Mzee Makamba aibua siri ya Urais 2015


Kazi gani nzuri alofanya? Kwa kuiua CCM? Labda hiyo.... Wewe ni mmoja wa familia hiyo umejidhihirisha mwishoni eti JM..thee tehh eteh ndio maana mzee ameanza kutabiri ili atakaye teuliwa na CCM aambiwe waende Tanga akaoneshwe nguvu za giza na amuombe ampe kazi JM huyo unayemtaka awe rais.. kazi kweli kweli....teh theheh
 
Makamba kwa nini asiwe kama Masishanga aliyetoka hadharani kumuunga mkono Sumaye,kuliko kujificha kwenye vivuli vya kpiga ramli.?
 
Mbona ni mapema mno kuzungumzia uraisi na mbona haikuwa hivi kwa mtangulizi wake.

Hii inaonesha ni jinsi gani watu wanavyowaza kujinufaisha na si kuwanufaisha wananchi na kama tabia hii haitakomeshwa taifa litaingia vitani kwa faida ya wachache huku waliowengi wasijue kinachogombaniwa.

Kama kanisa litaibuka kama ilivyokuwa 2005 na kusema ni chaguo la mungu je wananchi tutasemaje? Maana Chaguo la Mungu kwa maana yao ndo mwendo huu na wanaridhika nao maana walisema ni chaguo la Mungu.

Ndo maana nasema kwa mtindo huu tutapiganishwa kupitia misaada tunayopewa na hawa wanaokuwa baadae kuwa chaguo la mungu ili kufanikisha matakwa ya nafsi zao na jamaa zao.

Pia ni vizuri kujiuliza kanisa linaajenda gani na utawala? Maana huwa linatoa miongozo,matamko na hata maelekelezo juu ya nini kifanyike au ndo hisani ya kutoka kwa chaguo la mungu?
 
Kwani Mungu anapiga kura?

Mimi sijui kwa nini siku za karibuni nikajaribu kuingia kwenye Post zenye heading ya Mungu sipati access? Good Question Mwanakijiji. sababu the other day tuliambiwa so and so ni chaguo la Mungu? does He Vote? Good Question bother.
 
Kwa hiyo siri iliyoibuliwa na Makamba ni kwamba Mungu ndiye anayeamua nani awe Rais?
...Dalili ya kuja kimeo kingine. mnamtana mungu nyie? Mlidai MR. DHAIFU ni chaguo la mungu mbona ZERO!
 
Mimi sijui kwa nini siku za karibuni nikajaribu kuingia kwenye Post zenye heading ya Mungu sipati access? Good Question Mwanakijiji. sababu the other day tuliambiwa so and so ni chaguo la Mungu? does He Vote? Good Question bother.

Inategemea wewe muhusika mwenyewe kuwa, je una amini Mungu yuko, je una dini? dini yako ni ipi? mimi nina dini na katika dini yangu viongozi wote wananapata mamlaka ya kutawala kwa kibali cha Mungu. Mungu akitaka kuwatia adabu nyie kama taifa kwa dhambi zenu ndio atampa kibali asiyekidhi matarajio yenu vinginevyo mtampata anaye kidhi mliyo ya tarajia. wale waliosema ni chaguo la Mungu hawaja kosea hata kidogo kwa mujibu wa imani yangu mie. ila kwa haya maoni ya mzee makamba sikujua kuwa yeye ana kipaji cha utabiri pia.
 
Nani mwenye taarifa za huyu mzee Makamba kuhusu ile Pembe iliyokua kwenye paji la uso kama bado inaendelea kuota atuambie!
 

Kama kweli Mungu ndio anavote in, na ni kweli ameshiriki kuvote in yeyote kati ya Marais wote waliopita, na Marais wengine popote pale duniani, basi na He is a failed god. Lakini as much as I know him, hausiki na huu uchafu unaoendelea hapa. we are responsible for it and the other god we have chosen to save.
 
Inafurahisha, Makamba ameanza rasmi kazi ya marehemu Sheikh Yahaya
 
Mungu hachagui Rais ingekuwa ndiye anaechagua asingetupa hili janga!!

kabisaa!! Mungu anaona maisha ya baadae so kama alijua hii nchi ingekua hivi tulivyo sasa angetupa Rais mwingine ambae ni bora na ana uongozi bora mwaka 2010
 
Definition mpya ya KUJIVUA GAMBA....
CCM bana..

 

Umenifurahisha kwa 1. umeliandika neno Mungu (tofauti na god) kama mimi 2. umekubaliana na mimi bila kunielewa na bila kujua. ni fafanue kidogo labda utanielewa na utaendelea kukubaliana nami. kuwa watu wote tumeumbwa na Mungu kwa mujibu wa imani ya dini yangu. Mungu atampa kibali mtu wa kutuongoza kutokana na majority tunavyo wajibika au tusivyowajibika kwake. kama tunawajibika kwa shetani atampa kibali mtu anayewajibika kwa shetani ili kututia adabu.sasa ni wajibu wa wanaotawaliwa kuomba hekima ya Mungu huyohuyo iliwajue mamlaka inayotawala inamtii shetani au Mungu kwa kuangalia matendo yao wenyewe naya wa watawala wao halafu wachukue hatua. bahati mbaya masuala yanayo husu kumtii na kumuomba Mungu hayana spoon feeding ni juhudi za mtu mmoja mmoja na kwa mambo mengine kama taifa.
 

Hata ukikasirika, ukweli unabaki pale pale na hata yeye mwenyewe moyoni mwake anajua hivyo. The good news ni kwamba Membe anastaafu siasa in 2015 na hahitaji uteuzi wa yeyote yule.
 
Alisema lengo la kujivua gamba halikuwa likiwalenga baadhi ya wanasiasa wachache ndani ya Chama cha Mapinduzi wanaotuhumiwa kwa ufisadi bali ililenga kuwaondoa watu walioonekana kukaa kwa muda mrefu katika safu za uongozi ndani ya chama na kuleta damu changa ili nao waje waongoze wakiwa na mbinu mpya.

Alisema dhana hiyo imepotoshwa na wale wanaoitekeleza wanaitekeleza kwa malengo tofauti.


hiyo kauli hapo juu ndo anapochekesha kwelikweli!!!!

ha ha haaaa!!!muongo utamjua tu. huyu mzee ndo walewale tu wenye dhambi ya kula nyama ya mtu. hana jipya, angepumzika tu anazidi kujidhalilisha bure.

hata Nyerere tuliyemwamini sana aliishia kutuchagulia FISADI Mkapa.
Rais tutaamua sisi wenyewe watanzania na sio huyu mzee anayeweweseka!!!!

Aggggggggrrrrrrrrrhhhhhhhhh!!!!!!!!!!!
 
Makamba, JK,Nape, na baadhi wanaofanana nao kitabia ndo walioifikisha CCM hapo ilipo na kusaidia kuifikisha CDM hapa ilipo sitegemei leo hii Makamba awe na point za maana za kuongea kuhusu na Mstakari wa Chama chake na Taifa hili cha muhimu akae kimya ili angalau asahaulike asije ingizwa kwenye kashfa za ufisadi bure maana ndani ya CCM hakuna msafi
 

Mukama, Chiligati na Msekwa nao ni damu changa...ccm kwa sarakasi wameshindikana ..wanasema wasiyoamini na kufanya wasiyosema.....kaburi li karibu msihangaike sana Mwenyezi Mungu atawapumzisha kwa amani
 

mwakyembe alikua timu mwandosya 2005
 
Hata ukikasirika, ukweli unabaki pale pale na hata yeye mwenyewe moyoni mwake anajua hivyo. The good news ni kwamba Membe anastaafu siasa in 2015 na hahitaji uteuzi wa yeyote yule.

membe atafanya nini akistaafu? phd ilki awe mwalimu au?
 
Tunahitaji hii axis of power ichukue nchi 2015...Mwandosya (Rais) Sitta, (Pm), Magufuli (ujenzi na uchukuzi hamna kutenganisha hivi vitu) Mwakyembe (ardhi na maendeleo mijini aweke sawa wizara ngumu hii) Sospeter aendelee na nishati, fedha ateuliwe utouh(hamna tena misamaha ya kodi kijinga jinga) Kilimo na elimu ni wizara muhimu Prof anajua vichwa vyake ataviweka hapo.... hii ni timu ya ushindi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…