Kwako Mama Salma Kikwete; Naamini ulishastaafu hivyo haikustahili kwako kuupokea ubunge

Uzalendo Wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
1,010
2,000
KWAKO MHESH MAMA SALMA KIKWETE - NAAMINI ULISHASTAAFU HIVYO HAIKUSTAHILI KWAKO KUUPOKEA UBUNGE!

Kwako Mhesh Mama Salma Kikwete First Lady mstaafu awamu ya nne!

Kwa maoni yangu naona hukupashwa kupokea uteuzi wala kuamua kugombea Ubunge

Siyo kwamba huna haki Kikatiba ila naona kuwa unayo taswira ya kustaafu zaidi kama ilivyo kwa Mwenza wako aliyehudumu akiwa Rais wa Tanzania.

Kwa maoni yangu nyote wawili mlistaafu mwaka 2015 baada ya kutumikia ipasavyo nafasi zenu.

Ulihudumu vema na hakika Watanzania walikupenda ukiwa First Lady kwa miaka kumi (2005 - 2015).

Muda huo unatosha sana na ninaamini kuwa huu ni wakati muafaka kwako kupumzika ukiwa ilivyo kwa Mzee wetu Jakaya Kikwete

Itapendeza na itakuwa vema ukiachana na Ubunge ulionao ili kutoa fursa kwa wengine na badala yake ukapumzike Msoga.

Kuwepo kwako Bungeni kunaweza kuleta taswira isiyo nzuri ukizingatia nafasi yako ya awali.

Nitoe mfano mdogo, ikitokea unaikosoa Serikali iliyopo madarakani kwa nafasi yako ya Ubunge, je utazuiaje hisia kuwa unafanya hivyo kwa niaba ya mwenza wako?

Je unawezaje kujitofautisha na mwenza wako kwenye masuala au misimamo ya kisiasa?

Niombe Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania litunge sheria maalumu ili kutoa mwongozo wa maisha ya kisiasa kwa waliowahi kuwa First Ladies Wastaafu
 

Jasmoni Tegga

JF-Expert Member
Oct 28, 2020
4,518
2,000
Anawatumikia wananchi wake, sawa? Halafu, usije kudhani kuwa kazi ya Bunge ni kuikosoa serikali tu wakati wote. Kwani wakati akiwa Mbunge watu wasingeweza kuamini alifanya hivyo kwa mtazamo wa mumewe? Unaitaka nafasi hiyo? Kagombeeeeeeee!!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom