Mzee Malecela atakuwa "Tingatinga" kuipigia debe CCM yake? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzee Malecela atakuwa "Tingatinga" kuipigia debe CCM yake?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Quinine, Aug 8, 2010.

 1. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #1
  Aug 8, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,936
  Likes Received: 12,206
  Trophy Points: 280
  CCM imezoea kumtumia Malecela unapotokea uchaguzi ambao ni uncertainty, walifanya hivyo Busanda na Biharamulo. Kuna wakati niliwahi kumsikia Malecela akilalamika eti CCM inamfanya kama tingatinga kuwasafishia barabara baadaye hilo tingatinga haliruhusiwi kupita kwenye hiyo barabara.

  Sasa kwa kitendo cha wanaCCM wa Mtera kutomchagua tena ina maana hawana haja naye baada ya kuwasafishia barabara? au CCM itamhitaji kumtumia pindi kampeni zitakapoanza? Na je kwa kufanya hivyo Malecela hatajisikia kutumiwa kama tingatinga na baadaye kuachwa kama alivyowahi kusema? WanaJF mna maoni gani kwa hili, mtamshauri akatae au akubali kufanya kampeni.
   
 2. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #2
  Aug 8, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Afanye tu Kampeni Mimi Nitamdhamini aka Tingatinga
   
 3. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #3
  Aug 8, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,082
  Likes Received: 4,032
  Trophy Points: 280
  aingia chadema
   
 4. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #4
  Aug 8, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,936
  Likes Received: 12,206
  Trophy Points: 280
  sidhani kama huyu atahama ni wazee waliobaki na kina kingunge waliokunywa maji ya bendera ukimkata damu ni ya kijani.
   
 5. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #5
  Aug 8, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  ......mwaka huu wamempiga mzee malecela kote kote..anyway labda apoozwe kama Msekwa alivyopewa kazi baada ya kushindwa uspika...nadhani atamuuliza kama anautaka ubunge wa kuteuliwa akikubali ataweza kumteua....ila ni dhahiri kuwa JK alikuwa na kisasi na Malecela....,pamoja na kuwa mzee malecela alimsamehe Jk kwa tukio baya la mkewe kufanyiwa uhuni pale morogoro...na agents wa mutandawo....bado mzee malecela aliweza kuondoa kinyongo na kuendelea kukipigia chama kampeni za uchaguzi mdogo....
  Kimsingi mzee malecela ni mwana ccm wa kutupwa...na muumini wa demokrasia ....kwani alishawahi kushindwa ubunge miaka ya nyuma ......na akakubali matokeo ...akapelekwa kuwa mkuu wa mkoa Iringa...,alipata pia kushindwa urais mara mbili na amebaki mwana ccm....ni dhahiri kuwa ataendelea kuwa ccm ...damu ila hatumtegemei ampigie kikwete kampeni mwaka huuu!!
   
 6. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #6
  Aug 8, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mzee Malecela hakika hatahama CCM,ni mzee ni mvumilivu sana na ni most effective when pinned down.Ccm itafanya kosa kumtosa pamoja na uzee wake.Mimi ningemshauri sasa aandike memoirs zake
  na mapambano yake kisiasa
   
 7. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #7
  Aug 8, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Uhuni huo wa moro ni upi???
  Wengine tungependa kufahamishwa pia...
   
 8. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #8
  Aug 8, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Bana we...! huyu mtu kakataliwa kwao kama wenzake kwa kuwa hana mpya....hata hizo kampeni zikija haitwi tena!
   
 9. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #9
  Aug 8, 2010
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,974
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Jamani, wamwache huyu mzee apumzike kwa amani.
   
 10. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #10
  Aug 9, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,936
  Likes Received: 12,206
  Trophy Points: 280
  Huwezi kupumzika kwa amani kama bado unaishi duniani lazima utakuwa na utashi utakaokusukuma kutenda jambo ambalo hukulifanya wakati wa ujana wako hata kama hutafanikiwa angalau utajifariji umesikika..
   
 11. M

  MLEKWA Senior Member

  #11
  Aug 9, 2010
  Joined: Aug 18, 2007
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nafikiri mzee malecela nahitaji mabadiliko na mabadiliko hayo ni kufanya kama mrema alivyosema ccm sio baba angu wala mama yangu atimue zake kwani wanamtandao wamemmaliza makusudi huu ndio ukweli.
   
 12. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #12
  Aug 9, 2010
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Mkuu,binafsi namwona Malecela kama mroho wa madaraka as if alizaliwa kuwa kiongozi.Aliahidi 2005 kuwa angestaafu lakini kwa uroho wake wa madaraka akakiuka ahadi ya 2005.Kwanini hataki kujifunza kwa ex-PMs wenzake? Sasa record yake ya utumishi kwa umma imeingia doa kubwa zaidi.

  Malecela kuhamia upinzani ni ngumu kama kwa Makamba kuhamia upinzani.Hawa watu wawili wamewatukana sana wapinzani.Kauli zao kwa vyama vya upinzani zilitawaliwa na ngebe,kashfa na hata (equivalent to) matusi.

  Kwa uroho wa madaraka alionao Malecela sintoshangaa akifanya lobbying ya kupewa ubunge wa kuteuliwa kama si kuomba ubalozi nje ya nchi au hata U-DC.

  He can go to hell,just as he once told his voters.
   
 13. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #13
  Aug 9, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Kuna makosa mengine ukishayafanya, inakuwa ni vigumu sana kuyarekebisha tena. Lile la you can go to hell, amefanikuwa kulifuta kwa vile wengi wa watanzania wa leo hawalifahamu kabisa, lakini nadhani hili la kushindwa uchaguzi mwishoni mwa career yake litakuwa kubwa kwa vile ndilo litakalo husishwa sana na historia yake kisiasa, ingawa amewahi kushindwa uchaguzi tena mwaka 1985 baada ya you can go to hell. Nafikiri mwaka 1985 alishindwa na mtu anaitwa Kusupa ambaye hakuwa maarufu kabisa kiasi kuwa sijui aliishia wapi baada ya hapo ya uchaguzi wa mwaka 1990.

  Akiwa amefanya kazi serikalini kwa zaidi ya nusu karne, Malecela alitakiwa aachie madaraka kwa heshima, lakini alijidhalilisha sana kusubiri awe kicked out na watoto wadogo sana waliosoma chini ya mwongozo wake akiwa kama waziri. Sijui ndugu yangu Wassira naye atakuwa amepetaje, lakini naye anatakiwa afikirie tena kuachana na purukushani za kisiasa kwa vile atajikuta anatukanana na watu wanaolingana na watoto wake.

  Ningekuwa Malecela, ningeamua kukaa kimya kabisa na kuachana na mambo yoyote ya kisiasa na kuanza kula pensheni tu. Afterall watoto wake wote ni wakubwa na wana elimu na kazi nzuri tu, hivyo hana wasiwasi wa future ya familia yake tena.
   
 14. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #14
  Aug 9, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  Hata Winston Churchill alipata kushindwa uchaguzi long after his WWII heroics....na bado aliheshimika mpaka umauti ulipomfika....SIONI KWA NINI tumsakame Mzee wetu huyu...tunatakiwa kumpongeza kwa kukubali kushindwa...ndiyo demokrasia

  Sir Winston Leonard Spencer-Churchill, KG, OM, CH, TD, PC, FRS (30 November 1874 – 24 January 1965) was a British politician known chiefly for his leadership of the United Kingdom during the Second World War. He is widely regarded as one of the great wartime leaders. He served as prime minister from 1940 to 1945 and again from 1951 to 1955. A noted statesman and orator, Churchill was also an officer in the British Army, a historian, writer and artist. To date, he is the only British prime minister to have received the Nobel Prize in Literature, and the first person to be recognised as an honorary citizen of the United States.
  Although Churchill's role in the Second World War had generated him much support from the British population, he was defeated in the 1945 election
   
 15. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #15
  Aug 9, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  kuwasalimia na kuwapa warning ya kuanza kampeni kabla ya muda
   
 16. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #16
  Aug 9, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Huyu Jamaa alikuwa ang'oke 2005 akaomba Suluhu na Livingstone kwa ahadi kwamba asimpinge 2005 na yeye asingempinga 2010, ila tatizo ni hawa wanaojiita Wazee wa CCM wa Dodoma ndiyo waliomchuuza na kumhadaa kwamba Mzee watu wa Mtera bado wanakuhitaji, na yeye bila ya kujua kwamba hawa wazee ni wachumia tumbo akaingia kichwakichwa bila kusoma alama za Nyakati na kukana makubaliano aliyoyafanya na Lusinde, sasa kilichompata ndiyo hicho, ni Aibu kwa maana wana CCM wa Mtera hawamtaki so CCM watafanya kosa kubwa sana wakilirudisha jina lake. Namshauri akae pembeni hizi Siasa za Dot Com Haziwezi,
   
 17. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #17
  Aug 9, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Hapana,

  Marais wengi wa marekani kama Rais Clinton, Rais Bush, na Rais Obama pia waliwahi kushindwa uchaguzi mara kadhaa huko nyuma kabla hawajawa maarufu. Tatizo la Mzee Malecela ni kuwa ameshindwa wakati ni mtu maarufu sana tena akiwa ukingoni mwa career yake; mbona aliwahi kushindwa mwaka 1985 lakini leo haikumbukwi tena. Kwa sasa atakuwa na wakati mgumu sana kupata nafasi ya kufuta tukio hilo kutoka kwenye historia yake tena, ingawa huwezi ku rule out kuwa anaweza kuwa na alternative.
   
 18. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #18
  Aug 9, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  Churchill hakuwa mashuhuri na kwenye peak 1945 aliposhindwa?sidhani.....JCM aliposhindwa 1985 ilikuwa CCM tu na hakukuwa na media strength kama sasa...lakini si alirudi 1990 na kuwa Pinda wa wakati huo...replacing Warioba in the process....
   
 19. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #19
  Aug 9, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,276
  Trophy Points: 280
  TingaTingaaa!!anyway mimi ninawaomba CCM wakumbuke kwamba hakuna ukoo ukakosa wazee hivyo wajue nijinsi gani yakumuweka karibu kwani atakuwa mshahuri maana sasahivi hawa vijana wanaoingia katika siasa siyo watu wenye uchungu nanchi yao wala watu wao, wao wanatafuta pesa katika kijiji cha siasa!!!kubali au kataa ukweli ndiyo huo wao wanatizama ni jinsi gani watajinufaisha na matumbo yao tunaona wanavyopigana vikumbo na sikwamasilahi ya wanyonge!!Hivyo kuwepo wazee kama Marecela ni muhimu sana kichama.:shocked:
   
 20. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #20
  Aug 9, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,679
  Likes Received: 21,941
  Trophy Points: 280
  Unamaanisha Dr Slaa? (red)
   
Loading...