Mzee Cleopa Msuya naye ataka Katiba Mpya

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,600
217,996
Waziri Mkuu mstaafu Cleopa Msuya, leo amefika kwenye Kikosi Kazi cha Rais cha kukusanya maoni yanayohusu Katiba Mpya, ambapo mzee huyo hakumung'unya maneno, amewapasulia wazi wajumbe wa kikosi kazi hicho kwamba Katiba Mpya ni sasa hivi.

Mzee Msuya amesema kwamba ifike wakati sasa tuhitimishe jambo hili ili tuendelee na mambo mengine, badala ya kila mwaka kuzungumzia jambo hilohilo tu.

Chanzo: Mwananchi

Ujumbe: Kama hawa wazee wamechoshwa na danadana hizi za akina pinda na mukandala, wewe ni nani hata upinge Katiba Mpya
 
WAZEE wanapenda uzee mzuri, wakitengeneza na Mungu.

Tupate KATIBA mpya Ili tuondokane na Utumwa Kutoka MKOLONI mweusi.

RASIMU alosimamia Judge WARIOBA irudi mezani mjadala uanzie hapo.

Ameeeeen.
Hawa hawa ndo walikua wakisema nchi haina umuhimu wa katiba mpya zaidi ya madaraja na midege. Kwao material thing ilikua hitaji kuu la maisha kuliko vitu vya msingi kama katiba!!

Kwakua leo ni Samia wamebadili kauli... hii nchi itapona pale kizazi chote cha kijamaa kikipotea maana ujamaa uliwafanya watu wawe wanafiki, uliwafanya watu wawe mithili ya minyoo maana minyoo huwa yamwisho kufa so walijiona wanastahili uhai kuliko wengine mbele ya yule kichaa.
 
Katiba ya KKKT imeshindwa kutafsirika Mbeya!

Tusisahau na hilo

Hawa hawa ndo walikua wakisema nchi haina umuhimu wa katiba mpya zaidi ya madaraja na midege. Kwao material thing ilikua hitaji kuu la maisha kuliko vitu vya msingi kama katiba!!

Kwakua leo ni Samia wamebadili kauli... hii nchi itapona pale kizazi chote cha kijamaa kikipotea maana ujamaa uliwafanya watu wawe wanafiki, uliwafanya watu wawe mithili ya minyoo maana minyoo huwa yamwisho kufa so walijiona wanastahili uhai kuliko wengine mbele ya yule kichaa.
Akitubu husamehewa. Apumzike Kwa amani Mzee.
 
..Mwenyekiti wa Ccm amefungua akili zao.

..kabla Ccm haijawaruhusu walikuwa kimya.
Siku zote nasemaga ujamaa ni ushetani, wajamaa hawajali shida za wengine midhali wao wanashiba. Wajamaa hawaogopi madhila yawapatayo wengine kwakua wao ni salama. Ni minyoo ambayo hukaa tumboni mwa mwenye njaa ikifaidi utumbo... haijali maana yenyewe huwa yamwisho kufa.

No wonder akina Pinda walioona Magufuli atawale milele wao tena leo wanaona kuna umuhimu wa katiba mpya.

Ujamaa wa Nyerere na CCM umezaa watu wa hovyo sana kiasi cha haki zao kuchukulia kama fadhila.
 
Back
Top Bottom