Mkumbwa Jr
JF-Expert Member
- Mar 23, 2016
- 2,624
- 3,653
Mapema jana Mh. Jakaya Kikwete akiwa Chuo kikuu cha Daresaalam(UDSM) alilalamika mbele ya Mh. Raisi kwamba chuo hicho kina changamoto ya miundombinu mibovu kama barabara, mabweni nk
Nimeshangaa jana mzee Jakaya kumuomba Mh.Rais asaidie changamoto hizo kwani ukweli nikwamba wanaopata malazi ni 30% ya wanachuo wote.
Nakuuliza maswali haya Mh.Jakaya
Je,wewe ulichukua hatua gani kabla hujaondoka mapema juzi tu ?
Je kama akiweza kutatua changamoto hizo mapema mno utajisikiaje kama raia wa kawaida tukisahau siasa za wanasiasa?
Ni kwanini umbebeshe mwenzako zigo ambalo wewe hukulijaribu kwa sababu uzijuazo wewe?
Je unawezaje kukataa kwamba wewe sio miongoni mwa wazee wanaompa uzito mzito Mh Raisi wa JMT kama anavyodai?
Kwawale wasioifahamu UDSM ni kwamba ni chafu kutokana na uwingi wa wanachuo ikilinganishwa na miundombinu iliyopo. Mabwenini vyoo ni vibovu na mapungufu mengine.
Mzee Jakaya anajua kabisa kwamba UDSM ina maeneo ya wazi makubwa mno kuliko yale yaliyokwisha jengwa maana kuna pori kubwa kama hifadhi lakini wanafunzi hawana pakulala eti kisa hamna mabweni.
Ushauri wangu
Fedha nyingi mnazotumia kuwapeleka JKT wahitimu wa kidato cha sita, fedha za kugharamia mbio za mwenge nk zielekezwe kwenye ujenzi wa mabweni.
Wale waliohusika na mpango haramu wa kuratibu zoezi la wafanyakazi hewa wakiwemo WAKURUGENZI NA WAKUU WA IDARA ,wachunguzwe, wakamatwe, wapelekwe mahakamani na wakafilisiwe kufidia fedha zetu ili zijenge mabweni.
Ni bora wafilisiwe waachwe wawe huru kuliko kuwa kama yale ya Mgonja na mtani wake Mramba MAANA HAYANA TIJA KWA TAIFA.
Ni mawazo yangu naomba kuwasilisha