Mzee Mwinyi ulikuwa mtu mzuri lakini sio Rais mzuri

Katika vitu nilivyompuuza navyo JK na genge lake ni kitendo cha kumtengenezea zengwe huyo mzee ambaye alikuwa tunu adimu ya taifa hili. Kundi la kina JK ndio lilikuwa kundi la uasisi wa gutter politics hapa nchini, na Salim alikuwa muhanga namba 1 wa siasa zile.
Na hiyo itatumaliza kabisa
 
Dogo wewe umezaliwa lini? unamjua Salim S. S.
unayajua makundi ya Hizbu na Shiraz
Je wenyewe Wazanzibar walisemaji uteuzi wake mpaka leo
usimsingizie Mwinyw wala Mongela
hata majuzi amegombea tena na Mwandosya, Sumaye, Lowassa na kadhaa kwanini ANASHINDWA
hizo fikra zako kazifiche huko huko

Wewe uko biased against Dr Salim na aina fulani ya watu. Kwa mantiki hiyo hutakubaliana na lolote lililo kinyume na unachokiamini. Regardless of the reality.
 
Katika vitu nilivyompuuza navyo JK na genge lake ni kitendo cha kumtengenezea zengwe huyo mzee ambaye alikuwa tunu adimu ya taifa hili. Kundi la kina JK ndio lilikuwa kundi la uasisi wa gutter politics hapa nchini, na Salim alikuwa muhanga namba 1 wa siasa zile.
Kwa macho ya utu na ubinadamu ni kweli jakaya na kundi lake walikosea.

Ila kwa jicho na mizania ya kisiasa wako sawa kabisa kwa kuwa siasa ina michezo yake na michezo yake ndio kama hii ya kupakana matope ili wewe uonekane mbora zaidi ni kama vile mnagombea mwanamke mmoja,nyie wanaume lazima kila mmoja aonyeshe ubora wake huku akimpaka matope mpinzani wake.

Ndio siasa hivyo na inafanyika duniani kote na kisiasa inaruhusiwa.
 
Niliziishi siasa za uteuzi wa mgombea Urais wa awamu ya pili ya uongozi wa Jamhuri ya Muungano 1985 wakati huo nikiwa mwana UVCCM mwandamizi. Hapa ndugu yangu Mfiaukweli umedanganya na umefiauongo. Miongoni mwa sababu z akuteuliwa Mzee Mwinyi nimafanikio makubwa ya transformation ya kiuchumi aliyofanya kwa kipindi alipokua Rais wa Zanzibar. Wakati huo Tanzania Bara hali ya kiuchumi ilikua tete sana

Yawezekana kuna mapungufu katika enzi za utawala wa awamu ya pili ya Mzee Mwinyi lakini sijaelewa unamaanisha kitu gani kusema Mzee huyo alitusababishia haya tunayoyakabili leo. Tunayakabili yapi mkuu? Kiuchumi,kisiasa au kijamii?
ILIFIKIA NGUO TUNAFUATA zanzibar, frigi, tv
 
Kwa macho ya utu na ubinadamu ni kweli jakaya na kundi lake walikosea.

Ila kwa jicho na mizania ya kisiasa wako sawa kabisa kwa kuwa siasa ina michezo yake na michezo yake ndio kama hii ya kupakana matope ili wewe uonekane mbora zaidi ni kama vile mnagombea mwanamke mmoja,nyie wanaume lazima kila mmoja aonyeshe ubora wake huku akimpaka matope mpinzani wake.

Ndio siasa hivyo na inafanyika duniani kote na kisiasa inaruhusiwa.

Sasa kama hayo yanakubalika kwenye siasa, Magu na Polepole huwa wanaposema tufanye siasa safi wanamaanisha nini?
 
'Mwinyi aliharibu Sana uchumi'

Tuelezeni kwanza Uchumi ilikuaje 1980-1985

Mwinyi kapewa Nchi Kila kitu hadi upate Dukani lazima uwe baunsa Sasa hivyo Viwanda vili Kuwa C inazalisha nini ?
Kwangu mimi, rushwa ilianza kupendwa na kupenya hadi mahali patakatifu, nilikuwepo, nilikua napenda siasa na nilikua msilizaji sana wa siasa na hata bungeni pia, yalikua yakiendelea hata kwa wafanya biashara nako nilikua najua. Nina mlaumu sana Mrema maanake hadi leo bado hajatoa tafsiri na neon "VIGOGO" baada ya kukamata mali zilizokua zinakimbizwa nje ya nchi. Well, just a tip, pitia uzi hu wa muungwana mmoja humu kauleta leohttps://www.jamiiforums.com/threads/unaikumbuka-hili-suala-la-mchele-mbovu-wa-dewji.1498656/
Hope unaweza kuelewa
 
undefinednakumbuka kuna kipindi Zanzibar ilikuwa Dubai ya East africa,watu walikuwa wanakwenda kufunga mzigo zenj,ilikuwa kipindi cha mwinyi ama Abdulwakil?
Hiyo biashara ya watu wa bara kwenda Zanzibar nadhani iliisha kipindi cha Mkapa hasa baada ya ujio wa kitu inaitwa VAT kwenye kodi zetu, nadhani ni miaka ya 97-98 hivi, ikaanza kuonekana hakuna faida ya kufata vitu Zenji na kuleta Bara cause is like hakuna tofauti ya bei. Nakumbuka mwanzoni mwanzoni Wazanzibari waligoma kutoza hi kodi na TRA bara walikamata magari yote yenye namba za zenji na ikaleta shida kidogo but TRA wakakomaa kwamba wao kwenye issues za Kodi, Zanzibar ni nchi nyingine kama ilivyo Kenya.
 
Wewe uliondika hiyo post ni mawili yawezekana kipindi Mwinyi anachukua uraisi ulikuwa mdogo au ulikuwa kwenu kijijini
Maana ukiwa kijijini tena kipindi hicho hata TV hakuna huwezi kuona mabadiliko ya kiuchumi
Alikuwa bado hajazaliwa
 
Kwangu mimi, rushwa ilianza kupendwa na kupenya hadi mahali patakatifu, nilikuwepo, nilikua napenda siasa na nilikua msilizaji sana wa siasa na hata bungeni pia, yalikua yakiendelea hata kwa wafanya biashara nako nilikua najua. Nina mlaumu sana Mrema maanake hadi leo bado hajatoa tafsiri na neon "VIGOGO" baada ya kukamata mali zilizokua zinakimbizwa nje ya nchi. Well, just a tip, pitia uzi hu wa muungwana mmoja humu kauleta leohttps://www.jamiiforums.com/threads/unaikumbuka-hili-suala-la-mchele-mbovu-wa-dewji.1498656/
Hope unaweza kuelewa
Sio nipitie uzi ngoja nikupe Darsa

Ili kujua eneo kina Rushwa Au laa jambo la kwanza Ni uwepo wa uhuru wa watu wa kujieleza Na kutoa maoni Yao

Mzee Mwinyi aliruhusu watu kutoa maoni Yao ndio sababu kukawa Na taarifa nyingi Sana Za Masuala ya Rushwa

Wakati wa Nyerere Alifuta Vyama vingi 1965, alitengeneza Sheria kandamizi ya Vyombo vya Habari 1976, Vyombo bya Habari vikabaki vya chama Na Serikal Sasa Ulitegemea habari Za Serikal Kuwa Na Rushwa kuzipata kupitia RTD?

Moja ya Malengo ya kuminya uhuru wa Habari ilikuwa kuficha Habari mbaya dhidi ya Serikal

Mpaka Nyerere anaondoka Mamlakani 1985 tayari Vyama vya ushirika vili kuwa hoi bin taabani, Viwanda almost vyote vilikuwa vimekufa sababu kubwa ikiwa ubadhirifu, unajua Kwanini kulikuwa Na operation uhujumu Uchumi 1982-1984?, Kama hujui ni kukithiri Kwa Rushwa Na ubadhirifu lakin mnasema hapakuwa Na Rushwa

Record Za Masuala ya Rushwa zinasema Fedha zimeanza kufichwa Kwny Bank Za Uswis 1974 jee wakati huo Rais alikuwa Nani?

Hata Mwinyi angekuwa Mbabe Na Adui wa uwazi Serikalin Pengine nae Habar Za Rushwa zisingepatikana
 
Kwangu mimi, rushwa ilianza kupendwa na kupenya hadi mahali patakatifu, nilikuwepo, nilikua napenda siasa na nilikua msilizaji sana wa siasa na hata bungeni pia, yalikua yakiendelea hata kwa wafanya biashara nako nilikua najua. Nina mlaumu sana Mrema maanake hadi leo bado hajatoa tafsiri na neon "VIGOGO" baada ya kukamata mali zilizokua zinakimbizwa nje ya nchi. Well, just a tip, pitia uzi hu wa muungwana mmoja humu kauleta leohttps://www.jamiiforums.com/threads/unaikumbuka-hili-suala-la-mchele-mbovu-wa-dewji.1498656/
Hope unaweza kuelewa

Kuna watu hawatakubaliana nawe japo ulichokisema ni ukweli mtupu. Hakuna serikali iliyoendeshwa Kiswahili kama Mzee Mwinyi. His presidency was hijacked and then managed by hooligans. Kudhoofika kwa governance system kulisababisha maamuzi ya hovyo kabisa. Bahati mbaya hakuna mtu yeyote ndani ya ccm ambae angetaka utawala wa sheria na kufuata misingi ya mfumo wa utawala usiotokana na matamko ya mtu mmoja. Wanajua the moment that happens ccm itajifia kama KANU, UPC etc.
 
Yaani kabla sijaso
Ama hujasoma ujumbe wangu au hujaelewa nilichoandika. Yawezekana kweli ulishiriki "siasa za uteuzi" na umetoa version yako. Mimi nimetoa version niliyoambiwa (na sio na mtu mmoja bali wengi tu na katika mazingira tofauti - kwa mantiki hiyo sioni uwezekano wa kuwepo collusion). Na hujaainisha hata hayo mageuzi aliyoyafanya Zanzibar kuhalalisha madai yako (kumbuka alikuwa Rais wa Zanzibar chini ya miaka miwili). Niachojua - na nina uhakika nacho ni kuwa ilikuwa lazima Rais wa awamu ya pili atoke Zanzibar.

Kwamba mapungufu yalikuwepo kwenye awamu ya pili halina ubishi. Moja ya mapungufu yake makubwa ni kuteua watu kwa kigezo cha udini - waliokuwa wamemzunguka kina Kighoma Malima, mkwewe Kitwana Kondo et al - wali-coin terminology "uwiano wa kikanda" kuhalalisha dhana ya "kurekebisha waislamu kubaguliwa kulikofanywa na awamu ya kwanza chini ya Mwalimu". Matokeo ilikuwa ni kudhoofisha mfumo wa serikali na kuwezesha kuwepo kwa familia zenye nguvu ambazo ziliweza kufanya chochote (imports za Stella Artois bila kulipia kodi, dhahabu kutoroshwa, mchele mbovu, mikataba ya hovyo kama IPTL etc).
Yapo mengi ila hali tuliyonayo leo imezidishwa ugumu kutokana na dismantling of the system hadi leo tuna de facto kingdom
Yaani kabla sijasoma bandiko lako nilishajua kuwa wewe ni baadhi ya misukule wafia dini, Mara nyingi ukimuona MTU anamnanga mzee mwinyi katika uraisi wake atakwambia aliwapendelea waislam na ukiona anamnanga Jk ujue fika hapo itasemwa dini ya uislam, chuki yako hata iweje haitabadili ukweli wa kwamba hawa waislam ni wabobezi katika hekima na busara za uongozi, hawana roho mbaya na mtu. Mwacheni mzee Mwinyi apumzike
 
Huyo anayeitwa Baba wa Taifa alitaka kupinduliwa baada ya watu kuchoshwa kula ugali wa yanga na ile hali ya Mama zetu kuvaa nguo za kupika!. Mchonga alichokwa na akataka kuondolewa pale magogoni, lakini leo ndio father of the nation.

Hakuna rais mzuri Tanzania, wote watakuja na kuondoka huku wakitolewa kila aina ya kasoro. Inategemea na mtazamo wa mtu binafsi. Mfano hawa wapendwa ambao ndugu zao wameachishwa kazi kwa sababu ya suala la vyeti, hawatakuja kumpenda JPM.

Kila mtu anaiongelea awamu fulani kadri ya maisha yake binafsi yalivyofaidika na awamu hiyo. Kila rais anayekuja na kuondoka huwa hafai, kumbe kutofaa kwake ni kadri ya mahangaiko yetu ya kila siku.
 
Tv radio magazeti nguo za mitumba barabara za lami pesa saa 4 asubuhi mfuko umejaa sinza mikocheni tegeta tabata zimejengwa enzi za mwinyi hakuna foleni ya petrol sukari sabuni kanga etc
 
Huyo anayesema Mwinyi aliteua "kidini", anaweza kuweka hapa Listi ya Baraza lake la Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, MaDC, Wakurugenzi etc kisha tulete na hali halisi ilivyo nchini kwa sasa tulinganishe?.

Kwa udini wa chinichini uliopo nchini, nadhani akitokea Raisi Muislamu akateua baraza la Mawaziri lenye Waislamu wengi zaidi kuliko Wakristo vigango vyote kelele zitakuwa ni miguno tu ya udini!! udini!! udini!. Ila kwa mfano hali halisi ilivyo kwa sasa ambapo Baraza la Mawaziri lina more than 80% Wakiristo, Hizo kelele huwezi kuzisikia!, Kwa maana inategemewa iwe hivyo!!!

Mfano mzuri ni huyu Mleta mada na hoja yake Muflisi dhidi ya Mzee Mwinyi.
 
Nyerere ndio alichangia hata huo uchumi kufa kwa kuwapa kipaombele makada wa ccm kusimamia viwanda.
Stori za vijiwe vya kahawa hizi.

Nawafahamu waliokuwa mameneja kadhaa waliosomeshwa na wakashindwa kusimamia Viwanda, na hawakuwa hata Makada.

Sanasana walijineemesha binafsi.
 
Stori za vijiwe vya kahawa hizi.

Nawafahamu waliokuwa mameneja kadhaa waliosomeshwa na wakashindwa kusimamia Viwanda, na hawakuwa hata Makada.

Sanasana walijineemesha binafsi.

Ma manager walikuwepo lakini maamuzi yalikuwa ya makada. Mfano mrahisi wa hao makada ni kama sasa hawa maDC na maRC, kawaulize wakurugenzi, waganga wakuu, mahakimu, maOCD, maRPC nk kama wanaweza kuwakatalia jambo lolote kwa kisingizio cha kulinda weledi.
 
Ama hujasoma ujumbe wangu au hujaelewa nilichoandika. Yawezekana kweli ulishiriki "siasa za uteuzi" na umetoa version yako. Mimi nimetoa version niliyoambiwa (na sio na mtu mmoja bali wengi tu na katika mazingira tofauti - kwa mantiki hiyo sioni uwezekano wa kuwepo collusion). Na hujaainisha hata hayo mageuzi aliyoyafanya Zanzibar kuhalalisha madai yako (kumbuka alikuwa Rais wa Zanzibar chini ya miaka miwili). Niachojua - na nina uhakika nacho ni kuwa ilikuwa lazima Rais wa awamu ya pili atoke Zanzibar.

Kwamba mapungufu yalikuwepo kwenye awamu ya pili halina ubishi. Moja ya mapungufu yake makubwa ni kuteua watu kwa kigezo cha udini - waliokuwa wamemzunguka kina Kighoma Malima, mkwewe Kitwana Kondo et al - wali-coin terminology "uwiano wa kikanda" kuhalalisha dhana ya "kurekebisha waislamu kubaguliwa kulikofanywa na awamu ya kwanza chini ya Mwalimu". Matokeo ilikuwa ni kudhoofisha mfumo wa serikali na kuwezesha kuwepo kwa familia zenye nguvu ambazo ziliweza kufanya chochote (imports za Stella Artois bila kulipia kodi, dhahabu kutoroshwa, mchele mbovu, mikataba ya hovyo kama IPTL etc).
Yapo mengi ila hali tuliyonayo leo imezidishwa ugumu kutokana na dismantling of the system hadi leo tuna de facto kingdom

Nilichomgundua Mtoa Mada Tatizo lake sio Mwinyi Bali Anashindwa Kuwa Muwazi kueleza Hasa alichokikusudia!
Lakini Ukisoma Kwa Makini Aliyoyaandika Utagundua Kuwa Anacholaumu Kuhusu Mwinyi Ni Mambo 2 tu:

1) Dini Yake
2) Uzanzibari
 
Poor you!
 
Kiuchumi,kisiasa au kijamii?

Mimi nadhani ni yote kwa pamoja.

Mzee Mwinyi aliingia na wimbo wa "Fagio la Chuma'" kumbe fagio lake lilikuwa bovu kabisa, sijui ilikuwa ni chuma gani kile.

Mambo yanayoendelea kujitokeza kwa sasa ndiyo yanayofunua ubovu wa utawala wake.

Kwa mfano uliotolewa humu JF wa Mtaalam (Mkemia Mkuu) kuuliwa kwa kufanya kazi yake ipasavyo na hao wauaji wakaneemeka kwa uharifu wao huo.

Taarifa hiyo sikuwa nayo hadi leo hii na imenifanya nizidi kuamini kuwa utawala wake ndio chanzo kikuu cha matatizo yetu mengi wakati huu.

Ni wakati huu wa Mzee Mwinyi ndipo tulipoanza kushudia CCM kuwa chama cha "Huyu ni Mwenzetu'; na haijawahi toka huko wala haitegemewi kubadilika.

Mzee Mwinyi ni mtu mpole nakadhalika, lakini hakufaa kabisa kuwa kiongozi wa nchi hii. Ametutupa shimoni zaidi.
 
Back
Top Bottom