Mwita Maranya
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 10,565
- 7,988
Salam Wana JF,
Bila kutarajia asubuhi hii nimejikuta nalazimika kuitazama television ya TBC1 kwakua mazingira niliyokuwepo ndio channel pekee ya nyumbani inayoonekana.
Mtangazaji wa TBC1 amemkaribisha studio mzee Farijala ambaye ni kada wa CCM. Katika mazungumzo yake amejikita katika kumshambulia aliyekuwa Makamu Mkuu wa chuo kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT) cha Mwanza Dkt. Charles Kitima, kwamba pamoja na kuwa amesomeshwa na CCM lakini amekuwa akiikisoa sana na kuilaumu serikali ya CCM.
Mzee huyo anadai kuwa anamfahamu sana Dkt. Kitima kwamba ametoka katika familia duni sana alikuwa akivaa kaniki lakini leo hii amesahau fadhila ya serikali ya CCM.
Pia amezungumzia wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu kutofanya siasa kwa madai kuwa wako vyuoni kusoma na si kufanya siasa akitolea mifano vyuo vya SAUT TABORA NA SAUT MWANZA.