Mzee Butiku: Tume ya Warioba ilifanyia Marekebisho Katiba iliyopo haikuja na Katiba mpya, taifa hili liliasisiwa na Nyerere

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,891
141,824
Aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Katiba aka Tume ya Warioba mzee Butiku amesema Tanzania haihitaji katiba mpya kwa sababu Katiba ipo na misingi yake bado ni ile ile ila kinachohitajika ni kuifanyia marekebisho hususani kwenye Madaraka ya Rais na Bunge

Mzee Butiku amesema hata wao katika Tume ya Katiba iliyoundwa na mzee Kikwete walitengeneza rasimu ambayo misingi yake ni ile ile ya Katiba ya sasa.

Mzee Butiku anasisitiza kuwa taifa hili liliasisiwa na baba wa taifa Mwalimu Nyerere na wenzake na katiba waliyotengeneza haikuwa ya Kambarage bali ya Wananchi wa Tanzania

Misingi ya Katiba ni ile ile sasa hiyo katiba mpya inatoka wapi? ameuliza Butiku.

Chanzo: ITV Dakika 45
 
Mzee Butiku kazeeka huyu. Asamehewe tu

Mara katiba ya sasa inahitaji marekebisho ya madaraka ya rais, mara katiba mpya haihitakiki. Tumwelewe vipi? Shubamiti!
 
Kuna wakati ana akili kuna wakati akili zake hazisomi!
Katiba iliyoletwa na Kambarage haikuwa na baraka za wananchi. Na huo ndo msingi wa matatizo ya Tanzania.
 
Inshu katiba hii haitoshelezi..suala la muungano ni makangamyiko..tuwe na serikali moja au tatu..huu upuuzi wa serikali moja ya Tanganyika iliyojivika koti la muungano ifike wakati livuliwe.

Madaraka ya rais ni makubwa sana mpaka wengine wanajiona miungu watu..

Kuwepo na true separation of power katika mihimili ya nchi..sio hii danganya toto iliyopo.

Tume ya uchaguzi..wajumbe watokane na wananchi sio vibaraka wa ccm.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom