Mzee Mwinyi, Mkapa, JK Na Sheikh Yahya! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzee Mwinyi, Mkapa, JK Na Sheikh Yahya!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Oct 24, 2011.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Oct 24, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,

  Katika nchi, uwepo wa uhuru wa kujieleza ni jambo muhimu sana. Maana, nchi haijengwi kwa dhahabu au almasi bali fikra za watu. Na katika nchi, uwepo wa fikra tofauti ni jambo jema kabisa.

  Na kwangu mimi, Mzee Mwinyi namwona kuwa ni mmoja wa WaTanzania ambao ametoa mchango mkubwa katika kujenga utamaduni wa kuvumilia fikra tofauti na hata zenye kushutumu. Na mpaka sasa, akiwa amebaki na miaka minne madarakani, Jakaya Kikwete namwona kuwa ni kiongozi anayeonyesha uvumilivu mkubwa wa fikra zenye kushutumu , hivyo basi, kuchangia katika kuimarisha misingi ya uwepo wa fikra huru, hivyo basi, demokrasia. Na kimsingi haya ya ufisadi yaliimarika zaidi enzi za Mkapa. Enzi za Mkapa hayakuwekwa wazi, lakini wakati huu wa Kikwete ameonyesha kuruhusu kuanikwa hadharani.  Ndugu zangu,
  Tuliokuwepo tunakumbuka, kuwa pamoja na mema ya Mwalimu, lakini, enzi za Nyerere hakukuwa na uhuru wa fikra. Na si kweli kuwa enzi za Ben Mkapa zilikuwa za Ukweli na Uwazi. Hicho kilikuwa ni kibwagizo tu cha kwenye mikutano na hotuba za Mheshimiwa.

  Na namkumbuka Mkapa kwa kauli yake hii; Tanzania hakuna waandishi wa habari. Akamsifu sana mwandishi Riz Khan akisahau kuwa naye ' Mkapa', alikuwa mwandishi wa habari na waziri wa habari katika Tanzania. Na Mkapa aliposema Tanzania hakuna waandishi wa habari labda alikuwa na maana, kuwa mwandishi wa habari aliyebaki alikuwa ni yeye tu!  Kauli ile ya Mkapa kwa wanahabari inanikumbusha miaka ile ya 80. Kwenye moja ya hitimisho la mifungo ya Ramadhan, Sheikh Yahya akatamka; " Ramadhan hii WaTanzania waliofunga ni wawili tu". Baada ya kusikia hayo ya Sheikh Yahya, basi, kilichonijia kichwani ni hiki; yumkini wawili hao waliofunga ni Sheikh mwenyewe na mkewe!


  Na ruksa kwa wenye kutaka kunishambulia kwa haya niliyoyaandika.


  Maggid,
  Njiani kwenda Iringa.
  MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo
   
 2. Pezzonovante

  Pezzonovante JF-Expert Member

  #2
  Oct 24, 2011
  Joined: May 1, 2008
  Messages: 643
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0

  ni kweli ulicho sema huwa najiuliz je tukimpa dr slaa atatuvumilia kama jk na mwinyi wanavyo vumilia, huwa nahisi kuna aya ya kulwani wazee hawa hujisemea kuvumilia julius, benny wote walikuwa wabaya sana kwa wale atakaye dhubutu kuwakosoa si unakumbuka mzee wangu ulimwengu benny alivyo fanya
   
 3. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #3
  Oct 24, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hakika Mjengwa kikwete angeweza kuwa nyuma ya baba wa Taifa kwa uongozi uliotukuka kama tiu angeshughulika na Mafisadi waliojijenga enzi ya Mzee Mweni na kuimarika wakati wa Mkapa.

  Kwa asilimia kubwa Kikwete anastahiki heshikma ya kusimamia demokrasia ya uhuru wa kujieleza na watu kupanuka uhuru wa kuzaungumza kwa uwazi na bila kufuatwa fuatwa na waliokuwa na maendekezo na mifumo ya kikomunist ya kuona kuwa kila anaezungumza Seriakli kwa mabaya yake basi huyo anatishia usalama wa Taifa.

  Watu hao naona kitengo hicho sasa kimejiishia, na kwa bidii zake Jakaya Kikwete ameacha watu waongee watafute majibu na wachukue hatua wenyewe.Hiyo ndiyo siasa na uendeshaji wa Serikali ambao Taifa hili alijapata kuwa nao toka uhuru.Japo kuna baadhi yua wenzie wanaona kuwa kwa yeye kuwa na mfumo huo wa utawala CCM inakufa kwa kuwa uconservative ule ulisaidia wezi wa Taifa kujificha chini ya kuatarisha Usalama wa Taifa na uchochezi na wivu wa kike, nk.

  Kikwete kwa kujua Dunia inakokwenda na UTANDAWAZI AMELIKOMBOA Taifa na mafundo ya roho yaliyogandamana miaka nenda rudi ambayo kwa hasira wakubwa hao wakaamua kuwa WEZI NA MAFISADI WA MALI YA UMMA.

  Ila kwa kuwa yuko nao umri mmoja wanaoneana aibu lakini kesha waanika kazi ni kwa umma kuchukua hatua.Ndio maana wenye akili zao wamempa Udaktari wa kutunuku wa sheria wakijua mchango wake huo.

  Ila nae kwa mapungufu yake ata hukumiwa kwa kukosa sura ya UKATILI KWA WAALIFU NA MAFISADI WA MALI YA UMMAA, hata kama ni wanalika lake.Taifa litakuwepo daima lakini watu watapita.
   
 4. Noti mpya tz

  Noti mpya tz JF-Expert Member

  #4
  Oct 24, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mjengwa, kuna kipindi upepo huwezi kuuzuia tena na inabidi uuache na kuutazama unavyoenda, JK ana hak ya kuuacha upepo wa mabadiliko utawale fikra za watu na hata kama angejaribu kuuzuia kwa sasa asingeweza.
  Dunia ya sasa imebadilika sana na hata kama angekuepo Mwl. bado upepo huu asingeweza kuuzuia, Mkapa nae kipindi chake kiliisha vile na watu walikuwa bado wamelala lakini alisaidia sana wao kuwaamsha hasa baada ya kufanya madude pale magogoni.
  Tuseme ukweli JK ni mtu wakuangalia upepo unaendaje na ndio maana kuna kipindi huwa anashindwa kufanya maamuzi akisubiria wananchi watareact vp, mfano mzuri ni suala la Jairo N.K
   
 5. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #5
  Oct 24, 2011
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  mjengwa , si Mzee Mwinyi wala Kikwete anayeweza kupambana na vyombo vya habari uso kwa uso.
  Hao watu si great thinker , japo namsamehe mzee Mwinyi kwa hili.
   
 6. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #6
  Oct 24, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kabisa kwa uhuru wa kujieleza JK amefanya nike sana (tick) hapa mnyonge mnyongeni lkn haki yake mpeni, Lakini pamoja na kuuwacha uhuru huo wa kujieleza kafanya kosa moja kubwa sana!!bora hata huo ufisadi!!! Yeye amejenga misingi ya mgawanyiko wa taifa letu! bora hata angezuia huo uhuru wa kujieleza kuliko kuanzisha sera za udini katika taifa hili! Keshatugawa bwana huyu na athari zake zitaonekana tu soon!
   
 7. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #7
  Oct 24, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  kwa maoni yangu ccm ya kuanzia kwa mzee mwinyi ni ileile yenye kila aina ya sumu ya kuwaumiza raia wa taifa hili. Mabadiliko chanya kidogo tunayoweza kuyapata yamelazimishwa na mwenendo wa mambo mengi duniani, hii haijatokana na mwinyi, mkapa wala kikwete. Wakati wa Nyerere pamoja na kuwa wa chama kimoja alikuwa anaweza kwenda Mlimani na kujadiliana na wasomi... hawa wengine watakanyaga mbele ya wasomi kama tu wamehakikishiwa kuwa kuna uwanja wa kutapika (kuhutubia) tu mambo yao na kukimbia. Hiyo ruhusa ya fikra huru tungeiona ktk vyombo kama TBC, wabunge wa ccm, Tume ya uchaguzi,mikataba na wawekezaji wezi iliyofichwa nk. Hali ya sasa imelazimisha kuwepo kwa vyombo binafsi vya habari. Hawana ujanja wanashindwa tu wafanyeje... Kama kuna muwazi atuwekee wazi ripoti ya kamati ya Mwakyembe na nyingine zote zilizofichwa.
   
 8. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #8
  Oct 24, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Jk karuhusu nini kuwawekea sumu watu wenyeinfluence kwa Taifa, enzi za mkapa haya hayakuwepo watu waliothubutu walionywa waziwazi na si kumruhusu mtu aseme afu baadaye unamwagia tindi kali ni vema ukamwambia kuwa bwana hatuhiytaji uendelee kuandika mambo fulani ya serikali kuliko kuwauaw coz tunapunguza nguvu ya Taifa. Fikiri akifa sasa Dr Mwakyembe na Prof Mwandosya tutakuwa tumepoteza nguvu kiasi gani. Kwa hiyo mi naona ni afadhali enzi za Mkapa kulikiwa na nidhamu watu walifanya kazi kwa nguvu rushwa haikuwa kama sasa, elimu iliimarika wafanyakazi walithaminiwa ila sasa ni kinyume chake. Maisha yalikuwa mazuri mfumko wa bei ulikuwa controlled lakin sasa ni poor, inflation rate ilikuwa 7% sasa 17% enzi za mwinyi 14% sasa unaweza ukaona nani alikuwa ni mchapa kazi. Kikwete anaacha watu waseme watakavyo coz anaongoza kwa kuangalia watu wanasemaje afu pia hawezi kujenga hoja, wakati Mkapa alikuwa anauwezo wa kujenga hoja na kuisimamia, hivyo Mkapa alikuwa anawazidi upeo wananchi wake na hivyo kutawala mijadala ya wananchi wakati Jk anaupeo mdogo wa kufikiria hivyo wananchi atafikiri zaidi kuliko yeye na ndo maana watu wanamengi ya kuzungumzza kuliko rais wao. Jk hata hotuba ya mwezi tu imemshinda Mkapa alikuwa anahotubia kila mwezi na alikuwa harudii hotuba hebu angalia Jk hotuba za kawaida anashindwa kujenga hoja anarudia hotuba hazina mvuto. Naona Mjengwa uache kumsafisha Jk umeshaanza na thread zako za kumsifia Jk, ulianza na ile ya Jk asijeakasahaulika tumenzi, sasa unaanza kusema Jk eti angeenza baada ya mwalimu tungekula hadi nyasi sasa tu maisha yako hivi je kipindi kile ingekuwaje. Alikuta mihela kibao lakini sasa deni la Taifa limeongezeka, nchi haikopesheki, serikali inakopa mpaka kwa Benki za watu binafsi hivi ni nchi kweli kwanini watu wasizungumze wakati wanona wanyama wanaibwa na serikali yao ipo kimya.
  Nimeandika kwa kuchanganya hoja sana coz natumia simu. Nipo tayari kurekebishwa
   
 9. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #9
  Oct 24, 2011
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,993
  Likes Received: 1,003
  Trophy Points: 280
  Faida kuruhusu uhuru wa kujieleza kwa rais yale yote mabaya ya kweli yanayomuhusu anaweza kuyamaliza kwa nguvu ya kikatiba aliyonayo.Mkapa kama angefuata nyayo za Mwinyi ya Kiwira,Bank M na Mchuchuma yasingemkuta.
   
 10. Linyakalumbi

  Linyakalumbi JF-Expert Member

  #10
  Oct 24, 2011
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 259
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Mkapa alisema Waandishi wa habari wa bongo hawafikirii na kutafiti cha kuandika,He was right & perfect.We mjengwa ndo unaandikaga mwananchi sio?Baba umefulia.Uhuru wa kujieleza ndio unatatua umasikini na kuleta maisha bora sio?Zama za uwazi na ukweli zilikuwa porojo,Maisha bora kwa Kila mtanzania imetimia sio?Akili Masaburi,we Mjengwa???EL kila siku anasema maamuzi magumu na ni swahiba wake dunia inajua,bado wewe ambaye huwezi hata kwenda muhoji unasema anafanya kazi JK,Mfuasi mtiifu wa Dict.Gadaffi sio,Huyu Vita ya 1978 hakuwa Jeshini sababu ya kuchekacheka ndio maana alimkumbatia huyu dictator,maafande wa hasira naye.Maoni yangu:
  (1)Mjengwa karudie ulichoandika.JK bado sana kuwa prez.
  (2)JK amefanikiwa sana Kuwagawa wa TZ kiudini,tazama alizuga eti hatuwezi warudishia shule Waislam,Tehe tehe,Hiv hawa wanashule Madrasa?
  (3)JK fitina na Majungu ndio mwake,alimponda Bern In-direct,yalipomshinda kamwangua ambebe kampeni zilizopita,Mzee wa Baniani Mbaya...
   
 11. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #11
  Oct 25, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ok topic hii ilikuwa nzuri lakini wachangiaji kiduchu ebu kaka mjengwa badilisha heading ili ipate mvuto please!
   
 12. k

  kiloni JF-Expert Member

  #12
  Oct 25, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 575
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Usisahau sumu za Kikomunisti zinazoua wapinzani wa mawazo ya JK. Mwakyembe, na mwenzake mwandosya!! bado wengine wanawindwa!! JK na demokrasia ya kinafiki.
   
 13. B

  Bigaraone JF-Expert Member

  #13
  Oct 25, 2011
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 722
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35

  usichanganye kati ya uzembe, woga, carefree na laxity na kuzifanya kuwa ndio principles zinazoongoza watu ambao umewapigia upatu. Mwinyi alikuwa mtawala mwoga asiyekuwa na maono (visionary) wala sifa za kiuongozi ndio maana allishia kutoa matamko tata.Hakufata sheria achilia katiba ambayo ndio sheria mama. Kiongozi wa kweli unatakiwa ueleze msimamo wako, sifa zako (defined values) ili watu wakuelewe ktk hilo.Sio kuwa na sifa ya popo mnyama upo na ndege upo. Unaleta ubepari na huku unasema wewe ni mjamaa. Haiwezekani afadhali uwe wazi kuwa mazuri kadha wa kadha ya kijamaa na mazuri kadha wa kadha yaungiwa s kibepari tunayaunganisha pamoja. Basi msimamo huo unatungiwa sheria.

  Lakini Mwinyi alishindwa ktk hilo na ndio maana historia haiwezi kumkumbuka hata kidogo. Haya maneno ya ruksa ni ubabaiishaji wa watu wasiofikiria kwa kina. Na watu wa aina ya Mwinyi huishia kuhalallisha mambo ya ajabu ili umma usiwahoji. Mtu unasema aliruhusu fikra tofauti??? Hapa pana maswali kweli.Fikra zipi hizo ambazo hazikuandikwa? Fikra zipi zisizokuwa na emperical example? Tuache kujidanganya labda aliruhusu ndugu zake, maswahiba wake na waharabu na wahidi kuipora mama Tanzania.

  Mwingine aliyepigiwa upatu in Kikwete. Birds of the same feather flock together.Huyu naye kama alivyo baba yake mwinyi ni wabaka utawala. Wote wameupata kwa hila, rushwa, ufisadi, na kuua sifa za watu (character assassination). Watu wa aina hii huwa hawana dira na mara zote hupenda kufanya vitu ambavyo vitawafurahisha watu wasiofikiria urefu zaid wa pua zao. Kwa kuwa wabongo wengi pamoja na mleta thread ni watu wasiopenda kupanua bongo zao mbali na urefu wa pua zao wanapenda kuitimisha bila empirical example hufuraishwa na watu wa aina ya kikwete. Kikwete ana sifa ya panya ya kula na kupuliza. Hawezi kutetewa ktk wizi na uporaji wa maliasili ya taifa hili. kuanzia mikataba mibovu ya madini akiwa waziri na nishati, iptl, buzwagi, loliondo, richmond, epa akisaidiana na mkapa na safari zake nje ya nchi. wizi wa kura uchaguzi 2010 na mengine yote.

  Na yeye kwa sababu anajua madhambi yake lazima ajifanye mtu wa watu kwa unadfiki mtupu. viongozi tunawaona wanaokwenda vijijini wakashiriki kuboresha mazingira na social services, wanapinga wizi na rushwa kwa vitendo, ni wakweli wa kauli zao na wanaongoza kwa vitendo-examplary leaders. Sio Kikwete hata mkitaka kumpamba sifa za kiongozi mwenye kuvumilia fikra mbadala kikwete hana.kwanza chama anachokiongoza hakina fikra ya kupigiwa mfano.kila mtu anasema la kwakwe hata yeye ametoa kauli tata na zenye kupingana. ili mtu avumilie fikra za wengine kwanza yeye awe na fikra na fikra ilinganishwe na fikra zingine duniani (empirical examples) ndipo hapo unaweza kusema anavumilia fikra za wengine. kwa kuwa hana falsafa inayomwongoza basi anaishia kujichanganya na kuadaa public kwa upole usii upole bali woga kwani anajua watu wanajua mabaya yake.

  Hajatoa uhuru wa aina yoyote na ndio maana zuri lolote linatoka upinzani analibeza. Kama uvumilivu wa fikra na kushindwa kuwakamata wezi wa fedha za umma hapo sawa.

  Mwalimu Nyerere huwezi kumlinganisha na wote hawa hafanani nao kwa busara (wisdom), akili (intellect), visionary(maono) na insiprational leadership(uongozi uliotukuka). Aliongoza kwa mifano, mwadilifu, mkweli, mwaminifu na mtu mwenye fikra pevu. Utasema hakuvumilia fikra mbadala lakini zipi. Toa mifano yenye ulinganifu na mazingira ya wakati huo (empirical example).kumbuka wengine hawa wametawala wakati vuguvugu la vita baridi limekwisha. Mwalimu aliongoza kuazia harakati za uhuru na kupitia kipindi kigumu cha harakati za vita baridi. lakini aliweza kuivusha nchi na kungatuka akiacha imejejaa maziwa na asali-watu wamoja, madini, mbuga za wanyama, ardhi tele, viwanda, shule nzuri, hopitali nzuri na vituo vya afya. leo viko wapi. Daktari na nesi wanatukana mgonjwa, polisi anamkamata aliyekuja kushtaki, hakimu anamhukumu mlalamikaji kisa hana fedha ya rushwa, viongozi hawawajibiki, uongozi ni bidhaa inayouzwa, rushwa njenje. Mwisho viongozi wanishia kutoa majibu mepesi ili wawafurahishe watu na nyie mnafikiri wanarug=husu mawazo mbadala na fikra tofauti. rudini darasani mkajenge hoja
   
 14. m

  maggid Verified User

  #14
  Oct 25, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Linyakalumbi,
  Asante sana. Niliyoyaandika ni mawazo yangu huru, nawe umeandika yako. Naheshimu na nitaupigania uhuru wako wa kujieleza hata kama sikubaliani na ulichoandika.

  Hivyo basi, sina cha kurudia bali kuongeza, kuwa bado naamini, kuwa inapohusu uhuru wa watu kujieleza so far JK is far better than waliomtangulia. Na uhuru huu unaweza kuwa transformed kwenye kukuza demokrasia na kuinua uchumi wa nchi kama utaimarishwa na kutumiwa vema.

  Nakumbuka enzi za Mkapa ndugu yangu Jenerali Ulimwengu alipatwa kuambiwa si raia wa nchi hii. Kubwa lilikuwa kumyamazisha na makala zake za 'Rai ya Jenerali'. Nakumbuka nilifunga safari kwenda nyumbani kwa Jenerali kule Mbezi Beach kumpa pole ya kuvuliwa uTanzania wake. Na pale nyumbani kwa Ulimwengu alikuja pia kaka yangu Salva Rweyemamu. Nami, nikiwa kijana mdogo, nikajikuta naishia kushiriki kupanga gazeti la Rai kutokea nyumbani kwa Ulimwengu ambae wakati huo alisemwa ' hakuwa raia' wa Tanzania. Historia ni mwalimu mzuri. Ndio maana ya kukumbushana haya.

  Nakumbuka pia, siku mbili kabla Kubenea na Ndimara Tegambwage kuvamiwa na Kubenea kumwagiwa Tindikali nilikuwa ofisini kwa Kubenea nikiwa pamoja na Ndimara. Ilikuwa usiku wa saa moja. Mimi na Ndimara tulikuwa na mabishano makali ya hoja. Ndimara Tegambwage alikuwa na msimamo kuwa mwanahabari hapaswi kuandika mazuri yanayofanywa na Serikali. Kwamba hiyo ni kazi ya Serikali yenyewe. Mimi sikuona tatizo kwa mwandishi kuwa na uhuru wa kuikosoa Serikali na hata wakati mwingine kuweka wazi pia mazuri yanayofanywa na Serikali.

  Siku mbili baadae, katika muda ule ule niliokuwapo pale ofisi za MwanaHalisi, Kubenea na Ndimara wakavamiwa na watu waovu. Kubenea akamwagiwa tindikali na Ndimara akajeruhiwa. Na bila shaka, kuna waliotaka kuwafunga midomo Kubenea, Ndimara na wengine.

  Kamwe tusikubali kurudi tena katika enzi za ubabe na vitisho vya wanasiasa kiasi hata cha kuwanyamazisha hata wanahabari.
  Maggid
   
Loading...