Mzee Farijala na STAR TV | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzee Farijala na STAR TV

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kimbojo, Sep 23, 2012.

 1. Kimbojo

  Kimbojo JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2012
  Joined: Apr 12, 2009
  Messages: 387
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Leo asubuhi Mzee Farijala ameifagilia Star TV kwa kuamini kwamba STAR TV wako upande wao (CCM) ndo maana anaalikwa mara kwa mara kwenye vipindi vyao na kuichana ITV hadharani kuwa inatumika na wapinzani kwa.
  Hii imedhihirisha kwamba huyu mzee huwa anahudhuria vipindi ili kukitetea chama chake na sio maslahi ya Taifa. kuna kipindi alialikwa wakati wa mgomo wa madaktari akawatukana madaktari kwa kuwaita ni wala rushwa wakubwa( wanapokea rushwa kwa wagonjwa) na leo kichana ITV kupitia STAR TV. Hoja yangu hapa ni kwamba si dhani kama huyu mzee ana sifa za kualikwa kujadili mambo yahusuyo nchi kwa ujumla wake, STAR TV wapime uzito wa mada na waangalie watu wa wakushiriki katika mada husika. Huyu Mzee anafaa kualikwa kwenye vikao vya fitna na majungu ndani ya chama chake. La sivyo mkiendelea kumualika mtakidharaulisha kituo chenu/chetu na pengine mtaendelea kuomba radhi kwa wengine ambao wataendelea kudhalilishwa kupita kweu STAR TV kama Yahaya ulivyoomba radhi kwa ITV .
   
 2. K

  Kolero JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2012
  Joined: Apr 11, 2010
  Messages: 493
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mkuu asante sana kwa taarifa, huyo Mzee ni nani hapa Tanzania? Kama ni muasisi wa TANU na ana imani katika yale yaliyoasisiwa na TANU leo hii hawezi kusimamam mbele ya luninga na kuitetea ccm labda kama analipwa posho. Kuhusu kupondea vyombo vya habari vingine, hayao ni mawazo yaliyomo katika watu wenye mwelekeo wa chama kimoja na hasa Ukomunisti na Usoshalisti. Tatizo la watu wa aina hiyo, hawajazoea kukosolewa, kurekebishwa, na hata kupokea wazo mbadala, kumbe kama unavyoona wanaoukosoa upinzani wengi wana mawazo ya chama kimoja na ukomunisti wa zamani. Wazo la STAR TV kunagalia ni nani anapaswa kualikwa ni muhimu sana kwa nyakati hizi, kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi pia uaminika wa chombo cha habari chenyewe kwa watu. Nadhani watalifanyia kazi na kuepukana na kualika watu wanaojipigia debe ili kupewa posho na kupigiwa simu na macheameni wao kupongezwa kwa pumba wanazoongea. Hali itaeleweka, zama hizi si za tu kujiona mzee bali uzee wako una toa tija gani kwa taifa. Tushachoka na kupotezwa sasa tunataka kuijenga nchi yetu itakayotufaidisha wote na siyo jamii ya aina hiyo teule.
   
 3. n

  nndondo JF-Expert Member

  #3
  Sep 23, 2012
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 535
  Trophy Points: 280
  Acha hao STAR TV yawakumbe wakome, ni kweli hicho ndio wanachokifanya japo huyo farijala kakosea manake huko ITV wenyewe wako busy pia kujikomba kwa CCM, labda tusema STAR wanajikomba zaidi kwa hiyo ITV wamepigtwa na style. Lakini yahaha hana haja ya kuomba radhi, kwa ni kweli kwamba eti star hawaruhusiwi kurusha bahari za Mbunge Kiwia aliyembwaga Dialo?
   
Loading...