johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,937
- 141,908
Aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Katiba aka Tume ya Warioba mzee Butiku amesema Tanzania haihitaji katiba mpya kwa sababu Katiba ipo na misingi yake bado ni ile ile ila kinachohitajika ni kuifanyia marekebisho hususani kwenye Madaraka ya Rais na Bunge
Mzee Butiku amesema hata wao katika Tume ya Katiba iliyoundwa na mzee Kikwete walitengeneza rasimu ambayo misingi yake ni ile ile ya Katiba ya sasa.
Mzee Butiku anasisitiza kuwa taifa hili liliasisiwa na baba wa taifa Mwalimu Nyerere na wenzake na katiba waliyotengeneza haikuwa ya Kambarage bali ya Wananchi wa Tanzania
Misingi ya Katiba ni ile ile sasa hiyo katiba mpya inatoka wapi? ameuliza Butiku.
Chanzo: ITV Dakika 45