Kuna aina nyingi za dua. Mifano, dua ya kuku dhidi ya mwewe, dua ya panya dhidi ya paka, dua ya swala dhidi ya Chui, dua ya Simba dhidi ya Yanga, dua ya Chadema dhidi ya ACT, na dua ya Mmawia dhidi ya uimara wa Tanzania kiuchumi na kiusalama. Pia dua ya Mmawia ni dhidi ya ustawi wa tamaduni za mtanzania, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mengine mengi kama hayo.
Kwa ufupi dua ya Mmawia inaeleza yeye na wenzake wametuwekea nini kwenye 'maficho' yao sisi wananchi tunaopenda na tunataka Tanzania iendelee kuwepo, tofauti na Lissu anayewaaminisha akina Mmawia kuwa Tanzania si lazima kuwepo bali dunia yake Lissu ndiyo iendelee kuwepo.
Simba kula nyama pekee haimaanishi swala anaonewa kwakua ni kudra za Maulana tu hizo na MAAMUZI yake.
Nguruwe kula kila kitu Ila naye analiwa pia na hivyo ndizo hekima za muumba, ukiyawaza hayo hupatwi na tashwishwi za mbona yeye sijui imepanda ikashuka.
Hizi ndio tunaziita tamaa mtu ushakula bata mpka kuku wakakuonea wivu ushazunguuuka Dunia mpaka ukakinai ni wakati wa kula pensheni atulie leo unaenda kudanganya huko tena yaani kutoka first lady mpaka viti maalum sasa hivi tunawaona wakikuna mpaka nazi kuutaka ubunge sasa kama sio ulafi ni nini na mimi naona inategemea na maeneo wanapoomba hizo kura wananchi wa maeneo hayo wapoje kiuelewa huyu angekuwa kwenye ile mikoa inayojitambua mbona asubuhi tu angeangukia pua
Huyu na mwenzake mama Mkapa waliunda viNGO vya kukusanya mamilioni lakini huyu mama bado haja tosheka. Wana takiwa watupe mrejesho wa mamilioni waliyokuwa wana kudanya kupitia WAMA - Salma na EOTF -Anna
Mke wa raisi anatunzwa na kodi zetu mpaka ukamilifu wa maisha yake, ana haja gani ya kurudi kukaa vumbini kuomba kura? Mbona mama Nyerere, Mama Siti na mama Mkapa hawakurudi kuwa wabunge?