Mzee Jakaya ni mapema mno

Mzee Jakaya ni mapema mno

Mnamnyonga kwa lipi-alipokuwa raisi Tanzania yote ilikuwa jukumu lake, lakini sasa amevaa viatu vya Mkuu wa Chuo Cha Dar hivyo ni haki yake kumobilize fedha kujenga chuo hicho. Cha kufurahisha JPM alisema UDSM ndio aliposomea hivyo atakisaidia chuo hicho. Wasi wasi wangu asije akasahau hivi vyuo vingine vya umma kwani changa moto ya miundo mbinu na walimu ni kubwa mno.
Soma vizuri nilichoandika kule juu, inawezekana tunatetea kitu kimoja, ila sababu ya kutosoma vizuri kwanza alichoandika mtu, ndipo umjibu.
 
Soma vizuri nilichoandika kule juu, inawezekana tunatetea kitu kimoja, ila sababu ya kutosoma vizuri kwanza alichoandika mtu, ndipo umjibu.
Mkuu niliisoma vizuri sana nami nilikuwa nakuunga mkono kusisitizia tu ulichoelezea kwa njia tofauti. Sorry kama nimekukwaza.
 
Mkuu niliisoma vizuri sana nami nilikuwa nakuunga mkono kusisitizia tu ulichoelezea kwa njia tofauti. Sorry kama nimekukwaza.
Hujanikwaza mkubwa, sikukuelewa samahani, Hapa kumkwaza mtu labda umshambulie yeye binafsi au jamii anayotoka, vinginevyo tunapeana changamoto, kuhabarishana, kuelimishana kutoa Mawazo (Stress).
 
W
Mapema jana Mh. Jakaya Kikwete akiwa Chuo kikuu cha Daresaalam(UDSM) alilalamika mbele ya Mh. Raisi kwamba chuo hicho kina changamoto ya miundombinu mibovu kama barabara, mabweni nk

Nimeshangaa jana mzee Jakaya kumuomba Mh.Rais asaidie changamoto hizo kwani ukweli nikwamba wanaopata malazi ni 30% ya wanachuo wote.

Nakuuliza maswali haya Mh.Jakaya

Je,wewe ulichukua hatua gani kabla hujaondoka mapema juzi tu ?
Je kama akiweza kutatua changamoto hizo mapema mno utajisikiaje kama raia wa kawaida tukisahau siasa za wanasiasa?
Ni kwanini umbebeshe mwenzako zigo ambalo wewe hukulijaribu kwa sababu uzijuazo wewe?

Je unawezaje kukataa kwamba wewe sio miongoni mwa wazee wanaompa uzito mzito Mh Raisi wa JMT kama anavyodai?

Kwawale wasioifahamu UDSM ni kwamba ni chafu kutokana na uwingi wa wanachuo ikilinganishwa na miundombinu iliyopo. Mabwenini vyoo ni vibovu na mapungufu mengine.

Mzee Jakaya anajua kabisa kwamba UDSM ina maeneo ya wazi makubwa mno kuliko yale yaliyokwisha jengwa maana kuna pori kubwa kama hifadhi lakini wanafunzi hawana pakulala eti kisa hamna mabweni.

Ushauri wangu
Fedha nyingi mnazotumia kuwapeleka JKT wahitimu wa kidato cha sita, fedha za kugharamia mbio za mwenge nk zielekezwe kwenye ujenzi wa mabweni.

Wale waliohusika na mpango haramu wa kuratibu zoezi la wafanyakazi hewa wakiwemo WAKURUGENZI NA WAKUU WA IDARA ,wachunguzwe, wakamatwe, wapelekwe mahakamani na wakafilisiwe kufidia fedha zetu ili zijenge mabweni.

Ni bora wafilisiwe waachwe wawe huru kuliko kuwa kama yale ya Mgonja na mtani wake Mramba MAANA HAYANA TIJA KWA TAIFA.

Ni mawazo yangu naomba kuwasilisha
Well said
 
vituko vya rais mstaafu wa aina ya nne unaweza kutengeneza filamu ya aina yake kwani huyu ndio alisababisha kila mtu akajiona anafaa kuwa rais yeye muda mwingi alitumia angani badala ya kushugurikia matatizo ya msingi ya wananchi haya ndio matokeo yake anajiumbua mwenyewe wengine ni wale waliokuwa mawaziri kwenye serikali yake ambaosasa hawana nafasi nao kila mara wanalalamika kana kwamba hawakuwahi kuwa kwenye nafasi za kufanya maamuzi akiwemo Mary nagu na yule aliyekuwa waziri wa fedha
 
Una hoja mtoa mada! Analalamika nini,wakati yeye ndio alkuwa mwenye wajibu wa kuondoa changamoto hizo
 
Back
Top Bottom