Elections 2010 Mzee Malecela akubali matokeo

Nafikiri miaka 10 ijayo tutashuhudia mabadiliko makubwa sana ya kisiasa hapa nchini, wananchi wameanza kuamka!!

Pongezi kwa Mh. Rais Kikwete kwa kuleta mfumo wa kidemokrasia zaidi wa kuchagua wabunge na madiwani ndani ya CCM.

Hivi Kikwete kaleta vipi huu mwamko?
 
Nawapa pole wanaodhani Malecela kashindwa ubunge!! Ameshindwa kura za maoni tu. Anrudi bungeni mapema Nov'10. Shangaa!!


KK hilo kwangu si jipya, ila afadhali mzee tingatinga amefedheheshwa; tunajua mfumo wao, atarudi tu.

Message send anyways.
 
Akirudishwa mjengoni kwa aina yoyyote ile ,hakuna tena maana ya kura za maoni...
 
CCM yamtangaza Lusinde kashinda Mtera,FMES umeyakubali matokeo ?
 

Attachments

  • lusinde 2.jpg
    lusinde 2.jpg
    158.3 KB · Views: 51
Msiomjua huyo mwenye t-shirt ya kijani kwenye picha ya juu ndiye kijana Lusinde,aliyembwaga Mzee Tingatinga kwenye uchaguzi wa kura za maoni-Mtera.

Ikumbukwe kuwa mapema mwaka huu kijanas Lusinde alimuonya Mzee Malecela ili kutunza heshima yake ajitoe mwenyewe kwenye kinyang'anyiro cha Ubunge-Mtera tena akisisitiza kwa kusema kama Mzee Tingatinga atang'ang'ania kugombea itamkumba aibu kubwa.Lkn watu wa upande wa Mzee Malecela walifikia hatua ya kumuita majina yasiyofaa kijana Lusinde;na wengine walimkosea adabu zaidi kwa kumuita kijana Lusinde kama mlevi wa gongo asumbuliwaye na njaa!

Kwa wale waliokejeli kwa majina yasiyofaa kijana Lusinde,je sasa sio wakati wao wa kuja hapa jamvini na kumuomba msamaha?
 
Hata kama mzee Malechela kaanguka lakini si mnasikia kuwa ccm kazi zipo nyingi za kufanya?Wakichukua serikali tu utasikia ni mbunge wa kuteuliwa kama ilivyokuwa kwa KINGUNGE.
 
Hata kama mzee Malechela kaanguka lakini si mnasikia kuwa ccm kazi zipo nyingi za kufanya?Wakichukua serikali tu utasikia ni mbunge wa kuteuliwa kama ilivyokuwa kwa KINGUNGE.
Kazi gani? Wangefanya kazi walau kwa asilimia 10 maendeleo si tungeyaona? Upupu tu!.
 
Ohhhhhhoo Mzee kalamba sakafu jamani? atapata viti maalum kwa vyovyote
 
Back
Top Bottom