Mzee Kawawa afariki dunia!

BURIANI MZEE KAWAWA
KIFO KIMEMPATA KATIKA HOSPITALI IPI ?
TARATIBU ZA MAZISHI ZINAKUAJE MAANA WENZETU HUWA HAWALAZI MAITI

QUOTE=Halisi;721891]Kumaliza mwaka ni jambo ZITO sana. MUNGU ashukuriwe, maana ndiye mwenye uwezo wa kupanga na kupangua. Sote tuombe Mungu.. Mengine zaidi baadaye... INASIKITISHA[/QUOTE]
 
R.I.P Simba wa Vita. Mwenyezimungu akupe makazi bora katika Pepo yake. INNA LILLAHI WAINA ILLAIHI RAJIUNA.
 
Ni profile nzuri lakini sababu za kuitwa simba wa vita ni kipindi cha miaka ya late 50s akiwa labour unionist wakati wa mapambano ya siasa/hali bora za wafanyakazi hivyo ujasiri wake kukabili wakoloni ulimpa hiyo hadhi
 
Poleni sana wafiwa.
Natamani angefanya kitu / angetoa tamko wakati wa uhai wake siku za mwisho kuhusu mustakabali wa nchi yetu, basi tena. Poleni sana
 
Eeeeeeweeeee MUNGU wa IBRAHIM, ISSAC na YAKOBO Jina Lako liimidiwe na litukuzwee Milele AMINA
 
RIP Kawawa! Msalimie mpendwa wetu Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere mwambie Taifa alilolipigania linatafunwa na watu wachache. Chama alichokiongoza ili kiwe chama cha wakulima na wafanyakazi na nuru ya mafanikio katika ukombozi wa watanzania kiuchumi, ndo kwanza kimekumbatia matajiri wa kifisadi!!

Amen
 
Mungu ampumzishe kwa amani kamanda wa vita, Simba sports mwenzetu,mwana CCM na Mtanzania mwenzetu, Mungu amempumzisha katika staili ile ile ya Mwalimu JK, alimuacha Mkapa akijiandaa kwa term ya pili na Simba wa vita RMK amemuacha Jakaya akijiandaa na term ya pili, mbele yake, nyuma yetu. Jina Bwana lihimidiwe. Mungu ibariki Tanzania
 

Mungu awape faraja na uvumifivu familia ya marehemu maana sote tuko safarini.
 

MUNGU atakupokea katika ufalme wake Mzee wetu na shujaa wa kipekee. Msalimie sana Mwalimu.

Wana JF twende mbele zaidi na kufikiria ni kwa namna gani bora tutakuwa tukimkumbuka kila mwaka na kumuenzi SIMBA WA VITA.
 
 
another African legend has gone..ooh Lord, may his soul rest in peace! we r behind u
 
R.I.P jirani yangu kule madale...mungu akupe mapumziko ya milele na amani ya bwana iwe nawe..

Wafiwa poleni sana na mungu awatie nguvu sana na ujasiri katika kipindi hiki kigumu kabisa kupata kupita katika maisha yenu...

Rafiki Yangu Vita Kawawa mungu akupe subira na nguvu..

Amen
 
ooooooooooooooooooooooooooooooooh God!simba wa vita!tutakukumbuka daima,ulikuwa icon wa siasa za Tanganyika na Tanzania.oh,R.I.P
 
Poleni sana wafiwa mungu atawabariki wakati huu wa msiba
 
Kweli watu wazuri hawaishi muda mrefu,
Mzee wetu 83 miaka ni kama siku na sio kufuru,
Ni kutokana na mazuri mengi yaliyokupa umaarufu,
Hukusita kukemea viongozi na wakwapuaji sarafu,
Taarifa za msiba zimeufanya mwili wangu uka dhoofu.

RADICAL endelea machozi yananitoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…