuu mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim; Balozi wa Tanzania Malaysia, Dk. Ramadhani Dau; Jaji Kiongozi mstaafu, Hamis Msumi; Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba; Naibu Waziri wa Fedha wa zamani, Adam Malima na Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega. Malima pia alikuwa mbunge wa Mkuranga.

MWAKILISHI WA KAMPUNI
Mwakilishi kutoka Kampuni ya Ardhi Plan Ltd, Luziga Bundara, aliiambia Nipashe kuwa, wameshafungua kesi namba 98 ya mwaka 2016 katika Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi na kukabidhi samansi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Munde Mushamu.

Samansi zingine zimepelekwa kwa watendaji wa vijiji ambao watawasimamia wananchi wao katika kesi.

“Ofisi ya mkurugenzi pamoja na watendaji wa vijiji tumeshawapatia samansi toka mwishoni mwa Desemba mwaka jana na tunaimani mahakama ndio itatenda haki,” alisema.

Bundara alisema anasikitishwa na taarifa ambazo zinatolewa na baadhi ya viongozi wa wilaya kuwa waliokuwa wanayalipia hawatakiwi kuyapata maeneo hayo kutokana na kuyatelekeza. Alisema maeneo hayo hayajatelekezwa mpaka sasa yanalipiwa kodi katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Bundara alisema maeneo hayo yamekuwa yakimilikiwa na Kareem Manji na Rajani Manji tangu mwaka 1952 na wamekuwa yakilipiwa kodi na kwamba yana ukubwa wa ekari 2,472.

Bundara alisema uamuzi wa kutoa notisi ya siku 21 umetokana na wanakijiji kugomea uendelezwaji wa mipango miji katika maeneo hayo.

MBUNGE MKURANGA
Kwa mujibu wa Mbunge Mkuranga, Abdalaah Ulega, ambaye nae ni miongoni mwa watu wanaotakiwa kuhama maeneo hayo katika mkutano uliowakutanisha wakazi kutoka vijiji vinne vya Luzando, Mipeko, Mlamleni na Mwanambaya, hawawatambui kina Kareem Manji na Rajani Manji na wanatarajia kumwandikia barua Rais John Magufuri ili hati ya umiliki wa shamba hilo ufutwe.

Ulega alisema tangu mwaka 2012 ana hati za umiliki wa eneo hilo, hivyo yeye ni mkazi halali.

“Wanasema tutoke, sisi tupo hapa kihalali na kama hilo ni eneo lao mbona walishindwa kuliendeleza, baada ya kuona watu wamejenga wao ndio wanaibuka na kudai hilo ni eneo lao na kutoa notisi ya siku 21 ya kututaka tuhame,” alisema Ulega.

Alisema katika kuhakikisha wanafanikiwa kumzuia huyo anayejiita mwekezaji kuwasumbua wananchi, mikutano ya vijiji husika itafanyika na mihtasari itaandaliwa ambayo itawasaidia kutopokonywa haki yao na Baraza la Madiwani litaandika barua ya kumwomba Rais kufuta hati ya umiliki.

Alisema ana imani na serikali ya Rais Magufuli inawasikiliza na kuwasaidia wanyonge, hawezi kuacha watu wake wakikosa pa kuishi kwa maslahi ya hao ambao wanajiita wawekezaji.

KAULI YA DC

Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Sanga Filibert, alisema hana pa kuwahifadhi wanavijiji zaidi ya 4,000 ambao wanatishiwa kuondolewa katika maeneo yao.

Aliwataka wananchi kutokuwa na wasiwasi kwa kuwa uongozi wa wilaya uko pamoja nao katika kuhakikisha suala hilo linafanyiwa kazi na mwishowe kubainisha mmiliki halali ni nani.

Aliongeza kuwa kuna baadhi ya watu ambao hutumiwa na mwenye fedha katika kuwaonea watu wasio na uwezo wa kufedha na kwamba sheria zipo na haki itatendeka.

MWENYEKITI HALMASHAURI
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Juma Abeid, alisema hawatishiki kupelekwa mahakamani kwa kuwa wananchi wa eneo hili wanaishi kihalali.

Alisema shamba hili lilitelekezwa zaidi ya miaka 50 bila kuendelezwa.

Abeid aliongeza kuwa anashangaa kuona wanaojiita wawekezaji wanaibuka sasa kudai ni wamiliki halali baada ya wanakijiji kupewa na kuliendeleza.

Alisema sheria itatumika na itatoa haki kwa wananchi kutokana na kumiliki maeneo hayo tangu yakiwa mapori hadi kuendelezwa na kujengwa nyumba za kisasa.

MWANASHERIA

Mwanasheria wa Wilaya Halmashauri hiyo, Salum Ally, alisema katika mkutano huo kuwa watu wa Kampuni ya Ardhi Plan hawana mamlaka ya kuwapa notisi wanakijiji hao ya kuhama, bali mahakama pekee.

DEC AFAFANUA

Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Mshamu Munde, aliwataka wananchi kutokuwa waoga kwani halmashauri ipo kwa ajili ya kuwatetea na kuona haki inapatikana.

Alisema anachokumbuka ni kuwa watu wa Ardhi Plan walifika katika ofisi yake na kumweleza juu ya kuweka mipango miji katika vijiji hivyo na kwamba aliwapa baraka na akawataka baada ya kufanya mazungumzo na wenyeviti wa vijiji na vitongoji wampe mrejesho.

Hata hivyo, Munde alisema hakupata mrejesho ya kile walichokizungumza, zaidi ya Desemba 20 mwaka jana ndipo alipopelekewa notisi ambayo pia ilipelekwa katika ofisi ya Kijiji cha Mwanambaya ikiwa na ujumbe wa kuwataka watoke kwenye mashamba hayo ndani ya siku 21.

Alisema anasikitishwa na baadhi ya taarifa ambazo zinadai yeye aliwakubalia watu wa Ardhi Plan kwenda vijijini kuwapimia viwanja wanakijiji.

“Nashangaa baadhi ya watu kusema mimi ni miongoni mwa watu ambao nimewaambia watu wa Ardhi plan kwenda vijijini kupima ardhi, mimi niliwaambia wafike ofisi za watendaji na kufanya nao mazungumzo katika hiyo mipango miji na kama watakubaliana niletewe taarifa, lakini sikuletewa taarifa mpaka hapo ilipokuja hiyo notisi ya siku 21 ya kuwataka wanavijiji wahame,” alisema Munde.

MWENYEKITI WA KIJIJI
Awali, Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwanambaya, Leila Chaduma, alisema katika mkutano wa hadhara wa wanakijiji kuwa alipelekewa notisi ya siku 21 awape wanakijiji ili wayahame maeneo hayo.

Alisema baada ya kupewa notisi hiyo, alikutana na baadhi ya viongozi na kwenda hadi ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji na notisi hiyo kisha ulifanyika mkutano ambapo wanakijiji walipinga kuhamishwa katika maeneo hayo.

Mwenyekiti huyo aliiambia Nipashe kuwa baadhi ya vigogo wanaomiliki mashamba na nyumba Mwanambaya ni Mzee Mwinyi, Dau, Jaji Joseph Warioba, Hamis Msumi, Dk. Salim, Malima na Ulega.
 
stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
21,638
2,000
Maswala ya ardhi hua ni magumu sana! Mahakama hua inaangalia root of title kama title hakuna ila kama IPO! Mwenye hati ndiye mmiliki halali!
 
August

JF-Expert Member
Jun 18, 2007
6,193
2,000
Bundara alisema maeneo hayo yamekuwa yakimilikiwa na Kareem Manji na Rajani Manji tangu mwaka 1952 na wamekuwa yakilipiwa kodi na kwamba yana ukubwa wa ekari 2,472.''
Hivi Hawa wamiliki walisha fanya maendeleo yoyote Hapo iwe kulima au kujenga hata nyumba Za wafanyakazi Kama si ya Meneja wa shamba ??
 
spencer

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
3,487

Huyo bundarla ni Jipu
 
Mwanitu

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
910
500
Kwa nini huyu Bwana anakuwa na kesi nyingi hivo.Je ile kesi ya Quality Plaza imekwisha?
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
24,959
2,000
Mzee Ruksa hatarini kutua mahakamani
www.ippmedia.com/sw/habari/mzee-ruksa-hatarini-kutua-mahakamani

Sakata la baadhi ya vigogo wastaafu na wa sasa serikalini, pamoja na wakazi zaidi ya 4,000 wa vijiji vinne vilivyopo Mwanambaya Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani, kupatiwa notisi ya siku 21 kuhama maeneo hayo kwa ajili ya kupisha mipango miji, sasa limeingia katika sura mpya, baada ya Kampuni ya Ardhi Plan iliyowataka wahame sasa kufika mahakamani ili waondolewe kwa nguvu akiwamo Mzee Mwinyi.

Baadhi ya vigogo wengine zaidi ya Mzee Mwinyi ambao wanakumbwa na mkasa huo Waziri Mkuu mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim; Balozi wa Tanzania Malaysia, Dk. Ramadhani Dau; Jaji Kiongozi mstaafu, Hamis Msumi; Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba; Naibu Waziri wa Fedha wa zamani, Adam Malima na Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega. Malima pia alikuwa mbunge wa Mkuranga.

MWAKILISHI WA KAMPUNI
Mwakilishi kutoka Kampuni ya Ardhi Plan Ltd, Luziga Bundara, aliiambia Nipashe kuwa, wameshafungua kesi namba 98 ya mwaka 2016 katika Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi na kukabidhi samansi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Munde Mushamu.

Samansi zingine zimepelekwa kwa watendaji wa vijiji ambao watawasimamia wananchi wao katika kesi.

“Ofisi ya mkurugenzi pamoja na watendaji wa vijiji tumeshawapatia samansi toka mwishoni mwa Desemba mwaka jana na tunaimani mahakama ndio itatenda haki,” alisema.

Bundara alisema anasikitishwa na taarifa ambazo zinatolewa na baadhi ya viongozi wa wilaya kuwa waliokuwa wanayalipia hawatakiwi kuyapata maeneo hayo kutokana na kuyatelekeza. Alisema maeneo hayo hayajatelekezwa mpaka sasa yanalipiwa kodi katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Bundara alisema maeneo hayo yamekuwa yakimilikiwa na Kareem Manji na Rajani Manji tangu mwaka 1952 na wamekuwa yakilipiwa kodi na kwamba yana ukubwa wa ekari 2,472.

Bundara alisema uamuzi wa kutoa notisi ya siku 21 umetokana na wanakijiji kugomea uendelezwaji wa mipango miji katika maeneo hayo.

MBUNGE MKURANGA
Kwa mujibu wa Mbunge Mkuranga, Abdalaah Ulega, ambaye nae ni miongoni mwa watu wanaotakiwa kuhama maeneo hayo katika mkutano uliowakutanisha wakazi kutoka vijiji vinne vya Luzando, Mipeko, Mlamleni na Mwanambaya, hawawatambui kina Kareem Manji na Rajani Manji na wanatarajia kumwandikia barua Rais John Magufuri ili hati ya umiliki wa shamba hilo ufutwe.

Ulega alisema tangu mwaka 2012 ana hati za umiliki wa eneo hilo, hivyo yeye ni mkazi halali.

“Wanasema tutoke, sisi tupo hapa kihalali na kama hilo ni eneo lao mbona walishindwa kuliendeleza, baada ya kuona watu wamejenga wao ndio wanaibuka na kudai hilo ni eneo lao na kutoa notisi ya siku 21 ya kututaka tuhame,” alisema Ulega.

Alisema katika kuhakikisha wanafanikiwa kumzuia huyo anayejiita mwekezaji kuwasumbua wananchi, mikutano ya vijiji husika itafanyika na mihtasari itaandaliwa ambayo itawasaidia kutopokonywa haki yao na Baraza la Madiwani litaandika barua ya kumwomba Rais kufuta hati ya umiliki.

Alisema ana imani na serikali ya Rais Magufuli inawasikiliza na kuwasaidia wanyonge, hawezi kuacha watu wake wakikosa pa kuishi kwa maslahi ya hao ambao wanajiita wawekezaji.

KAULI YA DC

Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Sanga Filibert, alisema hana pa kuwahifadhi wanavijiji zaidi ya 4,000 ambao wanatishiwa kuondolewa katika maeneo yao.

Aliwataka wananchi kutokuwa na wasiwasi kwa kuwa uongozi wa wilaya uko pamoja nao katika kuhakikisha suala hilo linafanyiwa kazi na mwishowe kubainisha mmiliki halali ni nani.

Aliongeza kuwa kuna baadhi ya watu ambao hutumiwa na mwenye fedha katika kuwaonea watu wasio na uwezo wa kufedha na kwamba sheria zipo na haki itatendeka.

MWENYEKITI HALMASHAURI
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Juma Abeid, alisema hawatishiki kupelekwa mahakamani kwa kuwa wananchi wa eneo hili wanaishi kihalali.

Alisema shamba hili lilitelekezwa zaidi ya miaka 50 bila kuendelezwa.

Abeid aliongeza kuwa anashangaa kuona wanaojiita wawekezaji wanaibuka sasa kudai ni wamiliki halali baada ya wanakijiji kupewa na kuliendeleza.

Alisema sheria itatumika na itatoa haki kwa wananchi kutokana na kumiliki maeneo hayo tangu yakiwa mapori hadi kuendelezwa na kujengwa nyumba za kisasa.

MWANASHERIA

Mwanasheria wa Wilaya Halmashauri hiyo, Salum Ally, alisema katika mkutano huo kuwa watu wa Kampuni ya Ardhi Plan hawana mamlaka ya kuwapa notisi wanakijiji hao ya kuhama, bali mahakama pekee.

DEC AFAFANUA

Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Mshamu Munde, aliwataka wananchi kutokuwa waoga kwani halmashauri ipo kwa ajili ya kuwatetea na kuona haki inapatikana.

Alisema anachokumbuka ni kuwa watu wa Ardhi Plan walifika katika ofisi yake na kumweleza juu ya kuweka mipango miji katika vijiji hivyo na kwamba aliwapa baraka na akawataka baada ya kufanya mazungumzo na wenyeviti wa vijiji na vitongoji wampe mrejesho.

Hata hivyo, Munde alisema hakupata mrejesho ya kile walichokizungumza, zaidi ya Desemba 20 mwaka jana ndipo alipopelekewa notisi ambayo pia ilipelekwa katika ofisi ya Kijiji cha Mwanambaya ikiwa na ujumbe wa kuwataka watoke kwenye mashamba hayo ndani ya siku 21.

Alisema anasikitishwa na baadhi ya taarifa ambazo zinadai yeye aliwakubalia watu wa Ardhi Plan kwenda vijijini kuwapimia viwanja wanakijiji.

“Nashangaa baadhi ya watu kusema mimi ni miongoni mwa watu ambao nimewaambia watu wa Ardhi plan kwenda vijijini kupima ardhi, mimi niliwaambia wafike ofisi za watendaji na kufanya nao mazungumzo katika hiyo mipango miji na kama watakubaliana niletewe taarifa, lakini sikuletewa taarifa mpaka hapo ilipokuja hiyo notisi ya siku 21 ya kuwataka wanavijiji wahame,” alisema Munde.

MWENYEKITI WA KIJIJI
Awali, Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwanambaya, Leila Chaduma, alisema katika mkutano wa hadhara wa wanakijiji kuwa alipelekewa notisi ya siku 21 awape wanakijiji ili wayahame maeneo hayo.

Alisema baada ya kupewa notisi hiyo, alikutana na baadhi ya viongozi na kwenda hadi ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji na notisi hiyo kisha ulifanyika mkutano ambapo wanakijiji walipinga kuhamishwa katika maeneo hayo.

Mwenyekiti huyo aliiambia Nipashe kuwa baadhi ya vigogo wanaomiliki mashamba na nyumba Mwanambaya ni Mzee Mwinyi, Dau, Jaji Joseph Warioba, Hamis Msumi, Dk. Salim, Malima na Ulega.
Classmate wangu huyu anakaelement ka ugenious na ukichaa no vigumu kujua kama ni "kichwa" au "mbatata"
Nani? Bundala?
 
misasa

JF-Expert Member
Feb 5, 2014
10,530
2,000
Eti rajan manji na kareem manji, bundara kamchomea mtu ambaye atopenya na ubabaishaji wake alikuwa anaohufanya katika serikali zilizopita, uyu mtanzania mwenye asili ya asia ana wakati mgumu sana sasa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom